Operesheni KuKu (kufa kupona). riwaya ya kijasusi

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,687
Points
2,000

Kudo

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,687 2,000
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA


SIMU; 0758573660

SEHEMU YA SITA


--EAGLE WING HOUSE-DAR—


Mwanamke aliependeza kwenye sare zake za jeshi alishusha mkonga wa simu ya mezani huku uso wake ukiwa umejikunja na mdomo wake akiwa ameupeleka mbele kama kalambishwa konyagi.

Akakalia kiti chake cha kuzunguka na kuweka miguu juu ya meza iliokuwa mbele yake huku mikono yake akiufumbata pamoja na kuilaza juu kidogo ya kinena kisha macho yake yakatua juu ya ukuta na kukutana na picha ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mwanamama yule mabegani mwake alikuw na kola yenye ngao (bibi na bwana) kisha nyota tatu kumaanisha cheo chake kilikuwa Brigedia Jeneral na juu kidogo ya mfuko wa vazi lake la juu kulikuwa kuna jina lake.

Alikuwa ni Brigedia Jeneral Hawa Maiga.

Muda huo alikuwa ametoka kuwasiliana na simu mbili huku simu ya kwanza ikiwa ni kutoka nchini Congo kwenye vikosi vya umoja wa mataifa na kuarifiwa kuwa mkubwa wa waasi Chepe alikuwa amegoma kuzungumza nao hivyo walikuwa hawajui ni nini shida yake kwa waandishi wale.

Bi Hawa Maiga alishindwa kuelewa kama Chepe alishindwa kuzungumza ni kwa kuwa amejua aina ya watu aliowateka ama anahisi tu.


Bi. Hawa Maiga alimtambua vyema Chepe kuliko mtu yeyote na alijua ni lazima Chepe atakuwa amejua wale ni Zedi na Mina kutoka kwenye kitengo chake cha MI chini ya mwamvuli wa special operations..

“Lakini nimekutengeneza mimi Chepe na huwezi kushindana na mimi hata kidogo, uliowaua wanatosha, familia zao zimelia vya kutosha nisingependa tena damu imwagike ni lazima nikutie mikononi hata kwa kuingia mi mwenyewe” Brigedia Jeneral Hawa Maiga alijisemea huku akitikisa mguu wake wa kulia na kwa waliomfahamu hapo walijua yupo kwenye kiwango cha mwisho cha hasira na hata ukimzingua unaweza kuchezea risasi ama mbata za kutosha.

Bi Hawa pia alikuwa amepiga Simu kwa Kamishina Zenge wa Zenge ambae nae alikuwa ni msimamizi wa operesheni maalumu upande wa jeshi la polisi huku yeye akiwa ni msimamizi wa operesheni maalumu upande wa jeshi yani Military intelligence (MI).

Kwa nini walishirikiana?

Kwa sababu vijana wa special operations walikuwa ni wale wale huku wakijigawa kimajukumu kulingana na uzito wa kazi kila pande hivyo wakiwa chini ya Zenge wa Zenge walipaswa kufanya kazi za kipolisi na wakiwa chini ya Hawa Maiga wanafanya kazi za jeshi kikamilifu kwa kuwa wote walikuwa ni makomando waliofuzu kila idara na pia walikuwa wameiva kwenye mafunzo ya ujasusi na upelelezi.

Simu aliopiga ilimhitaji Kamishina afike makao makuu yao wote kwa kikao chao cha dharura kuhusu jambo lile.

Na kikao kile ndicho kilizaaa balaa na kizaaa zaa kikubwa ndani ya Dar na nchini Congo na ikawa ni operesheni kufa kupona iwe jua iwe mvua.

****
Kamishina Zenge wa Zenge aliingia kwenye ofisi ya Bi Hawa Maiga zikiwa zimebaki sekunde chache kutimia saa moja tangu alipopokea simu ya wito kutoka kwa Bi Hawa Maiga wa kitengo cha special operations ndani ya idara ya MI katika jeshi la wananchi.

Alikaa kwenye kiti bila kukaribishwa huku akitupa bareti yake karibu na miguu ya Brigedia Jenerali Hawa Maiga.

“Usiniambie kama hii ni priority Red!!” Kamishina Zenge wa Zenge alianzisha mazungumzo huku salamu ikiwa si kipaumbele chao wakati huo.

“Yes!! Ni priority red Kamishina!!” Hawa alijibu huku akishusha miguu kwenye meza na kumtazama Kamishina Zenge wa Zenge.

“So!!” Zenge alihoji hivyo..

“Rescue team!! Nadhani ndo kipaumbele chetu kwa sasa kwa sababu spies are blacked!!” Brigedia Hawa Maiga alimwambia Kamishina Zenge wa Zenge.

“Why!?” Kamishina aliuliza.


“Kila wanaokanyaga maguu kule Beni wanarudi vichwa chini kwa kifo ama vilema,idara ipo hoi sasa!!” Brigedia alijibu.

“Unataka kusema nini juu ya Mina na Zedi?” Kamishina aliuliza huku akiwa ametoa jicho kuashiria hakupenda kusikia habari mbaya kuwahusu.

“Mitambo ilitoa taarifa ya kuwa wao wapo matatizoni na ni ngumu kupona!!” Hawa Maiga alijibu.

“What!!!” Zenge wa Zenge alishangaa.

“Kompyuta ya malkia ilitoa mlio kuashiria moja ya vijana wa special op,yupo matatizoni na wataalamu walipojaribu kufuatilia waligundua ni kompyuta ya Mina ndio imetoa taarifa na tulipojaribu kifuatilia kwa Sattelite ilionesha ipo kwenye msitu wa Ndeko magharibi mwa Butembo!!” Brigedia Hawa Maiga alisema huku akichomoa picha mbili kutoka kwenye makabrasha yaliokuwa karibu na mikono yake..

Picha zile alimrushia Kamishina Zenge wa Zenge.

Zenge wa Zenge alizichukua picha zile na kuzitazama.

Picha zote zilikuwa ni za mtu mmoja ila isipokuwa picha moja ilikuwa ni ya mtu akiwa na mavazi ya jeshi la wananchi huku juu kidogo ya bega lake la kushoto kukiwa kuna mchoro wa ndege aliechanua mabawa hewani.

Hiyo ilimaanisha yule mtu alikuwa ni komando wa daraja la juu sana akiwa amefuzu hatua zote za ujasusi na ukomando. Na picha ya pili ilikuwa ni ya mtu yuleyule ila akiwa amevaa kanzu nyeupe na baragashia; lakini mtu yule alievaa kanzu alikuwa amevaa na kiziba jicho cha rangi nyeusi na mikanda ilionekana kupita kushoto na kulia ili kushikilia kizibo kile.

“Hii ina maana gani!!” Kamishina aliuliza baada ya kutoelewa kinachoendelea..


“Huyo ndie Chepe Mazonge; ambae ndie kiongozi mtendaji wa kikundi cha waasi nchini Congo!!”Bi Hawa alifafanua.

“Muasi Congo? Sa mbona anamavazi ya jeshi letu?” Zenge wa Zenge alihoji.

“Aliwahi kuwa hapa na pia nimemlea mimi hadi alipofikia kuasi na kukimbilia msituni huko Congo hivyo anatujua vizuri sana huyu jamaa!!” Bi Hawa alifafanua tena kuhusu picha zile.

Kamishina alijikuna kichwa kwa kidole cha mwisho huku akili yake ikicheza sombolo bila kupata majibu..


“Usitake kunambia kambi zetu zilizokuwa zinavamiwa aliongoza yeye!!” Kamishina alitoa hoja kwa wasiwasi.

“Ndo yeye huyo na kubwa anaua kila mtanzania anaehisi ni shushu bila kuwa na hakika!!” Bi Hawa alijibu.
.
“Ajabu hii!!” Kamishina alishangaa.


“Kwa hiyo unasemaje labda!!” Kamishina alihoji.

“Zedi na Mina kuwa chini ya Chepe ni kuliangamiza taifa,mi nadhani tupeleke huko kikosi maalumu kuwakomboa na ikibidi kumchakaza huyu jamaa.” Bi Hawa alimwambia Kamishina.

“Una hisi hilo ni wazo sahihi katika kipindi hiki?” Kamishina alihoji.

“Hakuna namna tena ya kupeleka jasusi wakati kila anaetia maguu kwenye anga za Chepe anarudi akiwa mbali na Dunia!!” Hawa Maiga alimwambia Zenge wa Zenge.

“Afu huyu Chepe ni mtu ambae alifanya kazi ya ujasusi kwa kiwango kikubwa sana, hivyo anajua ABC za kazi hii na kupeleka jasusi wengine ni kuwauza tu bila kuwahurumia.” Brigedia alimwambia Kamishina.

Kamishina alifikiria kidogo kisha akasema
“Na kwa nini huyu jamaa anawagundua vyema majasusi wetu kiasi hicho?”

“Hujuma Kamishina;tunahujumiwa kuanzia mamlakani hadi huko Duniani!” Brigedia Hawa Maiga alimwambia Kamishina Zenge wa Zenge.

“Kama tuhujumiwa kuanzia hapa basi tuna kazi kubwa sana ya kufanya.” Kamishina alisema huku akichukua simu yake na kutazama muda.

“Nadhani tunapaswa pia kufanya jambo ili kuondoa hujuma hizi!” Kamishina alisema.

“Unadhani tutaweza vipi?” Brigedia jenereli Hawa Maiga alihoji.


“Siku za karibuni nitamhitaji Honda Makubi ambae yupo masoni Israel lakini pia ni mtu anaeifahamu sana Congo,nadhani anafaa kuanza na hili jambo!!” Kamishina alimwambia Hawa Maiga.

“Ni sawa mawazo yako lakini kuna kitu tunasahau Kamishina.” Hawa Maiga alimwambia Kamishina Zenge wa Zenge.

“Jambo gani!!” Kamishina aliuliza.

“Alienyuma ya Chepe ni nani na anatokea nchi gani au ni nchi gani ilioko nyuma ya Chepe na Chepe kikundi chake kinaitwaje na kwa nini hadi sasa wanafanya kazi nyuma ya migongo ya waasi wengine?” Bi Hawa Maiga alimfafanulia Zenge wa Zenge.

“Yes!! Inafikirisha hii.” Kamishina aliitikia.

“Ni lazima tujue nguvu anatoa wapi na ni wapi anapata taarifa nyeti za uwepo wa madini kwenye sehemu vinapoweka mahema vikosi vya kulinda amani kutoka Tanzania!!” Bi Hawa alimwambia Kamishina.

“Kuna tatizo sehemu Brigedia na hatuna namna zaidi ya kujua ni wapi tunapopigiwa!!” Kamishina alimwabia Hawa Maiga.

“Hakuna kungoja inabidi operesheni kubwa ifanyike ili tuwakomboe Mina na Zedi.” Hawa aliendelea kusisitiza lengo lake.

“Sawa fanya kile kinachostahili kufanywa!” Kamishina alijibu huku akisimama na kisha wakapigiana saluti na kila mmoja akaendelea na shuguli zake.


Baada ya kamishina Zenge wa Zenge kutoka ofisini kwake; Brigedia jenerali Hawa Maiga alichukua ramani moja iliokuwa mezani kwake kisha akaelekea kwenye chumba cha mkutano katika ofisi ile na kisha akaandika ujumbe kwenye simu yake na kuusambaza kwa watu sita aliowahitaji muda huo.

Haukuchukua hata dakika arobaini, tayari chumba kilikuwa kimetimia wanaume sita huku mtu wa saba na akiwa ni mwanamke pekee akiwa ni Bi Hawa Maiga mwenye cheo cha Brigedia Jeneral.

Wanaume wale walikuwa wamejazia vyema miili yao huku nyuso zao zikionesha ukomavu wa hali ya juu katika medani za kivita.

Wanaume wote walikuwa na alama ya ndege akipaa kwenye mabega yao huku chini yake kukiwa kuna michoro ya jambia zilizopishana.

Ilimaanisha Bi Hawa alikuwa amekutana na timu ya makomando walio chini ya kitengo chake anachokiongoza cha Military intelligence na special operations.

Brigedia Hawa Maiga akawatazama wote baada ya kila mmoja kutoa saluti kwake na kukaa.

Aliwatizama mmoja mmoja huku akijaribu kuona kama nyuso zao zinaweza kuwa tayari kwa kile alichowaitia pale.

Bi Hawa Maiga alihitaji kufanya operesheni ya siri nchini Congo huku lengo lake likiwa ni kuwakomboa Zedi Wimba na Mina; watu ambao aliwathamini kuliko ngozi yake na aliamini wakibanwa wanaweza kutoa mengi kwa Chepe ambae hakuna anaejua uasi wake kama utaishia huko Congo ama utaibuka hadi hapa nchini mana ni yeye pekee aliejua kwa nini Chepe aliamua kuasi jeshi na mabishano yao yalikuwa ni nini hadi Chepe akamua kuvunja mkeka.

Bi hawa aliita Roger Team 6. Kikosi maalumu kwa kazi maalumu na hakijawahi kushindwa huku operesheni yao ya kukumbukwa ni ile ya kumkomboa Waziri wa ulinzi Kenya aliekuwa anazuiliwa na kikundi cha waasi wa Al shabaab huko Somalia na timu hii ikapewa kazi moja tu kuhakikisha waziri anarudi salama nchini mwake huku kazi ile ikiwa inajulikana na Rais wa Kenya na watu wachache nchini ili kuondoa hujuma ambazo Rais wa Kenya alizigundua kwenye baraza lake la mawaziri.

Timu hii haijawahi kumuangusha Bi Hawa Maiga na haijawahi kupoteza mpiganaji wake hata mmoja.

Roger Team 6 ilikuwa inaongozwa na Luteni Rambo (code name) ambae jina lake halisi aliitwa Zuri Sanadi.

Rambo hakuwahi kufeli katika misheni zote alizowahi kuziongoza.

Rambo mara nyingi hakupenda kikosi kiitwe timu 6 wawapo kazini bali alipenda kuita kikosi chake “BAMBADIKA” ikiwa na maana ya Shimo la Mamba; msemo maarufu sana huko Gambia na wao walijiona ni sawa na shimo hilo kwa kuwa adui kwao hajawahi kupona kila walipomweka kwenye rada za kuingia kwenye shimo hilo.

Bambadika chini ya Rambo walikuwa kimya kungojea maelezo toka kwa Brigedia Jeneral Hawa Maiga.

Wakati Bi Hawa akiweka akili sawa kutuma kikosi chake nchini Congo; Kamishina Zenge wa Zenge nae alikuwa anamalizia kuwasiliana na Komando na Jasusi Honda Makubi aliekuwa Israel kwa mafunzo maalumu baada ya kuwa ametoka kuuguza majeraha yake alioyapata huko Somalia katika mkasa wa Urithi wa Gaidi.

Ujio wake ilikuwa ni kawaida kwake yeye na Kamishina ila ilikuwa ni taharuki kwa majahili na wazandiki waliokuwa wanacheza na kitengo cha kazi maalumu “Special operations”.
 

kanonb

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Messages
349
Points
500

kanonb

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2016
349 500
Kama kawaida yangu Honda huwa na cheza kama rescue nipo njiani nakuja msohofu hao madogo akina Zedi na Mina watuliage tu (Maadui ninawaandalia putinga putuluu ya dasheee) saa za jion hv nitakuwa field
 

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,687
Points
2,000

Kudo

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,687 2,000
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA SABA
Rambo hakuwahi kufeli katika misheni zote alizowahi kuziongoza.

Rambo mara nyingi hakupenda kikosi kiitwe timu 6 wawapo kazini bali alipenda kuita kikosi chake “BAMBADIKA” ikiwa na maana ya Shimo la Mamba; msemo maarufu sana huko Gambia na wao walijiona ni sawa na shimo hilo kwa kuwa adui kwao hajawahi kupona kila walipomweka kwenye rada za kuingia kwenye shimo hilo.

Bambadika chini ya Rambo walikuwa kimya kungojea maelezo toka kwa Brigedia Jeneral Hawa Maiga.

Wakati Bi Hawa akiweka akili sawa kutuma kikosi chake nchini Congo; Kamishina Zenge wa Zenge nae alikuwa anamalizia kuwasiliana na Komando na Jasusi Honda Makubi aliekuwa Israel kwa mafunzo maalumu baada ya kuwa ametoka kuuguza majeraha yake alioyapata huko Somalia katika mkasa wa Urithi wa Gaidi.

Ujio wake ilikuwa ni kawaida kwake yeye na Kamishina ila ilikuwa ni taharuki kwa majahili na wazandiki waliokuwa wanacheza na kitengo cha kazi maalumu “Special operations”.


----------

Roger team 6 walikuwa katikati ya mazungumzo huku kila mara vidole vyao vikisonta kwenye ramani iliokua mezani kwao na wao wakiwa wameizunguka kwa mtindo wa mwezi mchanga yani nusu duara huku Bi Hawa Maiga akiwa ameshika pembe moja ya ramani ile kwa mkono wa kushoto na mkono wa kulia ukiwa umeshika kalamu ya mkaa na kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwaelekeza kila nukta na umuhimu wake katika ramani ile.

“Nadhani sasa tutakuwa tumeelewana kuhusu kambi hii na ni wapi mateka wetu watakuwa!” Bi Hawa aliwambia vijana wa timu 6.

“Lakini ni vipi kama mateka hawa watakuwa wameondolewa kwenye kambi hii ama kwenye nyumba hii na sisi tageti kubwa ipo kwenye nyumba hii?” Rambo ambae ndie kiongozi wa kikosi hiki aliuliza.


“Taarifa nilionayo si ya kupepesa kabisa na hii ndio kambi yao kubwa na mateka wote huwa wanawekwa humo na nasikia kuna shimo kubwa sana linaitwa hole of death!” Bi Hawa aliendelea kuwapa taarifa kuhusu kambi ya Chepe huko mjini Beni.

“Kumbukeni hii ni rescue mission na isizidi dakika thelathini na kisha mtaelekea point b kusini mwa kambi hii huko mtakuta usafiri na mtarejea wote na ni matumaini mtarejea mkiwa salama” Bi Hawa aliwasisitiza vijana wake huku akiwapigapiga vifuani mwao kuwapa ari ya mapambano.

Baada ya mazungumzo muhimu ilibidi Rambo achukue vijana wake watano na kuelekea chumba cha mazoezi na huko wakatayarisha nyumba kadhaa za bandia zikiwa sawa na zile ambazo zilionekana kwenye picha na pia ramani ya kuingia na kutoka ndani ya eneo lile.

Walipaswa kufanya mazoezi kuanzia muda ule hadi jua litakapozama na kisha usiku huo ulikuwa ni usiku wa kufa ama kupona kwenye misitu ya Ndeko magharibi mwa mji wa Bulembo.

Mazoezi yao yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na baada ya hapo walipanga kupumzika kwa saa moja pekee ili kila mmoja asali sala zake kwa imani yake.

Ilipotimu saa mbili kamili usiku, kila mmoja aliamka na kwenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo ambapo huko ndo wangeenda kupeana majukumu upya wakiwa watu sita pekee.

Baada ya kuingia kwenye kile chumba walijifungia ndani kisha wakaanza kuvaa kikazi huku kila mmoja akichagua kile alichoona kinamfaa wakati huo.

Makomando wote wakavaa fullgear bila kuacha kitu hata kimoja huku wakiwa na kofia ngumu vichwani mwao na visu vyenye ramani au kijeshi huitwa Compass na kisha kila mmoja akaweka kibuyu cha maji kiunoni mwake au kizungu huitwa water bladder kisha wakachukua chemical mace ambayo ni mabomu madogo yenye moshi mzito kwa ajili ya kujikinga au kuwakimbia maadui katika uwanja wa vita.
Lakini makomando hawa hawakusahau camouflage pants ambazo zilikuwa ni rangi za kujipaka usoni mwao na zoezi la kujipaka lingeendelea hukohuko ndani ya ndege kabla hawajashuka chini.

Na mwisho kabisa kila komando alichukua strob light ambayo ilikuwa ni mlipuko wa hewani wenye mwanga mkubwa ukiwa na kazi ya kutoa taarifa endapo wangepoteana au kumulika mbele kuona adui alipojificha.

Walikamilika kwa kila kitu vijana hawa waliojiita bambadika au shimo la mamba.

Yani ukikutana nao ni sawa umeingia kwenye shimo la Mamba.


“Tukishuka hapa inabidi nyoka wetu watangulie na kisha watatupa taarifa ya hali ilivyo kisha na sisi tutasonga mbele kwa kupitia njia hii ambayo ni salama kwa mujibu wa taarifa tulizonazo.” Luteni Zuri codename Rambo aliwambia vijana wake huku nyokaa akimaanisha wadunguaji wawili waliokuwa kwenye hicho kikosi cha watu sita.

Vidole vya Rambo vilizidi kuonesha maeneo yao ya kimkakati ili iwe rahisi kwao kuingia na kutoka salama ndani ya kambi ya Chepe.

“Mdunguaji wa kwanza ambae ni Rat atakuwa usawa wa lango la kambi na akiwa hapo atatuona vyema sana akiwa juu ya miti na kazi yake ya kwanza ni kuwaondoa walioko kwenye vidungu vitatu vililivyoko mbele ya kambi hii!” Rambo aliwambia huku akimsonta Tendwa ambae codename alikuwa ni Rat.

“Na wewe Pete utakuwa nyuma ya kambi nako kuna vidungu vitatu na ukiwa huko pia utahakikisha tunapita salama kabisa na kuingia kwenye nyumba kuwachukua watu wetu!” Rambo alimwambia Sauli codename yake akijijulikana kama Pete na alikuwa ndie mdunguaji wa pili.

Rambo aliendelea kutoa maelezo yake kwa wale wapiganaji wengine watatu ambao codename zao walikuwa ni Paroko;shotii na Odwe.

Walipokuwa kamili walichukua silaha zao na kutoka ndani ya makao makuu ya vikosi maalumu ambapo nje walikuta gari maalumu lililowabeba na kuwapeleka kwenye kambi ya jeshi la anga kisha wakaachwa hapo.

Punde wakaja makamanda wawili waliowaongoza kwenye ndege ya kivita ya F-32jet fighter yenye kasi ya ajabu bila kutoa mlio wala kuonwa na rada za nchi nyingine pindi wakiingia anga lao.

Walipanda ndani ya ndege ile ikiwa ni saa tatu na nusu huku wakitarajia kufika Congo saa sita kasoro na operesheni kutekelezwa saa Saba au saa nane usiku.

-------

BENI-CONGO.

Ndege iliobeba makomando wa Roger timu 6 ilikuwa inatambaa kwenye anga la jimbo la Kivu kaskazini na tayari rubani alikuwa ameshawapa taarifa wapiganaji wale wajiandae kwa kuvaa maparachuti kwa ajili ya kushuka chini.

“nyokaa inabidi watangulie!! Komandoooo!!” Rambo alitoa maagizo kisha akamalizia na kibwagizo cha kujipa ari.

“Nguvu mojaaa!!” Waliitikia kwa pamoja huku wakigonganisha mikono yao ya kulia kwa kukunja ngumi.

Nyuso zao zilijaa michoro ya rangi nyeusi na mikono yao ilikuwa imevikwa glavu zilozokatwa vidoleni.

Kila mmoja alininginiza silaha yake iliokuwa imevikwa kifaa maalu cha kuonea gizani (Night vision Goggles).

Sajenti Abas codename Odwe alikuwa anamalizia kuvaa mikanda ya parachuti lake kuzunguka kifuani na bahati mbaya au nzuri alitupia jicho lake kwa wenzake ambao walikuwa wanajikagua kujipa uhakika wa mafundo yao wasije anguka vibaya au kupoteza mwelekeo.

Muda huo kengele ya kujitayarisha ilikuwa imeshalia na taratibu mlango uliokuwa chini nyuma ya ndege ile ukaanza kufunguka hivyo kufanya upepo uanze kuingia kwa nguvu ndani ya ndege kiasi kupeperusha baadhi ya vitu vilivyokuwa mle ndani.

Odwe alipagawa kidogo kwa kile alichokiona kwa komando mmoja wao na ndie alikuwa anajiandaa kuruka.

“Petee!! Funga vizuri mrukooo!!” Odwe alipaza sauti ili kushindana na upepo na sauti yake isikiwe na komando Pete ambae alikuwa ni mdunguaji.

Odwe alikuwa ameona Pete kakosea kufunga mkanda mmoja na endapo angeshuka hivyo hivyo basi angepoteza uelekeo ama kushindwa kutua salama chini ya ardhi.

Kukosea kupo ila kwa nini iwe katika ile misheni?

“Yeeehaaa!!” Rat ambae alikuwa ni mdunguaji mahiri kabisa alijiachia huku akipiga ukunga wa ari.

“Nooo!! Pete! Nooo!!” Odwe alipiga tena kelele kumzuia Pete asiruke katika hali ile ya kutokufunga vyema mikanda ya parachuti lake.
Ila alikuwa amechelewa kwa mbwembwe kabisa Pete alijirusha na kupotelea chini.

“Ooho kwanini Pete!! Aagh!!” Odwe alilaani kitendo kile huku akianza kujiona ni mwenye lawama kwa kuwa alishindwa kumtahadharisha mapema Pete.

“Go Kamanda!!” Rambo alimstua Odwe ambae alikuwa bado anashangaa wenzake wanavyoruka huku yeye akimuwaza Pete.

Nae bila ajizi akajirusha kwa nguvu na kupepea angani huku nyuma yake akifuata Rambo.

Makomando watano walianguka sehemu moja huku komando mmoja akikosekana na alikuwa ni wa mwanzo kabisa kujirusha chini.

“Yuko wapi Pete?” Rambo alimhoji Rat.

“Nimeshuka mwenyewe na akafuatia Paroko; yeye sijamuona” Rat alijibu.

“Guys,it’s a problem!” Rambo aliwambia wenzake.

“Yah! Ni tatizo tangu tulipokuwa angani” Macho yote yakamtazama Odwe aliesema hivyo.

“Kelele zote mlizosikia napiga zilikuwa ni kumkumbusha Pete afunge vyema mkanda wake mmoja na nilipoona anadive nikajua tutamkosa!” Odwe alifafanua.

“Ooh shit!!” Kila mmoja alitamka kivyake.

“Tumjaribu kwenye simu yake!” Paroko alishauri huku akichomoa simu ya upepo kiuoni mwake na kisha kujaribu kupiga.

Wote walikuwa makini kufuatilia matokeo.

Ikawa sivyo walivyogegemea, simu ikaendelea kuonesha taa nyekundu kisha ikamulika mara tatu na kuzima kabisa.

Makomando wakaingiwa na fadhaa.

Simu ya Pete ilikuwa haipatikani.

Makomando wale walijitoa pale walipokuwa na kutambaa chini kidogo kisha wakatulia tuli huku wakitizama anga kuona kama wataona mwanga wowote wenye kuwaashiria lolote hasa kwa Pete.
Odwe bado fikira zake zilikuwa kwa Pete na aliona kabisa Pete ni kama alifanya makusudi hivi kuvaa vile na hata pale alipomwita aligeuka na kumchekea kabla hajajirusha.

“Guys,this thing was planned!” Odwe aliwambia wenzie.

“Tusifike huko wapendwa! Tupo pamoja kwa miaka mingi sana na hatujawahi kudouble cross why leo? Ni mistake tu ndogo!” Rambo alikemea huku akizungumza kwa sauti ya mamlaka.

Na mjadala ukakomea pale.

Lakini kwa nini Pete aliamua kufanya vile ni makusudi ama bahati mbaya? Na kama ni bahati mbaya kwa nini iwe ni katika misheni hii na siku huko nyuma.

Pete hayupo na hakuna wa kuwajibu.
 

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2009
Messages
6,929
Points
2,000

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2009
6,929 2,000
Pole Sana kama huwa nakukwaza hadi uone naringa kiasi hicho!!

Pia nisamehe kwa maringo yangu yanayokukwaza!!.

Tazama sehemu ya tatu jana nimejitahidi kuiposti saa saba usiku nadhani utaelewa kwa nini iwe huo muda wewe ukiwa umelala.

Lakini nisamehe pia kwa kuwa huwa naipeleka whatsapp wakati wewe unataka usome bure kabisa bila hata kunitumia vocha ya kukwangua nijiunge ili usome!!

Lakini pia naomba nikuulize upo nchi gani ambayo huwezi kupata mia tano tu (500) ya kununua riwaya mwanzo mwisho?.
Huna whatsapp tumia email, huna email tumia whatsapp..

Nchi yoyote Duniani unaweza kunitumia na nikapata mia tano tu, au elfu moja ikizidi sana huwa elfu mbili.

Na mwisho nikukumbushe kuwa hii ni kazi kama kazi zingine wala si kufurahisha watu bure, ndo mana ili uandike lazima ufanye utafiti kwa kina ikibidi usafiri mkoa au nchi kutafuta ukweli wa kile unachotaka kuandika.

Nadhani umeona kuna mdau huko juu kanitisha kwamba naandika vitu deep sana, unadhani nikiandika kwa kukurupuka bila tafiti nitapata vitisho hivyo ambavyo watu wanakuja hadi pm kuniomba nipunguze ukweli katika riwaya zangu hizi? Unajua garama inayotumika hadi naandika kitu kinachokuvutia bila kukutoa kwenye reli ya usomaji?.

Lakini dada yangu nikwambie kitu, duniani hakuna kitu cha bure na ndo mana hapa Jf unanunua vocha na bado google wanakulipia ili uingie bure kwa kuwa wanamlipa Melo. Kama wasingekuwa wanamlipa basi tungeingia kwa kulipia kama zilivyohuduma zingine duniani za kupata habari!!!

Narudia tena kukuomba radhi kama nimekukwaza ama nimekwaza yeyote kwa utaratibu wangu huu, ila hii ni kazi kama kazi zingine na ndo mana ina hati miliki kila kazi unayoona naweka hapa na huko pia nalipia ili kulinda kazi yangu.

Hivyo nisamehe bure kwa maringo yangu yanayokukwaza lakini jifunze kuheshimu kazi za watu bila kutoa lugha ya kuudhi ama kukera. Wapenzi wa riwaya hawana lawama wanajua ugumu wa kazi na faida wanazopata kwa kusoma kazi za wengine!!.

Afu mi niko poa Sana sema gubu lako tu, mimi wengi nimekuwa nawapa bure kama hawana pesa!! Waniomba kistarabu tu nawaelewa!!
Wapo hapa labda watakupa ushuhuda wa vile nilivyo.

Lakini pia kuna wezi wa kazi za watu, ukiweka hadi tamati anachukua na kuwek kwenye page yake au blog na kuuza! ....


Nimeamua kukujibu kirefu ili unielewe na wengine wenye kuniona nina maringo nao wajue kwa nini ipo hivyo!! Hakuna mwandishi anaetoa bure siku hizi,hii ni kazi kama kazi zingine!!

Nisameheni wote niliowakwaza!!
Pole Sana mkuu, watu hawajui kuthamini muda wa wengine. Vumilia then keep it up.

Nipe utaratibu wa kuipata simulizi nzima asee. Unaweza kuniPM if possible.
Thanks.
 

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,687
Points
2,000

Kudo

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,687 2,000
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA NANE


Makomando watano walianguka sehemu moja huku komando mmoja akikosekana na alikuwa ni wa mwanzo kabisa kujirusha chini.

“Yuko wapi Pete?” Rambo alimhoji Rat.

“Nimeshuka mwenyewe na akafuatia Paroko; yeye sijamuona” Rat alijibu.

“Guys,it’s a problem!” Rambo aliwambia wenzake.

“Yah! Ni tatizo tangu tulipokuwa angani” Macho yote yakamtazama Odwe aliesema hivyo.

“Kelele zote mlizosikia napiga zilikuwa ni kumkumbusha Pete afunge vyema mkanda wake mmoja na nilipoona anadive nikajua tutamkosa!” Odwe alifafanua.

“Ooh shit!!” Kila mmoja alitamka kivyake.

“Tumjaribu kwenye simu yake!” Paroko alishauri huku akichomoa simu ya upepo kiuoni mwake na kisha kujaribu kupiga.

Wote walikuwa makini kufuatilia matokeo.

Ikawa sivyo walivyogegemea, simu ikaendelea kuonesha taa nyekundu kisha ikamulika mara tatu na kuzima kabisa.

Makomando wakaingiwa na fadhaa.

Simu ya Pete ilikuwa haipatikani.

Makomando wale walijitoa pale walipokuwa na kutambaa chini kidogo kisha wakatulia tuli huku wakitizama anga kuona kama wataona mwanga wowote wenye kuwaashiria lolote hasa kwa Pete.
Odwe bado fikira zake zilikuwa kwa Pete na aliona kabisa Pete ni kama alifanya makusudi hivi kuvaa vile na hata pale alipomwita aligeuka na kumchekea kabla hajajirusha.

“Guys,this thing was planned!” Odwe aliwambia wenzie.

“Tusifike huko wapendwa! Tupo pamoja kwa miaka mingi sana na hatujawahi kudouble cross why leo? Ni mistake tu ndogo!” Rambo alikemea huku akizungumza kwa sauti ya mamlaka.

Na mjadala ukakomea pale.

Lakini kwa nini Pete aliamua kufanya vile ni makusudi ama bahati mbaya? Na kama ni bahati mbaya kwa nini iwe ni katika misheni hii na siku huko nyuma.

Pete hayupo na hakuna wa kuwajibu.

Waliendelea kusubiri kwa zaidi ya dakika kumi bila kuona lolote likiendelea ama ishara yoyote ambayo ingeweza kuwaarifu uwepo wa Pete maeneo yale au mbali na pale.
Makomando wale watano waliona kuendelea kukaa pale ni kupoteza wakati na watakuwa ni kinyume na muda waliohitaji kuutumia kukamilisha mpango wao.

Rambo alitoa ishara kwa wenzake na wakajikusanya kwa pamoja ili wapange upya mipango yao. Waliamua kujipanga upya kwa kuwa mwenzao mmoja hakuonekana, na hawakujua alipo usiku huo. Ilikuwa ni lazima wajipange upya tena ili kuona namna ambavyo wanaweza kukamilisha misheni yao, bila kuwapo mdunguaji mmoja.

“Odwe inabidi ukae upande ule ambao alitakiwa awepo Pete na unatakiwa utumie ujuzi wako wote kuhakikisha wapiganaji walioko kwenye vidungu wanatoka;mimi na Paroko tutakuwa sambamba huku shotii ukiwa nyuma yetu kuhakikisha usalama zaidi.” Rambo alielekeza upya na baada ya hapo kila mmoja aligeuka na kuanza safari msituni.

Ilikuwa ni safari ya kimya kimya huku vizuizi vya hapa na pale wakivikwepa. Iliwapasa watumie nusu saa kufika usawa wa kambi ya waasi,ila wakiwa wamebakiza kama dakika kumi kuifikia kambi, kuna kitu Shotii alihisi nyuma yake, haraka akapiga sauti ya hisi “psii” na makomando wote kwa pamoja wakaruka kila mtu kivyake na kuangukia katikati ya nyasi kisha kila nmoja akatulia tuli, kusubiri ishara zaidi.

Shotii ambae katika msafara ule alikuwa nyuma, alikuwa amehisi uwepo wa mtu mwingine zaidi nyuma yao, ila kila alipojitahidi kugeuka na kutazama, hukuona mtu.

Lakini masikio yake bado yalizidi kuhisi uwepo wa nyayo ngeni katika msafara wao na ndipo akawapa ishara wenzake na wakachukua tahadhari kila mmoja na upande wake.

Ni Shotii tena aliesimama na kuwapa ishara wenzake ya kuwa mambo ni shwari. Lakini licha ya ushwari huo bado hakuacha kuwatahadharisha uwepo wa kiumbe nyuma yao.

Safari iliendelea kwa umakini zaidi, na kila mmoja akiwa makini sana na mlango wa sita wa fahamu.
Tofauati na matarajio yao, kila kitu kilienda sawa na hakuna sauti wala mkwaruzo uliowasumbua tena.

Licha ya utulivu wote huo, ila bado Odwe alikuwa na dukuduku moyoni. Yeye aliamini kabisa sauti iliokuwa nyuma yake,ilikuwa ni sauti ya mtu au watu na walikuwa wanawala miguu.

Walifika hadi sehemu waliokuwa wamepanga kuweka ukomo wa safari yao. Na kama kawaida ya kazi yao, mara nyingi sana wadunguaji ndio hutangulia kuangalia usalama kisha kutoa taarifa.

Rat alielewa cha kufanya; Haraka akakimbia msituni kwa kutumia kanuni maalumu za kujificha kwa adui.

Alifika sehemu alioona kwake ni sahihi kujificha, akaweka makao juu ya mti na kisha akajipaka dawa maalumu ya kuzuia kushambuliwa na wadudu wa usiku.

Akaweka sawa bunduki yake ya kudungulia umbali wa mita 1500. Ilikuwa ni silaha yake pendwa ya Sniper rifle 338 Lapua Magnum.

Silaha hii pia ilikuwa na darubini pandikizi yani eye piece lens.

Rat alitulia tuli huku akiangalia mazingira vizier na alipojiridhisha akaamua kuwaita wenzake ambao walipaswa kuingia ndani ya kambi. Akawasha simu yake ya upepo na kuwapa taarifa Rambo na wenzake, kisha akamtafuta Odwe ambae kwa upande wake nae alikuwa ameanza kucheza na uhai wa wapiganaji waliokuwa kwenye vidungu nyuma ya kambi.

Baada ya Rat kuwasiliana na Odwe; nae aliamua kuanza kazi ya kutungua wapiganaji wale ambao walikuwa wanazungusha taa za ulinzi huku na huko.

Kwenye kidungu cha kwanza na cha pili, alitumia dakika mbili tu kukamilisha kazi aliohitaji kuifanya. Tayari watu sita walikuwa hawana uhai kutoka kwenye bunduki matata ya Rat. Mdomo wa bunduki yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti, akauelekeza upande wa kushoto kwake na akataka kuweka vyema shabaha yake, akasita.

Kuna kitu aliona.

Alimuona mtu akiwa amevaa mavazi sawa na yale waliokuwa wamevaa wao.
Akatumia darubini ya kupandikiza kukuza ili apate kuona vyema.

Akaguna.

Akarejea tena kutazama, na hapo akajiridhisha kabisa ya kuwa amemuona Pete akiwa chini ya milingoti minne iliobeba kidungu.

“Ana fanya nini tena huyu!” Rat akajiuliza huku akichukua simu yake na kutaka kupiga kwa Rambo kumpa taarifa, akasita kwa mara nyingine.

Kwa nini!!!

Kwa sababu alimuona Pete akitega bomu pale chini.
Na alikumbuka kwamba wao hawakuwa wamebeba mabomu ya moto, zaidi walikuwa na mabomu bandia yaani plastic explosive.

Kwa nini!!

Kwa sababu hawakutaka wajulikane kama ni wao ndio wameendesha operesheni ile.

“Anafanya nini huyu bwege!!” Rat akajiuliza na kabla hajachukua uamuzi mwingine tena, alama nyekundu kwenye simu yake ikapata uhai kuashiria kuna simu nyingine inaingia.

Akabonyeza kitufe ubavuni mwa simu yake.

Alikuwa anapokea ujumbe kutoka kwa Odwe; Odwe alikuwa anampa taarifa ya kuwa upande wake amemaliza kazi,hivyo alibaki peke yake ambae anatakiwa atoe ripoti na kikosi cha chini kianze kazi ya kuingia ndani ya kambi.

Haraka Rat akaweka sawa bunduki yake na kulenga wapiganaji waliokuwa wamesalia kwenye kidungu kile.
Alipomaliza akashusha tena darubini yake pale alipokuwa Pete; Hakumuona.

Yawezekana ni kosa ambalo hakujua kama analifanya,badala ya kutoa taarifa ya kile alichoona, yeye akaruhusu Rambo; Paroko na Shotii wasonge mbele kuelekea kwenye nyumba ambayo waliiwekea tageti kwa nia ya kufanya wokozi.

Rambo aliinuka kidogo na kisha akanyoosha kidole kimoja juu, hapo waliokuwa nyuma yake wakajiweka sawa kisha akachezesha mkono ulionyosha kidole mara mbili kwa kwenda mbele.
Paroko alijua ni yeye anaepewa ishara ile na haraka akaanza kumfuata Rambo.
Hatua zao zilikuwa ni zenye uhakika huku darubini pandikizi walizofunga kwenye bunduki zao ambazo zilikuwa ni Night vision goggles, zikiwasawaidia kuona mbele huku wakikabiliana na kila mpiganaji aliekatiza mbele yao.

Baada ya kuingia ndani kabisa ya kambi ya waasi; Rambo na Paroko walifika pahali ambapo sasa walihitaji kutulia kidogo na kutazama mazingira kabla ya kuvamia nyumba ambayo ilikuwa na mateka.

Walitulia kwenye vifusi vilivyotengenezwa na waasi huku chini kukiwa kuna maiti mbili za wapiganaji waliokuwa pale kabla hawajakutana na mikono ya Paroko.

Wakati wao wakiwa wametulia pale, upande wa pili alikokuwa Rat kuna jambo lilikuwa linamtokea.

Ni wakati alipokuwa ametulia mafichoni, mara simu yake ikaanza kupokea mkoromo wa ajabu kuashiria kuna simu ngeni ilikuwa inaingilia mawimbi ya simu yake.
Taa ya kijani na nyekundu zikaanza kumweka kwa pamoja.

Ilikuwa ni ajabu kidogo, ila alijua ni yawezekana kuna mawasiliano ambayo yanataka kufanyika na mtu aliekaribu yake.

Akarejesha jicho lake kwenye darubini na alianza kupitia maeneo yote ya karibu yake kwa umakini mkubwa.

Hakuona lolote la kutisha.

Lakini bado simu yake ilizidi kukoroma mithili ya radio inayokata mawimbi yake.

Akawaza kuizima kwa muda, na wakati huohuo akiweka sawa darubini yake ili irekodi picha wakati akishugulika kuizima.

Akaizima kwa sekunde kadhaa kisha akaiwasha tena.

Aliporidhika ipo sawa,akarejesha macho yake kwenye darubini pandikizi na kuyarejea matukio ilionasa.

E bana ee!!

Sura ya Pete ilikuwa imeonekana akihama eneo moja kwenda jingine.

“Huyu bwege si atulie tu na tukimaliza tumshitue!!” Rat aliongea kwa kugafilika.

Simu yake ikakoroma tena, na safari hii ikafuatia na mkoromo wa simu nyingine pale chini alipokuwa.

Haraka akatazama pale chini na macho yake hayakuamini kile alichokiona pale.

Pete alikuwa na mtu mwingine wakitizama juu ya mti aliokuwa.

Hisia mbaya zikamtambaa na haraka akakumbuka onyo la Odwe kuhusu Pete.
Rat akataka kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja; alinyakua simu yake kiuononi na kidole kikaelekea sehemu ya kupigia na huku mwili wake wote ukitaka kujitoa kwenye tawi la mti ili ahamie upande mwingine tena wa mti, lakini mguu wake wa kushoto ukanasa katikati ya maungio ya tawi mbili zilizoacha na kisha ukakwama kwenye majani mengi yaliokuwa yamejisokota pamoja.

Wakati akiwa katika mkwamo huo, tayari mkono wa kushoto wenye simu ulikuwa unakaribia kinywani kwake.

Lakini kuna jambo lingine zaidi lilimtokea akiwa katika harakati hizo za kujiokoa na kutaka kuwaarifu wenzake.
 

Forum statistics

Threads 1,356,607
Members 518,917
Posts 33,134,264
Top