Vitu 20 Usivyotakiwa Kusema Wakati wa Usaili wa Kazi (Job Interview)

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Inawezekana una maarifa stahiki pamoja na uzoefu unaohitajika kwenye kazi fulani, lakini ukakosa kazi hiyo kutokana na vitu ulivyosema au kufanya wakati wa usaili wa kazi. Ni muhimu kufahamu kuwa lengo la usahili wa kazi siyo kukufahamu wewe au kufahamu matakwa yako, bali ni kutathimini kama unafaa kwenye kazi au kampuni husika. Hivyo ni muhimu kuhakikisha yale yote unayoyasema na kuyafanya kwenye usaili, yanaonyesha kufaa kwako kwenye kazi husika. Ikiwa unatafuta kazi au umeitwa kwenye usaili wa kazi, basi fahamu vitu 20 ambavyo hutakiwi kuvisema au kuvifanya wakati wa usaili wa kazi

1. Sipendi kazi yangu ya sasa au ya awali. (Kwa hiyo utachukia na hii unayoomba?)

2. Mwajiri wangu wa awali ni mbaya. Kwa kusema hivi utaonekana utamchukia na huyu wa sasa.

3. Kampuni au taasisi niliyofanya nayo kazi ni mbaya. Utaonekana utachukia hata hii unayoomba kazi.

4. Kazi hii ina mshahara kiasi gani? Utaonekana uko kwa ajili ya pesa na si kufanya kazi.

5. Nitapewa likizo lini? Usiulize likizo hadi utakapopata kazi.

6. Je mtanipa usafiri au nauli? Utaonekana unatafuta manufaa yako binafsi kuliko ya kazi.

7. Samahani naomba nipokee simu. Zima simu yako wakati wa usaili; usipofanya hivyo utaonekana hauko makini na kazi.

8. Ninahitaji sana kazi hii. Inaonyesha kuwa unataka kazi kwa sababu ya shida na wala si uifanye vyema.

9. Sina uzoefu mnaoutaka, lakini mimi ni rahisi kujifunza. Acha mwajiri akutathimini yeye mwenyewe kutokana ujuzi wako.

10. Iko kwenye barua ya maombi. Mwajiri anafahamu kuwa unabarua ya maombi lakini jibu swali lake alilokuuliza badala ya kujitetea kuwa jibu liko kwenye barua.

11. Samahani nina miadi (appointment), je usaili utaisha mapema? Tafadhali epuka kosa la kwenda kwenye usaili ukiwa huna muda au utulivu wa kutosha.

12. Samahani nimechelewa. Hakikisha siku ya usahili huchelewi, utaonekana hujui kutunza muda.

13. Lugha mbaya au kuapa. Usiape wala kuzungumza lugha mbaya kwenye usaili. Haki ya Mungu nasema kweli, n.k. havitakiwi kwenye usaili.

14. Sera zenu zikoje kwenye swala la mahusiano baina ya wafanyakazi? Usiulize swali hili kwani usaili ni juu ya kazi na si maswala ya mahusiano yako binafsi.

15. Sina mwangalizi wa mtoto au familia, lakini ninamtafuta hivi karibuni. Usimwonyeshe mwajiri kuwa kuna mazingira yanayoweza kukuzuia kufanya kazi vyema.

16. Ratiba hii ni ngumu kwangu, je inaweza kubadilishwa? Usitake mabadiliko ya ratiba rahisi kwako hadi pale utakapopata kazi.

17. Sina swali. Unatakiwa uwe hata na swali dogo jepesi unapopewa nafasi ya kuuliza swali.

18. Mnajihusisha na nini kwenye kampuni hii? Tafiti kampuni au taasisi vyema kabla ya kwenda kwenye usaili badala ya kuuliza mswali kama haya.

19. Wafanyakazi wanapata manufaa gani kutoka kwenye ajira yenu? Usiulize kuhusu manufaa wanayopata wafanyakazi hadi pale utakapopata kazi hiyo.

20. Huwa sijisikii vizuri kwenye usaili. Watu wanaokusaili wanahitaji kupata na kusikia mtu anayejiamini na si anayeogopa usaili. Neno la Mwisho Naamini sasa hutokosa tena kazi kutokana na maneno au vitu ulivyovifanya wakati wa usaili. Usaili ni jambo linalohitaji maandalizi mazuri na utulivu wa kutosha. Hakikisha hufanyi makosa, waonyeshe wale wanaokusaili kuwa wewe ni jibu la mahitaji yao.
 
Kwa maana hiyo mtoa maada unataka tuseme maneno wanayotaka kuyaskia na sio kilicho kichwani mwetu
 
Kama ipo, ipo tu. Unaweza ukajiuma uma kwenye interview na kazi ukapata endapo watu wa hapo wamekupenda hasa kimuonekano!
Ukiwa na damu ya kunguni, hata ujieleze vizuri kiasi gani unatoka bila bila!
Kuna tafiti niliisoma inasema waajiri na wafanyakazi kiujumla wanapenda kufanya kazi na Good looking individuals either pretty woman au handsome folk
 
Kama ipo, ipo tu. Unaweza ukajiuma uma kwenye interview na kazi ukapata endapo watu wa hapo wamekupenda hasa kimuonekano!
Ukiwa na damu ya kunguni, hata ujieleze vizuri kiasi gani unatoka bila bila!
Kama ipo, ipo tu. Unaweza ukajiuma uma kwenye interview na kazi ukapata

Labda kama unayo connection
 
Namba nne mzeya tunafanya kazi ili tupate pesa....kama tungekuwa na pesa tusingejisumbua kuammka usubuhi usubuhi kwenda kwenye maofisi ya watu.

Hamna mwajili mwenye loyalty kwako na wewe upo pale kwa ajili ya hela pure and simple.
 
Duh...sie sura personal tunakataliwa na mademu na sasa hadi kazi nazo hawtutaki maofisini....aise!

nimecheka kwa sauti japo usiku

Sasa Mzabzab tuseme ww ni Hiring Manager wamekuja wanawake kufanya interview wote wana uwezo unaofanana kichwani

Ila kuna mmoja ana sura ya baba ake na mwingine ana sura ya mdoli na shape ya coca cola utamuajiri yupi
 
Kwa manufaa ya kampuni na pia taifa kwa ujumla ni bora nimpe kazi mwnmake mwenye sura personal.

Kwanza nitakuwa nailinda kampuni kwa kupunguza uwezekano wa sex scandals. Alishindwa clinton pamoja na ubusy wa kurun dunia.

Pili ni kwamba pisi kali ataweza kuishi tuu maana sie wanaume ikija suala la kumwaga mihela kwa pisi kali ili tuipeleke moto mbususu ni wepesi sana. Huyu sura personal kwa kweli akitomgozwa 2020 mtongozo mwengine atauona 2023 so bora awe na kazi yake angalau ana uhakika wa kuishi...lakini kumbuka hii ina apply kwa job ambazo huyu sura personal hataomekana sana kwenye front line....
 
Imagine uko kwenye finance industry... bank hivi

Jamaa uko vizur , very thoughtful
 
Back
Top Bottom