Orodha ya vigogo Benki Kuu katika kashfa ya EPA waongezeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Orodha ya vigogo Benki Kuu katika kashfa ya EPA waongezeka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 10, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Date::9/10/2008
  Orodha ya vigogo Benki Kuu katika kashfa ya EPA waongezeka
  Claud Mshana na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi

  ORODHA ya maafisa wa Benki Kuu Tanzania (BoT), waliong'olewa kutokana na kushindwa kuwajibika hadi kulitia taifa hasara katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu (BoT), sasa imefikia sita.

  Kuongezeka kwa kigogo huyo kumekuja wakati tayari maafisa wengine watano wakiwa wameng'olewa kutokana na tuhuma hizo za kushindwa kuwajibika katika kashfa hiyo ya udokozi wa zaidi ya Sh 133bilioni zilizokuwa zikizagaa kwenye akaunti ya EPA.

  Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alithibitisha hilo wakati akizungumza katika Mahojiano Maalumu na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1).

  Hata hivyo, Profesa Ndulu baadaye alifafanua kwamba, afisa huyo mwingine pia muda wake wa kustaafu ulikuwa umekaribia.

  Profesa Ndulu alitumia fursa hiyo kusisitizia umma kwamba, BoT katika mchakato wake, haimwonei mtu.

  Tayari Profesa Ndulu amekuwa akitoa kauli hiyo mara kwa mara kila alipozungumza na Mwananchi kuhusu tuhuma za kwamba mchakato huo umekuwa ukitoa kafara maafisa wa kati huku vigogo wa juu zaidi wakiachwa.


  Akizungumzia maafisa wote sita, Profesa Ndulu alisema waliitwa na kuhojiwa na pia walipewa nafasi ya kujitetea, na kuongeza kuwa kati ya hao, wanne wamekata rufaa kupinga adhabu hiyo.

  Hata hivyo, Profesa Ndulu aliwataka Watanzania kuachana na uvumi na tabia ya kuwazushia tuhuma za EPA watu ambao hawana hatia, akisisitiza kuwa mtu yeyote ana haki ya kukata rufaa iwapo hakuridhika na maamuzi yoyote yaliyofikiwa dhidi yake.

  Kuhusu taasisi hiyo na halisi ilivyo baada ya uamuzi huo wa kung'oa maafisa hao, alisema, BoT ipo imara na inaendelea na utendaji wake wa kazi ikiwa imejipanga vizuri katika kuhakikisha inafanya mambo yake kwa umakini na kuhakikisha masuala ya EPA hayajirudii tena.

  Katika kuhakikisha hayo, Profesa Ndulu alisema, BoT imeandaa mikakati mbalimbali ikiwapo kuhakikisha suala la utawala bora, uwazi na usimamizi ulio mkubwa katika akaunti zake.

  Alipoulizwa kuhusu ugumu katika kupatikana kwa fedha za EPA zilizohamishiwa nje ya nchi, Profesa Ndulu aliweka bayana kwamba, suala hilo lipo nje ya uwezo wa BoT kwani wenye mamlaka ya kufuatilia fedha hizo ni vyombo vya usalama vya ndani ya nchi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kimataifa.

  Kuhusu akaunti ya hifadhi ya fedha za kigeni zilizopo Benki Kuu ambako kumekuwa na wasiwasi kuwa hazitoshi, Gavana Ndulu aliwatoa hofu wananchi na kuwahakikishia fedha hizo za kigeni zinatosha kwa kuzingatia vigezo vinavyofahamika kimataifa.

  Akifafanua hilo alisema, hadi sasa zinafikia zaidi ya dola 2milioni za Kimarekani kiasi ambacho ni mara kumi ukilinganisha na mwaka 1995.

  Profesa Ndulu alisema, thamani ya shilingi ya Tanzania pia imekuwa ikiongezeka japo si kwa kiasi kikubwa, ukizingatia kwa kipindi kirefu shilingi hiyo imekuwa ikiporomoka mara kwa mara.

  Ufisadi katika EPA, ambao bado unaendelea kuitikisa BoT, ulitokana na ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Ernst &Young. Awali, ukaguzi huo ulifanywa na Kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini, lakini ikasitishwa.
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hii article bila majina ni uzushi na ushambenga mtupu, kama hamtaki watu wasio na hatia wasisemwe vibaya kwa nini hamtaji majina ya washukiwa ili angalau tujue washukiwa ni kina nani? Otherwise watu wote wa BOT walio katika level inayohusika wanakuwa potentially implicated.
   
 3. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pundit,

  Achana na kigazeti hicho kitupu cha Mwanachi cha crummy press ya Bongo. Mimi kinachonishangaza ni huyo Ndullu huyo anaeita media kuwaambia orodha imeongezeka, halafu basi. Nani kaongezeka hasemi.

  Hawa kina Ndullu na marehemu Ballali ndio walikuwa wanasifiwa sijui wamefanya kazi za kimataifa, ungedhani wamepata ka exposure kadogo ka world class public relations and accountability. Lakini bado vilaza. Kwa nini?

  Yani watu watupu watupu watupu watupu watupu! Watupu.
   
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Mimi hao siwahesabu kama mafisadi kwani walichokifanya ni kufanya taratibu za kila siku za kibenk wapo waliokuwa assigned kufanya hizo kazi na wengine wame question some of the documents na ushahidi upo. Tunachotaka ni beneficiaries wa EPA nani mmiliki wa Kagoda?je n R.A? Kapeleka wapi 40 bil alizochota kupitia EPA? Kuna uvumi ulivuma mwanzo mwanzo tume ya uchunguzi wa EPA kuwa kuna kampuni mmoja ya uwakili imo kwenye list ya waliochotewa mihela iliyokuwa "inazagaa zagaa BoT" hii ni kampuni ya ndugu w aliyewahi kuwa mwenyekiti wa moja za jumuia za CCM ambae baadae alitimuliwa mnajua nini kilitokea? Jamaa wamegoma kurudisha mikwanja na inasemekana wana kishina cha "cheque leaf " ya baadhi ya fedha walizo zi allocate CCM! Kwahiyo Mkubwa usitegemee list ya hao waliofaidika na hiyo mihela maana utakuja acha mdomo wazi na kupigwa na butwaa yaani hadi fulani anahusika! siamini! wengi pia hatuta amini na ndio maana tunazugwa eti haki za binadamu mara watuhumiwa ni hatari kama magaidi! sasa kama hiyo kweli situtumie sheria ya ugaidi isiyojali haki za binadamu? Mwenye akili ameshajua mchezo mzima itabidi ifikie point tuamue sasa EPA basi maana hakuta kuwa na jipya sana sana wataonewa watu ambao walitekeleza maagizo ya wakubwa wao! AMKENI
   
 5. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kuhani,

  Huyo Ndullu tunamjua kawekwa pale kulinda lango na ku obfuscate, mimi bado nawashangaa waandishi hawakuweza hata kuandika "alipoulizwa kutaja majina ya walioongezeka katika orodha hiyo Gavana Ndullu aliyeyusha hivi na vile"

  Yaani Gavana Ndulu siwezi kumvamia kwa sababu licha ya kwamba najua ni fisadi aliyewekwa pale kuficha maovu na kuokoa jahazi la Titanic lililozama tayari, lakini pia sijui hata alichotaka kusema ni nini, alichosema ni nini na pia sijui kama kilichoandikwa ndico kilichosemwa.Mimi nakula sahani moja na hao hao waandishi wanaoweza a juicy headline halafu article imejaa vioja kuliko vya Kitintale.
   
 6. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Do inashangaza na kusikitisha.

  Wakati wenzetu kenya wanafanya deals wanajenga maviwanda ya kuprocess matunda, sisi tunakwenda kuficha pesa nje ya nchi. Halafu warevu wanakopa wanakwenda kuinvest.
  Hivi sisi watanzania tunazo upstairs (akili) kweli?
  Kenya ni mfano mzuri, mawaziri na vigogo wengi wamejenga viwanda, wana ma airline n.k

  Sasa labda waziri mzima au mbunge au Katibu mkuu umeshawasomesha watoto wako mpaka vyuo vikuu vya nje, halafu unaiba tena mabilioni, angalau ungewekeza basi mbaya zaidi unakwenda ficha nje ya nchi. Faida yake nini?? Sioni faida maana watoto wameshasoma na watatumia akili zao kujitafutia. Sasa kuwawekea watoto mapesa mengi benki unadidimisha uwezo wa watoto na hata wajukuu zako kufikiri. Utaona yanajinenepea tu, yanaota vitambi na matiti, matoto ya mafisadi hayo, Shame!!!

  Pili unasabotage akili za watoto wako, una sabotage uchumi wa nchi yako.

  Mimi nafikiri mashujaa ni Anne Kilango, Shelukindo, Selelii, Mbunge wa Mbozi, Cleopa Msuya na Makongoro Nyerere ambao wamethubutu kukemea ufisadi hadharani. Mungu awabariki.

  Tanzania inatia aibu. Angalia uchumi wa angola Unavyopanda... sisi tuko wapi?? tumekosa nini NI akili tumekosa au ni ulafi wa wachache??

  Kwa sasa natafuta VISA nikafanya kazi Angola, wanahitaji watanzania waliosoma. Twendeni zetu jamani.

  Kitu kingine nashangaa tena, kwa nini Rushwa itumike kwenye uchaguzi?? Kama Mbunge au Diwani ametimiza ahadi na ameshirikiana wa wananchi kuleta maendeleo kuna haja gani kuwanunulia kanga, kofia, pilao na bia??

  Utaona matangazo utafikiri wanatangaza biashara??

  Ufisadi/Rushwa ndio matunda tunayaona ya EPA, Richmond, Ndege ya Rais, RADA, Air Tanzania, n.k
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Kuhani, ndiyo maana mimi nasema Ndullu hafai BoT. Inabidi aondolewe haraka sana.
   
 8. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Bubu,

  Pundit anasema - na mimi nakubali - Ndullu yupo pale kwa makusudi. Kwa hiyo hawezi kuondolewa.

  Na tunapotamka neno "Ndullu aondolewe" tutakuwa kama tunaamini huyo anaetakiwa kumuondoa, yani Kikwete, ana nia nzuri.

  Yani, BOT iligubikwa na skandali la jinai ya EPA, halafu unamfukuza CEO unamuweka VP wake. Kama sio aje kufukia ushahidi ni nini ?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Sep 10, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  We Pimbi vipi ile "investigation" yako kuhusu dokta Masau? Au na wewe ni crummy freelance investigator....?
   
 10. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  I suspect huyo ambaye muda wake wa kustaafu ulikuwa unakaribia ni LIUMBA.Or could be just a wishful thinking....
   
 11. M

  MKUDE WA MGETA Member

  #11
  Sep 11, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilichobaki sasa ni kuhakikisha mwaka 2010 vyama vya upinzani kuwa na 75% ya viti vya wabunge katika bunge la jamhuri ya muungano .hii itasaidia hata ikiwezekana kupiga kura ya kuto kuwa na imani na rais ili upinzani uweze kuwa na rais kutoka kambi hiyo ili tuweze kuwashtaki hawa mafisadi wa epa ikiwemo na kikwete mwenyewe
   
 12. M

  Major JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2008
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  SASA ina maana gani kutuandikia kichwa cha habari kikuuubwa halafu hakina maana yoyote, maana nilifikiri labda nitaona majina mapya kumbe ni uzushi ule ule,ee Mungu ni kwa nini usimwondoe huyu ndulu duniani?labda yangeweza kutokea mabadiliko ndani ya hiki chombo
   
 13. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuhusu akaunti ya hifadhi ya fedha za kigeni zilizopo Benki Kuu ambako kumekuwa na wasiwasi kuwa hazitoshi, Gavana Ndulu aliwatoa hofu wananchi na kuwahakikishia fedha hizo za kigeni zinatosha kwa kuzingatia vigezo vinavyofahamika kimataifa.

  Akifafanua hilo alisema, hadi sasa zinafikia zaidi ya dola 2milioni za Kimarekani kiasi ambacho ni mara kumi ukilinganisha na mwaka 1995.

  US$ 2ml Jamani mbona vijisenti?
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mimi nashangaa hata vyombo vya habari kuripoti vitu hewani hewani nakupamba gazeti huku hakuna details...........mlishindwa kumhoji huyo Ndullu awape majina???????si bora msinge andika tu ieleweke watu wanafichwa kulinda hadhi na heshima ya serikali........
   
 15. A

  AeIoU Member

  #15
  Sep 11, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ndullu na Mkulo wamefikia pabaya sana kwa hatua yao kuwadhihaki na kuwakejeli watanzania, eti majina yameongezeka kuvipi wakati hata ya mwanzo hayatajwi. Kuna mahali ukweki huwa unabaki kama ulivyo kitendo cha kutaka kuupindisha kinaweza kuleta madhara makubwa sana kwa taifa hili. Watanzania tuweni macho kupambana na udhalimu wa nduli ccm mwaka 2010 hawapati kitu la sivyo lazima damu imwagike ili kuonyesha ukomavu wetu katika wimbi la umasikini.
   
 16. A

  AeIoU Member

  #16
  Sep 11, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Jamani tumekwisha????
   
 17. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  It is really bugging me a lot! Kwanini mfano mzuri Nape ametolewa on instant basis hata katika uongozi wa chama. Kwanini ikiwa basi katika level ndogo ya chama wanaweza waungwana kufanya maamuzi ya haraka kwa kukinusuru chama, just chama wakati walioharibu uchumi wa Tanzania fikiria idadi ya watu ambao wanaadhirika, wakifa kidizaini, wakiishi kiaina, wengine wakiendelea na biashara zao kimtindo, wengine wakiendelea kufanya ufisadi kwa dhati! Its a shame and shame be upon them fisadis! Nape wamemtaja au kwa vile ni mmoja halafu minority just because ana public interest na sio interest za siri eti siri kwa vile ina ubaya. Siri JAMANI si lazima iwe ni jambo baya. Siri nzuri huwa jambo zuri na lenye mtazamo pina. Kamwe hata katiba haifundishi kuwa kitu kikiwa kibaya basi kipewe jina siri.

  Again its a shame! And shame be upon them and I pray to Allah the Almighty that all the missery life can offer be cast upon them immediately; those that have eaten our money, those that forfeit our rights, those that saw others eating our money and kept quiet, those that shared the stolen wealthy, those that according to authority are capable of making them (fisadi) responsible for their theft but are not and all that can make this work out but are not; to face the same consequences. Amina
   
 18. J

  Jobo JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani tutajieni majina ya hao mafisadi ndani ya BOT! Siamini kama Balali angeweza kufanya kazi ya uiba mabilioni hayo yote kwa kushirikiana na watu wa nje, tena wahindi na wanasheria bila kushirikisha wafanyakazi waliokuwa katika kitengo cha madeni, sheria na fedha. Sasa kinachogomba hapa ni akina nani hao? Mwenye majina atumwagie hapa ili tuwajue. Maana tumekuwa tunawasema walioko nje lakini wa ndani tunawaacha na mimi naamini hawa pia walipata mgao!
   
 19. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2008
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huyu baba nahisi ana matatizo ya akili.hizo ni pesa za kujivunia wakati wamewapa mafisadi wenzao 133m,kweli anacheza na akili za watz huyu.
   
Loading...