Building a Scalable Business

Jane Msowoya

JF-Expert Member
Aug 20, 2017
4,102
7,187
Heshima kwenu wakuu hope mapambano yanaendelea vyema leo ningependa ku share nanyi machache haya kuhusu biashara hapa nalenda zile biashara zinazouza bidhaa ambazo ni scalable hasa upande wa bidhaa (kuna baadhi ya biashara haziwezi kupanuka hata iweje)

Kujenga biashara inayoweza kupanuka ni mchakato na kimkakati unaohitaji maono, uwezo wa kujiendesha kwa mabadiliko, na uelewa mzuri wa soko (wateja wako lengwa) Hapa lazima ukubali kujifunza kila siku,ukubali kuusoma mchezo na kuwasoma washindani wako kipi wanafanya vizuri na kipi wanafanya vibaya yaani wewe lazima uwe active muda wote usilale lale na kulia lia ntaainisha mambo kadhaa na mifano

1. TAMBUA SOKO LINATAKA NINI
Ili kujenga biashara inayoweza kupanuka, kwanza tambua hitaji maalum sokoni, hii inajumuisha utafiti wa wa soko ili kuelewa changamoto za wateja na mapungufu katika huduma zilizopo sokoni (hspa ndo unapowasoma washindani wako). na kuangalia wapi wewe pamoja na washindani wako mnapwaya na jinsi gani unaweza kufanya vizuri zaidi yao.

HOW?
a) Fanya Utafiti wa Kina wa Soko mara kwa mara ili kujua upepo unaendaje
b)Tambua Mapungufu katika Huduma za Sasa Sokoni
c)Elewa Changamoto za Wateja
d)Boresha Bidhaa au Huduma Kukidhi Mahitaji Haya Maalum
2.Tengeneza Mpango wa Biashara Unaobadilika


Mpango wa biashara unaobadilika ni muhimu, Unapaswa kuweka malengo lakini ruhusu marekebisho, biashara inavyokua na hali ya soko inavyobadilika. Mpango unapaswa kujumuisha makadirio ya kifedha, uchambuzi wa soko, na mikakati ya ukuaji. Kuendelea kushikilia pale pale ni changamoto mfano umeweka budget ya matakangazo 500k kwa njia ya insta kwa mwezi sasa unaona kabisa umeshatumia 300k haijaleta mafanikio usilazimishe mpaka umalize kabisa ile 500k kwasababu ndo mpango wako unasema hivyo hapana, muda wowote unabadilisha na kuangalia plan B siku zote unapokuwa na mpango lazima uwe na plan A,B,C kwamba ya kwanza ikienda ndivyo sivyo ntafanya hivi na kila sekta lazima uwe na mbadala wake hapa inaingia hadi kwenye team yako usitegemee huyo huyo tengeneza mbadala wake

3. KURIDHISHA WATEJA WAKO
hapa wengi team inatuangusha unakuta mteja hapewi kipaumbele kabisa ni biashara chache sana zinazowapa kipaumbele wateja (Wenye biashara za shule wamejitahidi sana kushirikisha wazazi)

mfano unaweza tumia feedback za wateja kuboresha huduma yako kwani wale ndio mabalozi wazuri sana maana watu huamini in hearsay ndo mana network marketing wanaendelea kupiga hela miaka yote hutaona kampuni kama kampuni ikiweka tangazo ni wale distribitors wao ndo wanahangaika na marketing.

Gyseee nimechoka kuandika mwingine aongezee nyama lengo kujifunza
 

Attachments

  • 360_F_308630728_8ou9UHyAZzAW8fiO1S9irmJy1dRe4JA2.jpg
    360_F_308630728_8ou9UHyAZzAW8fiO1S9irmJy1dRe4JA2.jpg
    12.7 KB · Views: 5
nimeipenda hii,ningewashauri wakuu mtafute kitabu cha grant cardone kinaitwa SELL or BE SOLD.you will thank me later!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom