Paka wako ukimnyima chakula ataenda kula kwa jirani

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
PAKA WAKO UKIMNYIMA CHAKULA
ATAENDA KULA KWA JIRANI.

Sina shaka kuwa unawafahamu PAKA, kama hujawai kufuga, basi hata kwa jirani zako ushawahi kuwaona.

PAKA ni miongoni mwa wanyama wa kufugwa wanaoishi vizuri na binadamu, lakini pia wana tabia ya kubadilika na kuwa moja ya viumbe hatari kwa binadamu.

Moja ya tabia nzuri za PAKA ni kupenda anapopendwa.

PAKA ana uwezo wa kuwajua watu wote wa ndani anapofugwa ni nani ana upendo na yeye na ni nani ambaye hampendi.

PAKA ukimpenda na kumthamini atajua na atatulia ndani ya nyumba na kutelekeza majukumu yake.

PAKA ukimyima chakula, ataenda kula kwa jirani.

PAKA ni mpambanaji sana na anajua kujitafutia. Kamwe hawezi kufa kwasababu ya njaa.

PAKA ukimyima chakula, anaweza pia kuwa mwizi.

PAKA anahitaji mapenzi, PAKA anahitaji mahaba, PAKA anahitaji michezo, PAKA anahitaji furaha.

Kama utamnyima PAKA wako mapenzi, mahaba, michezo au furaha basi usije kumpa lawama siku ukimkuta kwa jirani yako au kwa moja ya mafiki zako au kwa mtu mwingine yeyote anayetambua thamani yake.

Sijui unanielewa lakini!!? Hahahaha!!! Basi hicho ndicho ninachokimaanisha.

Mtunze PAKA wako vizuri, mpe kile anachokihitaji kwa wakati. Njaa ni mbaya sana, kiu inaumiza.

Kamwe! Hakuna PAKA anayeweza kuvumilia njaa. Hakuna PAKA anayeweza kuvumilia mateso.

PAKA ukimyima chakula, ataenda kula kwa jirani na akirudi kwako yeye ni kulala tu, wala hana time na wewe. Yani kwa kifupi, atakuwa yupo kama vile hayupo.

Ukitaka akukamatie panya atakwambia sina uwezo wa kukamata panya. Ni vile tu na yeye anafanya kusudi.

Yani wewe unamyima hiki na yeye anakunyima kile. Hahaha!! Hii ni hatari sana!!

Tambua duniani hauko pekeyako, watu wanaomtamani PAKA wako ni wengi sana na wanaendelea kumshawishi kila siku ili wampate.

Usipokuwa makini, utampoteza kirahisi sana, ukija kushtuka keshaondoka na si wako tena. Bahati hairudi malambili.

Thamini sana ulichonacho, kiheshimu, kitunze na ukilinde.

PAKA wa watu unaowatamani, kuna wenyewe wanaowafanya wawe vile walivyo, hata wako ni mzuri kuliko wako lakini ni vile tu wewe umeamua kumchukulia poa PAKA wako.

Ujumbe huu ni kwako baba, kwako mama, kwako kaka, kwako dada. Neema ya Mungu na iwe juu yako katika kujifunza.

#No_Learning_No_Earning
So we have to Learn.

Prepared By
Mr George Francis
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

c53e15e61d30cf1fe1c7e53a8da11e17.jpg
 
Unaweza fanya hayo yote na bado ikawa kazi bure. Wanawake wengi walioumizwa walifanya yote haya ila wakasalitiwa na wanaume wao waliowapenda na pia wanaume wengi walioumizwa walifanya haya yote na mwisho wao wa mahusiano ulikuwa mbaya zaidi. Haya mambo kwa njia za kibinadamu hayana formula maalumu.

Nimekuja kugundua hakikisha unamkabidhi mke wako au mume wako kwa Mungu huku ukiishi maisha matakatifu, Mungu ataipigania ndoa yako hakuna mfano.

Ila pia kwa walioumizwa wasiwe na uchungu, wasibadilishe tabia zao kuwalipizia kisasi wengine, watapata waliofanana nao. Wasiache tabia njema.

Kuishi maisha matakatifu ni pamoja na kumjali, kumpenda ila kuhakikisha pia humwachi Mungu kwasababu ya huyo paka ikitokea kakengeuka kipindi cha uchumba kabla ya ndoa.
 
Back
Top Bottom