Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 1,465
- 4,083
Nimeolewa, na ndoa yangu ina miaka 7 sasa hivi. Nina watoto watatu, lakini mtoto wangu wa kwanza sikumzaa na mume wangu wa sasa.
Kuna mwanaume niliwahi kuzaa naye kabla ya kuachana, na baadaye yeye akaoa mwanamke mwingine, ndipo mimi nikampata mume wangu wa sasa. Maisha yangu yanaendelea vizuri.
Sasa hivi, mume wangu ananihudumia mimi na watoto wote, hakuna anayebagua hata mmoja. Sababu ya kuja kwako ni kuhusiana na baba wa mtoto wangu wa kwanza. Ni mwanaume ambaye anapenda kunishirikisha mambo yake mengi; hawezi kufanya kitu chochote bila kuniambia, hata mambo ya familia yake yeye na mke wake ananiambia.
Kuna kipindi alipitia changamoto na mke wake. Yule mwanamke alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine, hivyo akaondoka na kukaa huko kwa mwaka mzima bila sababu. Baadaye alirudi, na baba wa mtoto wangu alimpokea, ingawa nilimshauri asiwe na haraka kumkubali kwa sababu hakuwa na uhakika kwa nini aliondoka. Hata hivyo, hakunisikiliza na wakarudiana.
Waligombana tena mwezi wa nane, na kila mmoja akaanza kulala kitanda chake. Sasa baba wa mtoto wangu ameamua kuoa mwanamke mwingine. Tayari ametoa mahari, na harusi ni mwezi ujao. Mke wake mkubwa anajua, lakini baba wa mtoto wangu anataka nishiriki kwenye kila kitu, na anataka niende na mtoto wao kwenye harusi.
Nimemkatalia, nikimwambia kuwa nina familia yangu. Mtoto ni mkubwa, kama ni harusi ya baba yake, aende mwenyewe au atafute mtu mwingine wa kumpeleka, lakini hataki. Amekuwa mkali na ameniblock, na nikimpigia kwa namba nyingine ananiambia niamue vipi. Mimi nashindwa kweli nifanye nini, nataka tu tuwe na amani, lakini mimi nina ndoa yangu.
Yeye alikuwa anamwambia mke wake kila kitu kuhusu sisi tunavyozungumza, lakini mimi siwezi kumwambia mume wangu. Mume wangu anajua tu kuwa tunawasiliana kuhusu mtoto, hajui kuwa ananiambia mambo yake binafsi. Je, ni sawa mimi kumpeleka mtoto kwenye harusi na mimi kwenda kukaa huko wiki nzima?