Padri Amkimbia Muumini...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Padri Amkimbia Muumini...!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mkare, Feb 11, 2011.

 1. M

  Mkare JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu.
  Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya
  ishara ya msalaba akaanza kuungama.

  "padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"
  "endelea"


  "bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba
  shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi.
  Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua
  tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"

  "utasamehewa"


  "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama
  loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku
  na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe
  na hiyo?"

  "utasamehewa"


  "nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti
  akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama
  huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"

  "utasamehewa"


  "nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo?"

  - kimya........

  "padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"

  - kimya.........

  Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona

  kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha
  katikati ya majoho anatetemeka.

  "sasa baba mbona umenikimbia?"

  padri kwa taabu akajibu


  "nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"
   
 2. d

  docotera Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi anayo
   
 3. s

  shosti JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mhh uchakachuaji kila mahali:sick:
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli wewe ni mkare kwa uchakachuzi!!!
   
 5. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Duh!..
   
 6. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  ....Alimsahau hadi Mungu?..
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii mbona ipo hapa na ilisababisha watu wakapewa BAN, muwe mnapitia thread kabla ya kupost!!
   
 8. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Padri alifanya wajibu wake na wala hakijifikiria yeye binafsi - aliamua kumwondolea jamaa opportunity ya kuua tena.
   
 9. B

  Big dee Member

  #9
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anajua kitakachofuta ni nini ndio maana akakimbia coz walikuwa wawili
   
 10. 2k Genius

  2k Genius Member

  #10
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kal sana
   
 11. k

  kipakaMwitu Senior Member

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 159
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ya longi sana! Mpaka ilishachuja.
   
 12. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Itawezekana kweli members kupitia threads zote toka mwanzo kabla ya ku-post?
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Padri aliunganisha mtiririko wa mambo akaona atakuwa next
   
 14. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Baab kubwa!! Nimeipenda sana!
   
 15. mkonomtupu

  mkonomtupu JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mtaliano aliopoa dadapoa na kwenda kula nae raha mpaka asubuhi. Namchana huohuo jamaa alikuwa anarudi kwao. Asubuhi jamaa badala kumpa dolar 100 akampa mia3. Dadapoa kuona hivyoa akaona mpango si ndio huu. Akaamua amsindikize ili akirudi awe ndo mteja wake. Kufika airport jamaa wakati anamuaga demu kwenda kupanda ndege akamtambia dadapoa.
  Mtaliano: Hey fake dollaré
  Dadapoa naye akamjibu: ukimwi guarantino
   
 16. kuru

  kuru Member

  #16
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbuka pia kuna member ambao ni wapya so hawajaisoma
   
Loading...