Padri amkimbia muumini

Padri amkimbia muumini

BIN BOR

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
1,013
Reaction score
407
Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.

"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"

"endelea"

"bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"

"utasamehewa"

"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"

"utasamehewa"

"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"

"utasamehewa"

"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo?"

- kimya........

"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"

- kimya.........

Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka.

"sasa baba mbona umenikimbia?"

padri kwa taabu akajibu

"nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"
 
Hhahahaaaaaaa taratibu mbavu zangu jamani,unanidai kachori:clap2::clap2::clap2:
 
Kwikwikwiii, du hapo Padri lazima alipata haja kwa Kabati....:amen: :clap2:
 
hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa teheeeeeeeeeeeeeeeeeeee kwi kwi kwi kibano kilikua kinaenda kwa padre
 
hahahhahha unafanya mchezo na kifo......
 
Bora alikimbia maana aliona trend inavyoenda kila aliyebaki na jamaa alipewa chuma so na yeye akaona amebaki na jamaa so ah ni nduki tu.
 
Padre kama unapenda pepo kwann uogope kifo?unachekesha ah unanipa raha unafikiri mbinguni utakwenda kwa motokaa?
 
this is upselute hilaries
sante kwa kuniongezea siku za
kuishi dear
nimecheka sina hamu....
 
Tehe! tehe! tehe! tehe! mbavu zangu mie..
 
Tuko wawili peke yetu, ilimwogopesha Padri. ha ha ha
 
Padri aliona sasa njia iko wazi ya kukutana na malaika mtoa roho, kwa hiyo ikabidi asepe!
 
Duh! mi mwenyewe nilikuwa nataka kuondoka kimywa kimya nilipokuwa naisoma hii
Nilihisi tupo wawili!
 
Dah maskini padri wa watu lazima na yeye ni marehemu tu
 
Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
hahahahahahahahaaaahahahaahahahaaaahahahaahahahaaa

Senx mkuu! umeclear my day
 
Back
Top Bottom