P.A.Y.E na TIN number | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

P.A.Y.E na TIN number

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by fxb, Jun 23, 2011.

 1. fxb

  fxb Senior Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wadau hebu nipeni uzoefu wenu kuhusu mtumishi aneyekatwa tax kwenye mshahara wake (P.A.Y.E) Ninavyo fahamu mwajiri hupeleka makato hayo TRA. Swali hivi mwajiri anatakiwa kuwa na TIN number za wafanyakazi ili ijulikane mwajiri huyu amechangia kiasi gani au makato yake ni kiasi kadhaa?
  Nani anakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa P.A.Y.E inacorrespond na TIN number ya mfanyakazi ni Mwajiri au Mfanyakazi mwenyewe?
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naomba nikupe uzoefu wa kwenye taasisi niliyopo kama Meneja wa Mradi

  Sio kwamba kila mfanyakazi ana TIN number yake bali taasisi inayo TIN number ambayo ndiyo inayotumika kwenda kulipa PAYE za wafanyakazi wote. Hata hivyo kwa mfanyakazi akitaka kujua kiasi cha kodi anachokatwa ataangalia kwenye Salary Slip yake ambayo inaonesha kwa ussahihi kuwa hiyo imelipwa. Lakini pia kila baada ya miezi sita kuna report tunayopeleka TRA (wana form maalum inayoitwa PAYE STATEMENT AND PAYMENT OF WITHHELD kwa kuanzia Jan 1 mpaka June 30 na pia kwa July 1 Maka Dec 31 yenye ref ITX215.01.E-P.A.Y.E. Statement) ambazo zinapaswa kujazwa pamoja na viwango vya mishahara kwa kila mlipa kodi ambao nao wanahakikisha kuwa kweli imelipwa sawa.

  Pia huwa tunapopeleka benki hupeleka kwa pamoja bila kuonesha kwa kila mfanyakazi amelipa kiasi gani kwani fomu zao za TRA za kujaza PAYE ( EMPLOYMENT TAXES PAYMENT CREDIT SLIP ITX300.01.E Employment Taxes Payment Credit Slip) hazina sehemu za kuonesha mchango wa kila mfanyakazi

  Hope itasaidia kwa sehemu na wadau watakusaidia kwa undani

  BTW: Umehisi wakuu wanakulambia nini? Nenda wasiliana na ofisi za TRA karibu wakusaidie zaidi
   
 3. fxb

  fxb Senior Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante kwa maelezo mazuri nitafuatilia kwa wahusika kama ulivyo shauri
   
Loading...