Mamzalendo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 1,670
- 558
Juzi kaka anayetusaidia kazi alikamata panya watatu mmoja mkubwa, wawili wadogo lakini mkubwa na mdogo mmoja akawaua akampa paka wangu ambaye naye amezaa watoto watatu akawala wale waliokufa. akamtupia paka wangu katoto kamoja ka panya kaliko hai huwezi amini alikachukua hadi kwenye box walipo watoto wake mpaka leo kale kapanya kapo hai na kanalala na hao watoto wa nyau na mama nyau yupo! hapa nyumbani tumekumbwa na mshangao hivi kuna mtu alishaona hili? na je huyu paka ana akili timamu?