Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015

JK amechagua Tabora pa kutoa ahadi kama hiyo kwa kuwa anajua wana-Tabora wanaburuzika na kudanganyika kwa urahisi tu -- ni utamaduni tangu enzi za Waarabu karne ya 18 na 19!!

Enyi wana-Tabora -- hebu mjitutumue kidogo mumwambie huyo mtani we
nu Mkwere kwamba 'hatudanganyiki tena, haturudi katika historia!
 
Mbona jana kasema anaondoka na anavunja ndoa na JF kwa sababu ya UDINI....kwamba hawezi ona dini yake inatukanwa yeye kakaa kimya.....b4 sikujua kuwa malaria sugu ana dini yake anayoimiliki.

Mkuu, umenifurahisha sana hapo.
 
JK kaahidi kujenga na kukamilisha reli mpya ya Kati (central line)... mimi kimtazamo na kwa kuangalia rekodi ya nyuma naona si rahisi kujenga na kukamilisha ujenzi wa reli ndani ya miaka mitano.. kama km chache za barabara ya mandela zinachukua miaka na miaka, sembuze reli... sitaki kuamini hilo,... labda kama watakamilisha upembuzi wa reli.
lakini lazima tujiulize kwa makini.. je kama wameshindwa kuendesha iliyopo, je miujiza gani itafanyika kujenga na kuendesha reli mpya.. AU KUNA MALAIKA ANAKUJA KUTUOKOA!!!

Ila treni ya umeme Dar-Mwanza kwa masaa matatu aliyoahidi Dr. Slaa huoni kama ni miujiza. Kama siyo uwendawazimu sijui maradhi gani yanayowasumbua. :becky: :becky: :becky:
 
The man has never been serious, whenever i look at his face he always avoid eye contact, which means that he doesn't mean what he says.
 
Hebu tulinganishe enzi za MKAPA NA JK kuhusu mfumko wa bei na kushuka kwa dhamani ya madafu yetu.

KIONGOZI BENJAMIN WILLIAM MKAPA Vs JAKAYA MRISHO KIKWETE

MWAKA 2000 - 2004 Vs 2005 - 2009

Unga 460 Vs 1000 = 217%
Mchele 600 Vs 1200 = 200%
Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
Mkate 250 Vs 700 = 280%
Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
Nazi 100 Vs 550 = 550%
Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%


unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafuta taa kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo 250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500, hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi.

Okay kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni 120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo
hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie
wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila waalimu na wenzao.........! 3 years.


Yeye huyu JeyKey na hao wapambe wake na hao wanajipendekeza kama Shigongo waulizeni watoto zao ni akinani? utaambiwa mbunge, mara yuko BOT mara yule wa mwisho yuko ulaya kamtembelea shangazi yake, mara yuko busy na tenda ya kusuply komputa Wizarani. Wewe je unae mpigia kura tupe wasifu wako hata hao watoto wako na wategemezi wako. Hata baiskeli kule kijijini huna wala wazazi wako ndo unakesha kuwaombea wasiumwe kwa kuwa gharama za hospitali zitakuwa zako.


Muulize kesi za mafisadi vipi? Na je wanampango gani? utaambiwa yuko busy na harakati ya kutafuta ulaji kwa mara ya pili.

Hao wapambe wake na mawaziri wanaendesha magari gani utaambiwa aah wana tano tano kila wizara VBV8, uliza bei zake kila moja, inatumia mafuta kiasi gani kwa mwezi, na majukumu yake ni yapi? Na je zinakoenda akina RAV4, Suzuki, BMW ndogondogo hawafiki? Utaambiwa
wanawahi kuwasilisha agenda. KWEEELI?

Na je hizo gharama za uendeshaji fedha zinatoka wapi? Utajibiwa kwenye mfuko wa serikali. Waulize serikali ina miradi gani ya kuweza kuendesha hayo magari tu achana na posho zao na mengineyo? Jibu ni KODI ZENU wananchi waungwana tulio na amani na utulivu kwetu. KWEELI
kwa mshahara wa laki mbili zangu/zako?

FUNGUENI MACHO NA AKILI ZENU WAUNGWANA. Wenzenu Zenji wameshaliona hili wameamua kujichorea MIPAKA yao Mapema.

MTAENDELEA KUZUBAISHWA NA STORI ZA KUTUNGA NA UDAKU NA KUSHANGILIA MISAFARA MIREFU YA KAMPENI INAYOUNDWA NA KODI ZENU.
 
Ukweli ni kuwa wanaletwa wahindi wengine......watang'oa reli zilizopo na kuleta nyingine kwa stanaadrd gauge ya mita moja kama TAZARA...hii ya sasa ni futi tatu...KULIWA KWETU NI KUWA hizo reli za mjeremani ni high quality steel na zitaenda kuyeyushwa na kuwa chuma ghafi na kuuzwa huko ughaibuni.....hizo za wahindi ni very poor quality ambazo zitakuwa zinalika kirahisi na friction na kutu..TAARIFA NDIYO HIYO
 
mimi nina wasiwasi sana na uwezo wa huyu jamaa wa kufikiri,sidhani kama anafikiri sawasawa,pengine ana matatizo ya ubongo msimlaumu sana kampeni zimemchanganya
 
Ndiyo hapo sasa tupime kuangalia utendaji wa huyu jamaa kuanoa kama JK anafaa kuongoza hata shule ya Makongo..

Ukiangalia tangu 2005 - 2010 wakatia anachukua serikali kwa kebehi eti 1995 hazikutosha sasa zimetosha.. utajua kuwa kweli huyu jamaa hakustahili kuwa Rais wa Tanzania.. Ndiyo maana hata Ben alitaka kumpiga chini lakini atajitengenezea mtandao wake ukiwa chini ya mwenyekiti wa kampeni Lowasa.. watapata nchi japo kwa gharama kubwa sana na kwakutumia hela za hazina, epa and mfuko wa chakula.. sasa angalia alivyoanza kwa pressure, alijua kuwa Salome Mbatia iko siku atamgeuka kwa sababu ule mama alikuwa mchapakazi, wakamtengenezea zengwe la ajali, akafa yeye alikuwa mhazini wa chama.. chama kilichofanya kampeni kubwa bila kuwa na hata pe kwenye mfuko wake...

Jamaa ameahidi Reli ya kati, embu tazama amefanya nini yeye kwenye awamu yake??? miradi yote ni ya Ben.....

Yeye hawezi kwa sababu amezoea majungu sasa miaka mitano imeisha hayafanya kitu,, aliahidi chuo serengeti hata tofali moja hakuna sembuse kiwanja cha ndege???

Watanzania tufungue macho JK and Ebola... Ugonjwa mbaya sana.....
 


Sasa hivi Arusha; karibu kila siku, usiku kuanzia saa moja hadi saa moja na nusu umeme unakatika na udadisi wangu wa kijuujuu umebaini umeme unakatika kwa sababu uzalishaji wa nishati ni duni.

Ahadi za kupeleka umeme kila mahali hususani vijijini nimezisikia lakini kama uzalishaji ni huu basi ni nguzo tu na nyaya zitawafikia walengwa kama kule Kigoma ambako umeme upo lakini hauna nguvu.

Kulikuwa na mkakati wa kuligawa Tanesco vipande vitatu ili kuondoa ukiritimba na kuruhusu hata sisi hoehae tununue vipande miliki na kuyapunguzia mashirika haya ukata unaowakimbiza kukopa kwa Benki kwa gharama kubwa.

Mikakati hii imewekwa kando kwa sababu ambazo haipo wazi. Swali ni Tanesco kwa mfumo uliopo ni kiwavi jeshi na kila kiingiacho kule ni sawa na kile kiendacho kwa mganga huwa haklrudi.

Kwa utani utani huu tunapelekwa wapi?
 
Niemkutana na changamoto hii iliyotolewa na mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA na ikanigusa akili.

Source Mwananchi.

Dk Slaa alibeza ahadi zinazotolewa na mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete kuwa ni za kazi za halmashauri na si rais na kwamba ziko ndani ya bajeti na zinaweza kutekelezwa na yeyote atakayeingia madarakani.
Dk Slaa alisema ahadi zinazotolewa za kujenga barabra, shule, miradi ya maji, zahanati ni za halmashauri ya miji na majiji na sio kazi ya rais.
"Kazi nyingine ni za halmashauri sioni haja ya kuzitaja sana wakati kiini cha matatizo hakishughulikiwi kwa kuwa maadui watatu wa taifa bado wanaitafuna nchi hii," alisema Dk Slaa.


My take:
Kama ahadi nyingi za kikwete ni za ngazi ya halmashauri, inakuwaje watanzania tuchague rais asiyeweza kutekeleza majukumu ya kitaifa?
Je, uwezo wa kikwete uko kwenye ngazi gani?
 
Tunajua maadui maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Je, serikali ya Kikwete ina sera gani madhubuti za kupambana na hawa maadui?

Takwimu ya ujinga inaonyesha kuwa watanzania tunaendelea kuwa wajinga kwani mwaka 1974 tulikuwa na watanzania 10 katika kila 100 wasiojua kusoma na kuandika, lakini takwimu za wizara ya elimu zinaonyesha kwamba kwa sasa wastani huo umepanda na kufikia 31 katika kila 100.

Maradhi ndo usiseme, na kwenye moja ya mikutano yake kikwete amesema wanaopata Ukimwi ni viherehere vyao. Je, kwa kuwanyanyapaa wagonjwa wa ukimwi, huyu mgombea wa urais ataweza kuwasaidia wagonjwa wengine? Baadae atauliza, inakuwaje watu waugue malaria wakati Bush amegawa vyandarua?

Umaskini wa Tanzania unazidi kukua kwani hivi leo mwananchi wa kijijini anashindwa kulipia malipo ya zahanati ambayo ni sh5000 kwa mwaka. Je, hiyo si tosha kuwa uamaskini umekua?
 
No mission to win 2010 election, No vision to eradicate poverty ENEMIES by the ruling party CCM. Ni mchanganyiko maalum.Tutasikia mengi mwaka huu
 
Tunajua maadui maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Je, serikali ya Kikwete ina sera gani madhubuti za kupambana na hawa maadui?

Takwimu ya ujinga inaonyesha kuwa watanzania tunaendelea kuwa wajinga kwani mwaka 1974 tulikuwa na watanzania 10 katika kila 100 wasiojua kusoma na kuandika, lakini takwimu za wizara ya elimu zinaonyesha kwamba kwa sasa wastani huo umepanda na kufikia 31 katika kila 100.

Maradhi ndo usiseme, na kwenye moja ya mikutano yake kikwete amesema wanaopata Ukimwi ni viherehere vyao. Je, kwa kuwanyanyapaa wagonjwa wa ukimwi, huyu mgombea wa urais ataweza kuwasaidia wagonjwa wengine? Baadae atauliza, inakuwaje watu waugue malaria wakati Bush amegawa vyandarua?[/COLOR
:[/COLOUmaskini wa Tanzania unazidi kukua kwani hivi leo mwananchi wa kijijini anashindwa kulipia malipo ya zahanati ambayo ni sh5000 kwa mwaka. Je, hiyo si tosha kuwa uamaskini umekua?



Hahahahaa unaweza kukuta anajiuliza hivyo.:party
 
bala safari za nje mngekufa njaa/malaria wakati dawa tunajinunulia wenyewe, mihogo/mtama/ugali/viazi/mchele tunanunua wenyewe au kulima wenyewe, kisamvu tunachuma kwa jirani, oicha ya samaki tunayo ukutani. au tunakula kwa kuona picha ya bushii>? au jamaa akibembea jamaica?
 
Ndugu Watanzania nimategemeo yangu wengi amabao tumekua tukifuatilia kampeni za uchaguzi za CCM kila amapohutubi JK hotuba zake zote zimejaa ahadi.Tutanunua meli ya kisasa ziwa victoria,nitatwanunulia trekta,nitajenga treni ya kisasa,nitajenga nyumba bora kwa walimu,nitawaleatea maji kutoka ziwa victoria,nitajenga barabara n.k.Hapa inafahamika kwanini anaweza kutoa ahadi hizo bila aibu na kujiamini.Kwa sababu AHADI ZOTE HIZO HAZINA DHAMANA(GUARANTEE)Baada ya miaka mitano hatakua Rais na wala hawajibiki kwa ahadi alizozito na CCM wataturuka na kusema ahadi hizo alizitoa JK muulizeni JK,Mwacheni mzee wetu apumzike n.k.Miaka mitano ya mwanzo katika uongozi wake inatosha kumpima katekeleza vipi ahadi zake.Na damana hapa ilikua ni miaka mitano mingine.Tuzipime ahadi zake za muhula wa kwanza zimetekelezwa kwa kiwango kipi?Hapo ndipo tutaelewa tumpe au tusimpe kura zetu.AHADI ANAZOZITOA HIVI SASA HAZINA DHAMANA NI UDANGANYIFU MTUPU TUSIDANGANYIKE BAADA YA MIAKA HATUTAKUA WA KUMUULIZA MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Ndugu Watanzania nimategemeo yangu wengi amabao tumekua tukifuatilia kampeni za uchaguzi za CCM kila amapohutubi JK hotuba zake zote zimejaa ahadi.Tutanunua meli ya kisasa ziwa victoria,nitatwanunulia trekta,nitajenga treni ya kisasa,nitajenga nyumba bora kwa walimu,nitawaleatea maji kutoka ziwa victoria,nitajenga barabara n.k.Hapa inafahamika kwanini anaweza kutoa ahadi hizo bila aibu na kujiamini.Kwa sababu AHADI ZOTE HIZO HAZINA DHAMANA(GUARANTEE)Baada ya miaka mitano hatakua Rais na wala hawajibiki kwa ahadi alizozito na CCM wataturuka na kusema ahadi hizo alizitoa JK muulizeni JK,Mwacheni mzee wetu apumzike n.k.Miaka mitano ya mwanzo katika uongozi wake inatosha kumpima katekeleza vipi ahadi zake.Na damana hapa ilikua ni miaka mitano mingine.Tuzipime ahadi zake za muhula wa kwanza zimetekelezwa kwa kiwango kipi?Hapo ndipo tutaelewa tumpe au tusimpe kura zetu.AHADI ANAZOZITOA HIVI SASA HAZINA DHAMANA NI UDANGANYIFU MTUPU TUSIDANGANYIKE BAADA YA MIAKA HATUTAKUA WA KUMUULIZA MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Nitanunua bajaj 400 (dili za kina Manji)
Nitajenga Chuo Kikuu Shinyanga

Hivi huyu jamaa akili yake nzuri kweli?
 
Back
Top Bottom