Pamoja na JK kuhutubia Nchi juuu ya Rasimu kumbe watanzania wanataka Serikali ya Tanganyika ?

Tafiti finyu hizo, wanaotaka Tanganyika waulize sababu ya msingi hawana. Nn wanakosa Tanzania mpaka wadai Tanganyika? Na Tanganyika ni serikali iliyooachwa na mkoloni je wanataka mkoloni? ,

Wewe Mjinga wa karne tambua Kuwa Ukoloni ni Unyonyaji Yaani Wachache kuwanyonya wengi . Mfano ni huu hapa Tanganyika sasa ni koloni la Zanzibar Maana wanainyonya Tanganyika ambayo haijapata uhuru wake lakini inatumia pesa zake kuwalea Zanzibar wasio na shukran Maana wanakula wakishiba wanaanza Ulalamishi ili kuwapumbaza watanganyika wasijue Kuwa Zanzibar ni Mkoloni mambo Leo .
 
binafsi sitaki serikali 2 na wala sitaki serikali 3..nataka serikali moja tuu ,na kama hilo haliwezekani basi wavunje tu muungano kieleweke.
 
Hili jina Tanzania ni jina lililotoka Tanganyika hivyo siku Muungano Ukifariki na Zanzibar kwenda zao kwa waarabu Tanganyika italitumia jina la Tanzania Kama a.k.a ili kuondoa usumbufu wa kusajili jina pale UN tambueni jina Tanzania ni Mali ya watanganyika hata muungano Ukifariki tanganyika inaweza kulitumia jina la Tanzania bila swali kwani Zanzibar hawakuja na jina walikuja na mchanga kwa ajili ya kuchanganya udongo wa bara na visiwani tu
 
Nilipenda hii ya aliyotoa Waryoba kuwa "Waasisis walituanchia nchi moja yenye serikali mbili, hawakutuachia nchi mbili zenye serikali mbili". Kuna mabadiliko mengi yamefanyika bila hata kuangalia Katiba na mwisho tukajikuta na nchi mbili zenye serikali mbili ambamo muudo wa serikali mbili haufanyi kazi tena.
 
binafsi sitaki serikali 2 na wala sitaki serikali 3..nataka serikali moja tuu ,na kama hilo haliwezekani basi wavunje tu muungano kieleweke.

Hayo Ndio yalikuwa malengo ya Nyerere sasa wamekwenda kinyume Ndio Maana muungano umekuwa wa ajabu hausomeki Zanzibar sasa ni Mkoloni wa Tanganyika huku Tanganyika akihaha kuubembeleza muungano kwa pesa nyingi . ! Zanzibar yeye anachuma kisha anajiimarisha kisha atimukie kwa waarabu. Watanganyika zindukeni tuukatae Ukoloni wa Zanzibar kwa Tanganyika
 
Wadau
Usiku kwenye ITV katika maoni imeonyesha wazi kwamba Watanzania wako na Warioba . Katika kufanya utafiti huo kwenye ITV watanzania walio hojiwa 61% wanasema wanataka Tanganyika na huu ni ujumbe tosha kwamba Kikwere is desparate na watanzania wamesha amka. Hakuona kosa la zanzibar kuuvunja muungano sasa mjadala umeanza upya na kwa hakika CCM hawatafanikiwa kuwaburuza watanzania . CCM na JK wamehaha lakini sasa ona watanzana na maoni japokuwa CCM na JK hawayathamini maamuzi yao wananchi .Je na wewe umeona hilo kwenye ITV usiku huu na unasemaje ?

Tusishangae wakaja na hoja kwamba wananchi wanaotazama taarifa ya habari ni wachache sana ikilinganishwa na wananchi wanaotazama kipindi cha "original comedy", kwahiyo swali lingeulizwa kwa watazamaji wa original comedy, matokeo hayo ndiyo yangeakisi maoni ya wananchi walio wengi;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Jk amewaangusha watanzania wengi sana, amewakatisha tamaa sana, ameunda tume, imekula mapesa mengi, ameteua wajumbe wabunge maalum la katiba na wanakula 300000 kwa siku, baadae anakuja kuwaamulia nini wafanye, huu ni zaidi ya ufisadi na uhujumu kwa taifa letu! Afadhali amalize utawala wake haraka!
 
Mkuu Lunyungu, endelea kujifariji na matumaini hewa ya kukufuliwa kwa marehemu Tanganyika!. Watakao amua mfumo gani wa kufuata, sio hao waliohojiwa na ITV, wala sio Watanzania milioni 45!, bali ni wale wateule 600, kati yao ASILIMIA 80% yaani wajumbe zaidi ya 500 ni CCM!. Matokeo ya mwisho ni kuendelea kwa serikali mbili!.
Nimeshauri hapa, tuwahamasishe Watanzania wote waikubali katiba hiyo ya serikali mbili![h=3]Mchakato Huu wa Katiba, ni Umasikini Wetu!,[/h]Pasco
Serikali tatu itaharibu mkakati wa Mungu wetu Lowasa.
 
Tusishangae kwamba wananchi wanaotazama taarifa ya habari ni wachache sana ikilinganishwa na wananchi wanaotazama kipindi cha "original comedy"
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
This may sound like a joke!, ila viewership survey, imethibitisha ni kweli watazamaji wanaotazama original comedy ni wengi kuliko wanaongalia taarifa ya habari, kufuatia hali hii, note, siku ya comedy, kila kituo pia kinaweka comedy yake wakati ule ule!.

Ila sio kwenye comedy tuu, hata kwenye magazeti, wasomaji wa magazeti ya udaku ndio wengi zaidi!.
Sisi ndio Watanzania wenyewe, na haya "comedy, udaku" ndio mahitaji yetu muhimu ya info!.
Pasco
 
Tafiti finyu hizo, wanaotaka Tanganyika waulize sababu ya msingi hawana. Nn wanakosa Tanzania mpaka wadai Tanganyika? Na Tanganyika ni serikali iliyooachwa na mkoloni je wanataka mkoloni? ,

Hujui unachokisema. Tanganyika ilipata uhuru wake na kuunda serikali ya jamhuri huru iliyodumu hadi 25 Apr 1964. Kwani kwa mawazo yako, walioitaka Zanzibar yao sababu zao ni za msingi au si za msingi? Mimi nitakutajia sababu yangu moja ya msingi ya kuitaka Tanganyika yangu: ituwezeshe kutumia rasilmali za Tanganyika kwa maendeleo ya Tanganyika, tofauti na sasa ambapo zinatumika pia kutunza nchi nyingine ya Zanzibar bila watanganyika kufaidi chochote. Hizi wizara zinazoitwa "za muungano", gharama zake zote zinatokana na bajeti zinazopitishwa Dodoma na kututoza kodi sisi watanganyika, lakini zinatumikia watu wengine kwenye nchi yao!
 
This may sound like a joke!, ila viewership survey, imethibitisha ni kweli watazamaji wanaotazama original comedy ni wengi kuliko wanaongalia taarifa ya habari, kufuatia hali hii, note, siku ya comedy, kila kituo pia kinaweka comedy yake wakati ule ule!.

Ila sio kwenye comedy tuu, hata kwenye magazeti, wasomaji wa magazeti ya udaku ndio wengi zaidi!.
Sisi ndio Watanzania wenyewe, na haya "comedy, udaku" ndio mahitaji yetu muhimu ya info!.
Pasco

Sababu comedy inagusa maisha ya watu kuliko taarifa ya habari sasa unadhani wananchi wanataka kujua nani yuko wapi anafungua jengo sijui barabara au nani kakamatwa kwa maandamano au kujaziwa habari za kampeni uchaguzi mdogo!!!!!

Amkeni watu wa media comedy ni jina tu ila wako serious na maisha ya watu ndio maana wanapata audience kubwa!!!!!!

It is the content that counts!!!!! Not the mere label
 
Mimi sioni nini nitafaidikan kwa kupata Tanganyika, sanasana itaabidi tuanze upya kuitangaza Tanganyika hadi ifahamike kimataifa, Kilicho niudhi kwa Kikwete ni kuchambua rasimu ya katiba badala ya kuhutubia Bunge la katiba katika mambo ya msingi, angeacha wajumbe waichambue wenyewe, vinginevyo na yeye akawe mjumbe

Kwa mara hii umetoA point kubwa sana AKAKENDE kama siyo AKAGAYA.rais wetu angewaachia wabunge wafanye kazi yao.mimi naona kitendo cha rais kuwa msemaji wa bunge hii kitu imeibua hisia kali kwa watanzania juu ya kwanini serikali haitaki hizo serikali 3.
 
Mimi napenda kuuliza hapa kwa wale wa CCM wanaomnanga Warioba . Je Kikwete alipata kura ngapi mwaka 2010 kuwa rais hadi muda huu ? Watanzania tulikuwa zaidi ya 30mn lakini alishinda jwa 5mn ina maana ni watu wa Dar na kuongeza mikoa michache lakini ni Legit president mbona hakuhoji kura hizo ?
 
Sababu zisizo za msingi kwako, ni za msingi kwa mtu mwingine and vice versa ! Wewe unazoona ni za msingi, kuna wengine wanaziona ni rubbish !

At the end of the day, wanachokitaka wengi, ndicho kitakachokuwa chetu sote.....Kama waTz wengi wanataka serikali ya Tanganyika iwepo, hakuna mtu yeyote anaweza kulizuia hilo !

Tafiti finyu hizo, wanaotaka Tanganyika waulize sababu ya msingi hawana. Nn wanakosa Tanzania mpaka wadai Tanganyika? Na Tanganyika ni serikali iliyooachwa na mkoloni je wanataka mkoloni? ,
 
BILA KUIASI SERIKALI YA CCM NA KUANZA KUITAFUTA Tanganyika KWA MTUTU WA Bunduki KAMWE HATUTALIPATA TAIFA LETU ZURI LA Tanganyika
 
Nilipenda hii ya aliyotoa Waryoba kuwa "Waasisis walituanchia nchi moja yenye serikali mbili, hawakutuachia nchi mbili zenye serikali mbili". Kuna mabadiliko mengi yamefanyika bila hata kuangalia Katiba na mwisho tukajikuta na nchi mbili zenye serikali mbili ambamo muudo wa serikali mbili haufanyi kazi tena.

Je hoja hiyo kuna mtu ameweza kuijibu?! Sana sana watu wanaikwepa!
 
nitakacho mm ni mfumo wa muungano ubadlike na
vilevile serikali ya tanganyika iwepo kwanini
serikali ya mapinduzi zanzibar ipo ya tanganyika haipo
huo si ni unyonyaji kwa raia wa nchi ya tanganyika
tumefunikwa shuka la muungano wakati tunanyonywa bila kujijua
tumeamka sasa tunataka mfumo huu ubadilishwe kabisa
 
Mkuu Lunyungu, endelea kujifariji na matumaini hewa ya kukufuliwa kwa marehemu Tanganyika!. Watakao amua mfumo gani wa kufuata, sio hao waliohojiwa na ITV, wala sio Watanzania milioni 45!, bali ni wale wateule 600, kati yao ASILIMIA 80% yaani wajumbe zaidi ya 500 ni CCM!. Matokeo ya mwisho ni kuendelea kwa serikali mbili!.
Nimeshauri hapa, tuwahamasishe Watanzania wote waikubali katiba hiyo ya serikali mbili!Mchakato Huu wa Katiba, ni Umasikini Wetu!,

Pasco

Wateule 600+ watapitisha serikali 2, SAWA! Ila nina mashaka na watakaopiga kura ya Maoni! Kwa kutumia daftari la wapiga kura lililopo, ongeza non-interest towards voting waliyonayo waTZ, ni hakika serikali 2 zitaendelea kutamalaki, na katiba mpya haitaandikwa, na ikiandikwa basi itaanza kupigwa viraka ndani ya miezi sita ya kwanza tu! Toumbe uzima tutashuhudia mambo ya ajabu kabisa!
 
Tafiti finyu hizo, wanaotaka Tanganyika waulize sababu ya msingi hawana. Nn wanakosa Tanzania mpaka wadai Tanganyika? Na Tanganyika ni serikali iliyooachwa na mkoloni je wanataka mkoloni? ,

Soma kwa makini hoja za tume kabla hujaanza kuchangia mada, naona umekurupuka mno hizo ni takwimu halali za tume iliyoundwa na serikali ya ccm ubaya wake ni kuwa zinaweka mashakani maslahi ya watawala na kuyaweka wazi maoni ya wananchi sijui mngesemaje kama tume hiyo ingeundwa na upinzani shame on you:embarassed2:
 
Back
Top Bottom