Ovalution &fertility window

Depretty

JF-Expert Member
Jun 14, 2013
248
96
Naomba kujuzwa zaid kuliko nijuavyo kuhusu hicho kipindi katika mambo ya uzazi hyo OVULATION (sjui nimepatia kwenye kuandika)na hyo Fertility window ni kipindi gani na kipi kinaanza na huwa kinamaana gani ?naomba ufafanuzi wa kina ili niweze kuelewa zaidi.
shukran
 
Ovulation ni kitendo cha yai(ova) lililokomaa kutoka katika mfuko wa mayai(ovary) tayari kwa kurutubishwa

Kwa kithungu:

Ovulation is when a mature egg is released from the ovary, pushed down the fallopian tube, and is made available to be fertilized.

Fertile window ni kipindi ambacho mwanamke anaweza kushika mimba, hii inajumuisha siku ya Ovulation na siku 5 baada ya Ovulation.
Hichi kipindi kinasaidia wanandoa kukutana wakati wa kutafuta mtoto ambapo ndio urutubishaji unafanyika katika hichi kipindi.Kithungu:

The “fertile window” refers to the period of time in the female fertility cycle during which a woman is able to get pregnant — this typically includes the day she ovulates and the five days preceding ovulation. This is the best time to have intercourse if you’re trying to conceive.
 
Samahani naomba kuuliza.....kwa sisi wanawake ambao tarehe zetu hazijirudii na mzunguko unapishana pishana.....namaanisha kuna mwezi unaingia baada ya siku 28 then 36 then 25 then 32 Kujua siku ya ovulation inatumika njia gani??
 
Mwanamke akiovulate kwanza joto la mwili huongezeka na hutoka maji mazito mfano wa ute wa yai

Kwa kweli hapo ni ngumu subiri wajuzi watakujuza zaidi
 
Samahani naomba kuuliza.....kwa sisi wanawake ambao tarehe zetu hazijirudii na mzunguko unapishana pishana.....namaanisha kuna mwezi unaingia baada ya siku 28 then 36 then 25 then 32 Kujua siku ya ovulation inatumika njia gani??
Ahsante kwa swali lako zuri:
Kuna dalili za kuonesha siku ya Ovulation hata kama mzunguko wa mwezi unabadilika badilika jinsi ulivyoeleza hapo juu kama ifuatavyo.

1. Kwa mzunguko wa kawaida wa siku 28 ambao ndio wanawake wengi wanakuwa nao, siku ya Ovulation ni siku ya 14 tangu hedhi itokee.
Kwa hiyo unatakiwa kuhesabu siku kuanzia siku ya kwanza ya hedhi hadi ya 14, ndio Ovulation inatokea.

2. Kupata maumivu chini ya tumbo wakati yai linatoka kwenye mfuko wa mayai.
Hapa inatakiwa uwe makini maana unaweza kupata maumivu kwa muda mwingine ambao sio Ovulation ukadhani ndio Ovulation imeanza, unachotakiwa ni kujaribu kulinganisha huo muda na ule wa hedhi ilipoanza ili kutofautisha maumivu ya wakati wa ovulation na maumivu mengine ambayo hayahusiani na ovulation.

3. Kiwango cha joto la mwili wakati wa ovulation kinapanda sana ukilinganisha na siku za kawaida. Hapa unafakiwa uwe makini kutofautisha pengine una dalili ya homa.

4. Kiwango cha maji maji ukeni kinakuwa kikubwa sana ambacho kinafanana na utezi wa yai ukilinganisha na siku zingine za kawaida. Pia mlango wa uzazi(cervix) unakuwa mlaini na kufunguka kidogo na kujivuta ndani kuelekea mfuko wa uzazi(uterus) kwa maandalizi ya kupokea mbegu ya kiume(sperm).
Ili kujua hii dalili, tumia kidole kimoja au viwili kuchnguza hali mlango wa uzazi ili kuona kama hizo dalili zipo au la.

5. Pia unaweza kutumia kifaa maalumu(Ovulation Predictor Kits) cha kupima kiwango cha hormone inayoitwa Lutenizing hormone. Hii hormone wakati wa Ovulation inatolewa(kuzalishwa) kwa kiwango cha juu ili kusaidia Ovulation kutokea.

NB: Anayejua zaidi aweza kuongezea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom