Padre amwagiwa Tindikali huko Zanzibar

Padre amwagiwa Tindikali huko Zanzibar

Status
Not open for further replies.
>Waliua padri huko huko mwingine wakamjeruhi kwa risasi sista wakampiga.. Leo wamemwagia padre tena tindikali... Hawa ni waislam... Hakuna mkristo hata awe kichaa anaeweza kufanya upuuzi kama huu! Roho zinazotenda haya ni za kishetani..
 
Huo ni mpango u s a ili apate sababu ya kuingia tz kuvuna mafuta na gesi hao ni fbi na wala sio uamusho sema watz uwezo wao wa kuchambua mambo mdogo ,
 
Haitatokea KAMWE kwamba eti TANZANIA NI NCHI YA WAISLAM PEKE YAO AU WAKRISTO PEKE YAO, Nasema KAMWE HAITATOKEA. Ni MWEHU TU NDIYE ANAWAZA HILO LITATOKEA SIKU MOJA!!
 
Ponda alishasema "Mtu yoyote asiyekuwa mwislamu ni kafiri, na makafiri lazima wauwawe ili dola ya kiislamu isimame." Naona wanatekeleza maagizo.

Ndugu yangu,Debe tupu haliachi kupiga kelele.Dini inayomwamini Mungu wa kweli huwa ni tulivu na Isiyo na Jazba kwani inajua Mungu wake ni Mwenye Nguvu na ana uwezo wa Kujipigania.
 
tunaomba ushahidi.
lakini ngoja tuweke sawa jambo hili.
jamii yoyote inayo jitegemea huwa inataratibu za kujihami na uadui wowote kutoka nje.hata tanzania ipo sheria ya uhaini dhidi ya serikali. kwa hiyo kama utaunguzumza uislam katika sheria ya kujihami hilo haliusiani na kadhia hii.
na suala uadui dhidi ya dini ya m/mungu sio kipindi cha muhammad peke yake ,hata yesu kwenye biblia anasema wala msidha nalikuja kuleta amani la bali upanga. lakini mbele akaeleza kwamba fitina itatokea kati ya ndugu na ndugu kwa sababu ya kumfuata yeye.
sasa kama una ushahidi kuwa uislam umefundisha kumdhuru mtu asie na hatia naomba unisaidie mkuu.

Mimi ni muislamu khamsu swalawatu labda hujanielewa. Alichokisema ritz ndio uislamu khaswa unatufundisha.
 
Ndugu yangu,Debe tupu haliachi kupiga kelele.Dini inayomwamini Mungu wa kweli huwa ni tulivu na Isiyo na Jazba kwani inajua Mungu wake ni Mwenye Nguvu na ana uwezo wa Kujipigania.
nini sababu ya crusade?.
 
Hawajasoma ila wame elimika!!! hii kauli yao naanza kuwa na mashaka nayo
 
Hata kutolewe maelezo gani, itakuwa ni vigumu sana kuamini kuwa hakuna mkono wa serikali kwenye matukio kama haya. Kwa sasa kuna mambo makubwa matatu yametokea yanayoitesa serikali ya CCM. Moja ni umoja wa Wazanzibari na Watanganyika, wakristo na waislam juu ya kutaka Wazanzibari wawe na uwakilishi sawa na Tanganyika katika uundwaji wa katiba mpya. Pili ni umoja uliooneshwa na Watanganyika na Wazanzibari, wakristo na waislam kupinga njama zinazofanywa na CCM kuhodhi uundwaji wa Katiba mpya. Tatu ni umoja unaotaka kuibuka kati ya CHADEMA (chenye wafuasi wengi bara) na vyama vingine vya upinzani ikiwemo CUF (yenye wafuasi wengi visiwani) katika kupinga CCM kuhodhi mchakato wa katiba.

CCM wanajua kabisa ushiriki sawa wa wajumbe wa Zanzibar na Tanganyika kwenye bunge la katiba, ni dhahiri kuwa Mwungano utakuwa wa serikali tatu, kitu ambacho wameapa hawataki. CCM inaamini inaweza kuwaburuza Wazanzibari kufikia nia yake ya kutokuwepo serikali tatu kama hakutakuwa na umoja kati ya Watanganyika na Wazanzibari, na kati ya wakristo na Waislam.

Kwenye hili tuwe na utulivu huku tukiendelea kuchukua kila tahadhari. Tutashuhudia mengi ya kuhuzunisha kadiri CCM inavyozidi kuonekana kutoungwa mkono. CCM na serikali itafanya kila jitihada kipindi hiki kuhakikisha hakuna umoja wa vyama vya upinzani, umoja na maelewano kati ya dini wala umoja kati ya bara na visiwani. Tukianza kugombana tu na kunyosheana vidole kwa misingi ya kidini, kivyama au kibara na kivisiwani, CCM WATAKUWA WAMEFANIKISHA NIA YAO MAANA NDIYO WANACHOTAKA.

Wazanzibar ni watu wa amani sana na huu utakuwa ni mchezo wa wale wanaogogopa kuiona ZNZ ikiwa huru. Hatuwezi kumeza propaganda za kijinga kama hizi, haingii akilini mtu mwenye akili timamu akammwagia tindikali au kufanya jaribio lolote la kutaka kumdhuru kiongozi wa kidini au yeyote yule.

Nadhani ni muda muafaka kwa wananchi kuilazimisha serikali kuweka wazi uchunguzi na uwajibishaji wa wanaofanya hivi vitendo kama kweli haya yanafanywa na wananchi wa kawaida!
 
Tunapochangia huu uzi, ni Lazima kwanza tutenganishe ugaidi na uislam.
 
poleni wakristo wa zanzibar hakika serikali inahitajika kutoa majibu inaonekana ni tatizo sugu zanzibar.
wakristo poleni take care
kama vpi helment inahitajika kujikinga.....
 
Naona ulikuwa na uhakika kwamba ushaidi upo ndio maana ukaanza kujitetea.
AL - MAIDA 5:51
51. Enyi mlio amini!
Msiwafanye Mayahudi
na Wakristo kuwa ni
marafiki. Wao ni
marafiki wao kwa wao.
Na miongoni mwenu
mwenye kufanya urafiki
nao, basi huyo ni katika
wao. Hakika Mwenyezi
Mungu hawaongoi watu

* 51. Enyi mlio amini! Si
halali kwenu
kuwachukua Mayahudi
na Wakristo mkawafanya
ndio marafiki zenu. Wao
hao ni sawa sawa katika
kukufanyieni uadui. Na
mwenye kufanya urafiki
nao, basi ni kundi moja
nao. Na hakika
Mwenyezi Mungu
hawaongoi wanao
jidhulumu nafsi zao kwa
kufanya urafiki na
makafiri.

Hivi ndivyo waislam wanavyofundishwa,
 
Haitatokea KAMWE kwamba eti TANZANIA NI NCHI YA WAISLAM PEKE YAO AU WAKRISTO PEKE YAO, Nasema KAMWE HAITATOKEA. Ni MWEHU TU NDIYE ANAWAZA HILO LITATOKEA SIKU MOJA!!

Itatokea Zanzibar kuwa nchi ya waislamu peke yao. Zanzibar ni taifa la kale, Tanganyika siyo taifa la kale.
 
Mimi ni muislamu khamsu swalawatu labda hujanielewa. Alichokisema ritz ndio uislamu khaswa unatufundisha.

nilikuwa sijakuelewa kwa sababu sentes yenyewe ilikuwa fupi na ilikuwa tata. labda ushauri wangu uwe unaainisha vizuri kuna watu tunachukulia tafsiri tofauti.
niwie radhi kwa kuto kukuelewa sentens yako.
 
Wazanzibar ni watu wa amani sana na huu utakuwa ni mchezo wa wale wanaogogopa kuiona ZNZ ikiwa huru. Hatuwezi kumeza propaganda za kijinga kama hizi, haingii akilini mtu mwenye akili timamu akammwagia tindikali au kufanya jaribio lolote la kutaka kumdhuru kiongozi wa kidini au yeyote yule.

Nadhani ni muda muafaka kwa wananchi kuilazimisha serikali kuweka wazi uchunguzi na uwajibishaji wa wanaofanya hivi vitendo kama kweli haya yanafanywa na wananchi wa kawaida!

Kama walimuua hata Rais wao, hawa watu sio wa kuamini kabisa. Tuwaache peke yao, tuvunje Muungano tu, coz ni hatari kwetu kwa kutokuwa na mpaka wa kinchi na watu waliokubuhu kwenye uhalifu kwa kiwango hiki kila kukicha. Mungu awalaani wote walioshiriki ktk uhalifu huu.
 
watanzania tunatizo la kufunika ukweli na kufanya kila jambo siasa, huu ushabiki wa kisiasa hautatupeleka popote mimi nimesema kitu kilicho halisia ya kuwa ukristo hautakiwi na especially watu kutoka bara.

nimeishi zanzibar zaidi ya 15 yrs na nimesoma huko tukiwa na akina zito ingawa hakusoma muda mrefu akajiunga na udsm. tuache siasa wazanzibar hawataki muungano na mfumo kristo.
 
Hayo mambo yanafanywa na waislamu,dalili zote ni wao.
Huku bara hatumwagii mapadri tindikali wala shehe.HAO WAISLAMU WANAOFANYA HAYO hawawezi kulazimisha kueneza uislamu kwa njia za kipuuzi kama hizi.

Unaonaje? ww ukakaa kimya km huna kumbukumbu sahihi na yule aliyeua kw bomu ARUSHA na kuua na kujeruhi alikua je? UPAKO ndio unavyosambazwa?
 
Hakuna cha waislam wala nini hapo. Sheikh kamwagiwa acid znz. Mkurugenzi wa baraza la manispaa kamwagiwa acid nae, wale wadada wa kizungu, hao ni wahuni tu waso kazi wanataka kuchanganya watu. Cha muhimu serikali ni kupambana na watu wa aina hio kwani inaonekana matukio kama haya yanashamiri lkn hakuna anaekamatwa kama watu hawajaendelea wafanyeje? Hali ishakua ya hatari hata kwa sisi raia wa kawaida mana si ajabu kesho na keshokutwa hata mimi yakanikuta haya Yarab salama. Mchana kweupe mtu anamwagiwa tindikali tena hakamatwi, kweli ndo kuna ulinzi na usalama kwa wananchi .
 
Je serikali yetu isiyokuwa sikivu itakimbilia kusema ni wahuni ama itachukua hatua? Inasikitisha na nalaani kitendo hiki ambacho kimelelewa na serikali yetu pasipokuchukua hatua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom