SoC03 Wahitimu wa vyuo wanaotakiwa kujiajiri na wawekewe mfumo maalum na mahsusi wa kodi ili kukabili tatizo kubwa la ajira na kukuza uwajibikaji wa vijana

Stories of Change - 2023 Competition

Lugano_20

New Member
Jul 10, 2023
2
2
Hali ilivyo sasa.

Sheria za Kodi ya Tanzania inaelekeza ulipaji wa Kodi kwa Kampuni zote zinazoanzishwa (changa) kuwa sawia na kampuni kongwe kama Tanzania Breweries Ltd (TBL), Vodacom Tanzania, Azam, Cocacola Kwanza Tanzania na Mohamed Enterprises METL.

Mfumo unataka kampuni zote zilizosajiliwa chini ya Sheria ya Kampuni za Tanzania kufanya malipo sawa bila kujali umri wa kampuni, hivyo basi hii imekuwa na changamoto kubwa sana kwa vijana ambao wangetamani kujiajiri na kutengeneza ajira kwa vijana wengine walio hitimu.

Katika kukabiliana na Changamoto ya ajira ningeshauri kuwepo namna ya kusamehe baadhi ya kodi kwa kampuni zinazo anzishwa na Vijana wahitimu wa Vyuo Vikuurasmi mbalimbali hapa nchi.

Pendekezo 1
Vyuo viwe na namna ya kuongoza vijana katika masuala ya biashara, inaweza kufanya hivyo kwa kualika wafanya biashara mbalimbali walio sokoni ili wanavyuo wapate mwanga wa biashara ingali wawapo vyuoni.

Pendekezo 2
Vyuo vilivyo vingi hapa nchini wanafunzi ufanya somo la Research au Project kwa Mwaka wa Mwisho, hivyo walimu wawawezeshe wanafunzi namna ya kusajili mawazo yao na wawatafutie mwongozo kutoka sekta tofauti ambazo mawazo ya wanafunzi yatajikita huko.

Pendekezo la 3
Wanafunzi na wahitimu wa angalau Miaka 3 (baada ya kuhitimu) watakaotaka kufanya/ kuanzisha biashara kuwe na Mfumo rasmi kwenye Vyuo ambao utawasajili ili kuwezesha Mamlaka ya Mapato (TRA) nchini wawatambue na kuwatolea/ kuwasamehe baadhi ya kodi ili kuweza kuwajenga kwa kipindi cha angalau Miaka 3-5.

Kodi ambazo Vijana wahitimu wanaweza kusamehewa kwa lengo la kuwakuza na kuwawezesha kuendelea katika kutatua tatizo la ajira ni kama ifuatavyo.

Kodi ya Mshahara (PAYE)
kodi hii inalipwa na mwajiri ambayo anaikusanya kutoka kwa wafanyakazi ambao amewaajiri kwenye kampuni au ofisi yake wafanya kazi hawa wanaweza kuwa wa mda mfupi au muda mrefu, na kodi hii haina tofauti na kodi ya zuio na kisheria mwajiri anatakiwa kutoa kiasi cha mshahara kutoka kwenye mshahara au kwenye ujira ambao mfanyakazi anapata na kiujumla wafanyakazi hawa ni wahitimu wa vyuo hapa nchini.

Kodi ya Zuio (withholding tax)

kodi hii inakusanywa pale tu malipo yamefanyika na malipo hayo yanaweza kuwa malipo na kodi ya jengo, malipo ya huduma, malipo ya mikataba pia malipo ya kuuza bidhaa kwa serikali au baadhi ya mashirika.

Kiwango cha kodi ambacho sheria ya kodi imeweka ni asilimia 10 kwenye kila malipo yaliofanyika na kodi hii inawasilishwa kwa kamishina kila baada ya siku 7 ya mwisho wa mwezi

Kodi ya Provisional
Hii ni kodi ya Makadirio inayolipwa kama kianzio (advance) inayolipwa kwenye vipindi vya kila tarehe ya mwisho ya robo mwaka. Makadilio haya yapo ya aina tatu, aina ya kwanza (self assessment) yanafanyika na mlipa kodi mwenyewe na aina ya pili (adjusted assessment) ni makadilio ambayo mtaalamu(tax officer) wa kodi anafanya kwaajili ya mlipakodi ameshindwa au amejikadilia kiasi kidogo cha malipo ya kodi yake na aina ya tatu (jeopardy assessment) ni makadirio ambayo yanafanyika kwa mtu ambaye hayupo ndani ya nchi kwenye kipindi cha makadilio.

Kodi ya Forodha (customs import duty)

Kodi inayowekwa kwenye bidhaa ghafi, mitambo na mashine mabalimbali zinazoagizwa na kununuliwa kutoka nchi za ng’ambo. Serikali imeandaa vocha ya hazina hii inatumika kulipia baadhi ya bidhaa ambazo serikali imeorodhesha baadhi ya bidhaa ambazo zinalipiwa na serikali mfano gari yenye miaka 0 hadi 7 linapata msamaha bila ya kodi ya uchakavu. Serikali ikiweka utaratibu huu kwenye bidhaa zinazoagizwa na vijana waliohitimu itasaidia vijana kuweza kuagiza mitambo na mashine mbalimbali zitakazo saidia kwenye kukuza uchumi wa taifa.

Kodi ya Kampuni
Kodi inayolipwa kila baada ya mwaka na kampuni pale inapotengeneza faida baada ya matumizi, kampuni hizi zinaweza kuwa limitedi na taasisi zingine kama vikundi na taasisi mbali mbali.

Sheria ambayo inatumika inatoza asilimia 30 ya faida ambayo kampuni inapata na kama kodi hii itaondolewa itasaidi kukuza kampuni kwa sababu asilimia 30 inayolipwa kama kodi inasaidia kukuza kampuni kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa.

Ni wazi kuwa kuna baadhi ya Kampuni au Biashara kubwa zinazoletwa na wawekezaji nchini kupitia Kitengo cha Uwekezaji Tanzania zinapewa Msamaha wa Kodi wa Vipindi vya mpaka Miaka 5.

Pia, suala la serikali kuajiri kila mhitimu wa Vyuo hapa nchini ni la kufikirika na ieleweke haitakuwa rahisi. Kuna vyuo vingi sana nchini ambavyo vinazalisha wahitimu kila mwaka.

Hivyo basi Serikali kwa Ujumla kungekuawa na Wizara zinazohusika na Elimu, Ajira, Vijana, Fedha na Uchumi zishirikiane kwa pamoja kuwezesha hili jambo kwa namna ya kuwezesha vijana waweze kujiajili na hili ili kuleta suluhisho endelevu la ukosefu wa ajira nchini kwa maendeleo ya Vijana na Taifa kwa Ujumla.
 
Back
Top Bottom