Operesheni KuKu (kufa kupona). riwaya ya kijasusi

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,666
Points
2,000

Kudo

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,666 2,000
Tatizo akiona wafuatiliaji wamekuwa wengi anaanza kuringa, mara ana majukumu, mara anaumwa halafu baadae anasema inauzwa.
Pole Sana kama huwa nakukwaza hadi uone naringa kiasi hicho!!

Pia nisamehe kwa maringo yangu yanayokukwaza!!.

Tazama sehemu ya tatu jana nimejitahidi kuiposti saa saba usiku nadhani utaelewa kwa nini iwe huo muda wewe ukiwa umelala.

Lakini nisamehe pia kwa kuwa huwa naipeleka whatsapp wakati wewe unataka usome bure kabisa bila hata kunitumia vocha ya kukwangua nijiunge ili usome!!

Lakini pia naomba nikuulize upo nchi gani ambayo huwezi kupata mia tano tu (500) ya kununua riwaya mwanzo mwisho?.
Huna whatsapp tumia email, huna email tumia whatsapp..

Nchi yoyote Duniani unaweza kunitumia na nikapata mia tano tu, au elfu moja ikizidi sana huwa elfu mbili.

Na mwisho nikukumbushe kuwa hii ni kazi kama kazi zingine wala si kufurahisha watu bure, ndo mana ili uandike lazima ufanye utafiti kwa kina ikibidi usafiri mkoa au nchi kutafuta ukweli wa kile unachotaka kuandika.

Nadhani umeona kuna mdau huko juu kanitisha kwamba naandika vitu deep sana, unadhani nikiandika kwa kukurupuka bila tafiti nitapata vitisho hivyo ambavyo watu wanakuja hadi pm kuniomba nipunguze ukweli katika riwaya zangu hizi? Unajua garama inayotumika hadi naandika kitu kinachokuvutia bila kukutoa kwenye reli ya usomaji?.

Lakini dada yangu nikwambie kitu, duniani hakuna kitu cha bure na ndo mana hapa Jf unanunua vocha na bado google wanakulipia ili uingie bure kwa kuwa wanamlipa Melo. Kama wasingekuwa wanamlipa basi tungeingia kwa kulipia kama zilivyohuduma zingine duniani za kupata habari!!!

Narudia tena kukuomba radhi kama nimekukwaza ama nimekwaza yeyote kwa utaratibu wangu huu, ila hii ni kazi kama kazi zingine na ndo mana ina hati miliki kila kazi unayoona naweka hapa na huko pia nalipia ili kulinda kazi yangu.

Hivyo nisamehe bure kwa maringo yangu yanayokukwaza lakini jifunze kuheshimu kazi za watu bila kutoa lugha ya kuudhi ama kukera. Wapenzi wa riwaya hawana lawama wanajua ugumu wa kazi na faida wanazopata kwa kusoma kazi za wengine!!.

Afu mi niko poa Sana sema gubu lako tu, mimi wengi nimekuwa nawapa bure kama hawana pesa!! Waniomba kistarabu tu nawaelewa!!
Wapo hapa labda watakupa ushuhuda wa vile nilivyo.

Lakini pia kuna wezi wa kazi za watu, ukiweka hadi tamati anachukua na kuwek kwenye page yake au blog na kuuza! ....

Nimeamua kukujibu kirefu ili unielewe na wengine wenye kuniona nina maringo nao wajue kwa nini ipo hivyo!! Hakuna mwandishi anaetoa bure siku hizi,hii ni kazi kama kazi zingine!!

Nisameheni wote niliowakwaza!!
 
charrote

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Messages
882
Points
1,000

charrote

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2017
882 1,000

Hujanikwaza mkuu ila nimesema nionavyo mimi, sijui nikoje lakini mimi ni mtu ninayeamini katika taarifa kuwa ukianza kupost hadithi sema kabisa utaweka mpaka sehemu fulani halafu utauza

Binafsi ni mwandishi na ninatamani sana siku moja taaluma hii ikue na ithaminiwe kama kazi nyingine za fasihi.

Nimefuatilia riwaya zako nyingi ,ni nzuri lakini kuna hatua inafika unakwaza sisemi uweke bure hapana lakini nakushauri uwe muwazi kuliko kuwa unaanza kutoa sababu ambazo hazipo lakini kumbe lengo lako likiwa kuuza.

Wengi tunapenda kazi yako ,kupitia wasomaji naamini kazi yako inakua zaidi. Ichukulie hii kama kazi na uifanye kwa ueledi ikiwa kuna mabadiliko tujulishe mapema.

Kazi njema.
 
bobefu zoefu

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2018
Messages
357
Points
250

bobefu zoefu

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2018
357 250
Itaisha au itahamia wasap?
Haitoisha ndugu kumchangia mda wake na mb zake,,yatupasa zikibaki sehem tatu au nne tumchangie Sawa mkuu ujue huyu mtunzi tofauti na wengine yeye huwa haizidi buku tatu au mbili na mpaka Mia tano huwa anatuuzia.Ila wengine mpaka elfu tano na kuendelea wanatuuzia vipande
 
bobefu zoefu

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2018
Messages
357
Points
250

bobefu zoefu

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2018
357 250
Pole Sana kama huwa nakukwaza hadi uone naringa kiasi hicho!!

Pia nisamehe kwa maringo yangu yanayokukwaza!!.

Tazama sehemu ya tatu jana nimejitahidi kuiposti saa saba usiku nadhani utaelewa kwa nini iwe huo muda wewe ukiwa umelala.

Lakini nisamehe pia kwa kuwa huwa naipeleka whatsapp wakati wewe unataka usome bure kabisa bila hata kunitumia vocha ya kukwangua nijiunge ili usome!!

Lakini pia naomba nikuulize upo nchi gani ambayo huwezi kupata mia tano tu (500) ya kununua riwaya mwanzo mwisho?.
Huna whatsapp tumia email, huna email tumia whatsapp..

Nchi yoyote Duniani unaweza kunitumia na nikapata mia tano tu, au elfu moja ikizidi sana huwa elfu mbili.

Na mwisho nikukumbushe kuwa hii ni kazi kama kazi zingine wala si kufurahisha watu bure, ndo mana ili uandike lazima ufanye utafiti kwa kina ikibidi usafiri mkoa au nchi kutafuta ukweli wa kile unachotaka kuandika.

Nadhani umeona kuna mdau huko juu kanitisha kwamba naandika vitu deep sana, unadhani nikiandika kwa kukurupuka bila tafiti nitapata vitisho hivyo ambavyo watu wanakuja hadi pm kuniomba nipunguze ukweli katika riwaya zangu hizi? Unajua garama inayotumika hadi naandika kitu kinachokuvutia bila kukutoa kwenye reli ya usomaji?.

Lakini dada yangu nikwambie kitu, duniani hakuna kitu cha bure na ndo mana hapa Jf unanunua vocha na bado google wanakulipia ili uingie bure kwa kuwa wanamlipa Melo. Kama wasingekuwa wanamlipa basi tungeingia kwa kulipia kama zilivyohuduma zingine duniani za kupata habari!!!

Narudia tena kukuomba radhi kama nimekukwaza ama nimekwaza yeyote kwa utaratibu wangu huu, ila hii ni kazi kama kazi zingine na ndo mana ina hati miliki kila kazi unayoona naweka hapa na huko pia nalipia ili kulinda kazi yangu.

Hivyo nisamehe bure kwa maringo yangu yanayokukwaza lakini jifunze kuheshimu kazi za watu bila kutoa lugha ya kuudhi ama kukera. Wapenzi wa riwaya hawana lawama wanajua ugumu wa kazi na faida wanazopata kwa kusoma kazi za wengine!!.

Afu mi niko poa Sana sema gubu lako tu, mimi wengi nimekuwa nawapa bure kama hawana pesa!! Waniomba kistarabu tu nawaelewa!!
Wapo hapa labda watakupa ushuhuda wa vile nilivyo.

Lakini pia kuna wezi wa kazi za watu, ukiweka hadi tamati anachukua na kuwek kwenye page yake au blog na kuuza! ....

Nimeamua kukujibu kirefu ili unielewe na wengine wenye kuniona nina maringo nao wajue kwa nini ipo hivyo!! Hakuna mwandishi anaetoa bure siku hizi,hii ni kazi kama kazi zingine!!

Nisameheni wote niliowakwaza!!
Saluti komledi
 
Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,666
Points
2,000

Kudo

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,666 2,000
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA NNESami na Kakere walitupwa kwenye gari kama vifurushi vya viatu vya bondo alimaarufu saa sita utanikoma.
H
Hawakujua wanapopelekwa na ni nini kitatokea huko.

Ila kuondoshwa kwao katika mapango ya milima Meko ndio kukazua kizaazaa na ikawa ni kufa kupona katikati ya Mji wa Beni.

***

Kabla hawajaondolewa kwenye mapango ya milima Meko; Sami na Kakere walifunikwa nyuso zao na kisha wakabebwa kibabe na kutupwa nyuma ya gari na kisha wakasikia maongezi baina ya waasi wale na kisha walisikia vishindo vya wapiganaji zaidi ya wanne wakipanda kwenye gari walilokuwamo na kisha gari ikaondolewa huku makelele mengi yakisikika kutoka kwa wapigaji kuonesha walifurahia sana hekaheka za aina ile.

Safari ilikuwa ya furaha kwa wapiganaji wale lakini ilikuwa ni karaha kubwa kwa Sami na Kakere ambao walikuwa wamelazwa kwenye gari huku wakiwa wamefungwa mikono na miguu na nyuso zao zikiwa zimefunikwa kwa mifuko mizito kiasi hata kupumua ilikuwa ni shida.

Mbali na yote, ubovu wa barabara waliokuwa wanapitia ilikuwa ni adha nyingine kwao, mana mara kwa mara walijikuta miili yao ikipaa juu na kujibwaga chini kwa sababu ya gari kupita kwenye mashimo mashimo huku ikiwa kwenye kasi kubwa..

Kila mmoja alizidi kusali ili Mungu azidi kumweka hai katika adha ile..

Vumbi la barabara walizokuwa wakipita lilizidi kuwa kero kubwa kwao hasa kwa kuwa sasa vumbi lilipenya na kuingia kwenye mifuko huku wakishindwa kupumua vyema na hata pale Sami alipojaribu kuomba wa wafunguliwe vifuko vile wapate kupumua vyema; hakuna aliemsikia zaidi ni yeye mwenyewe alijisikia akiunguruma peke yake!!Safari ilikuwa ni zaidi ya saa mbili na muda wote huo hakuna aliejali maumivu waliokuwa wakipitia hasa kwa miili yao kurukaruka na kutupwa huku na huko ndani ya gari walilokuwamo.

Magari yalisimama kisha Sami na Kakere wakashushwa mzegamzega hadi chini na kufunuliwa uso wao.

Walipigwa na butwaa kidogo ili macho yao yapate kufanya kazi na kuozea mwanga.

Walizongwazongwa na kusukumwa kuelekea kwenye nyumba moja ya bati iliokuwa miongoni mwa nyumba nyingi za tembe pamoja na mahema.

Macho yao yaliona namna kambi ile ya waasi ilivyokuwa kubwa na kila kona ya kambi ile kulikuwa kuna kidungu na kila kidungu kilikuwa kina wapiganaji zaidi ya mmoja na kila mmoja mpigaaji alikuwa ameshikilia silaha ya kivita yenye uwezo mkubwa na ya kisasa sana na nyingi zilikuwa ni modified colt Canada rifle..

Sami alijiuliza swali moja
“Hizi silaha huwa zinatumiwa na mataifa makubwa barani ulaya na ni aghalabu sana kukuta silaha zile zipo kwenye majeshi ya aafrika; Ni nani anawapa silaha hizi?” Likabaki swali bila majibu.

Waliingizwa hadi ndani ya nyumba ile na kama kawaida waliona na kukutana na ulinzi mkali kuanzia kwenye lango la kuingilia hadi ndani ya nyumba ile ambayo ilikuwa ni ya kisasa sana ndani kuliko nje ilivyokuwa inaonekana.
Wakaingizwa kwenye chumba kimoja kilichokuwa na viti vitatu na meza moja huku viti vile vikiwa vimeiweka kati meza ile.

Wakakalizwa upande ambao kulikuwa na viti viwili kisha bila kuambiwa lolote wakafunguliwa kamba zililizokuwa zimesalia mikononi mwao.

Ukimya ulitanda mule ndani huku walinzi waliokuwa mule wakiwa bize na kazi yao kama vile walikuwa peke yao.

Kakere alikiri kwamba kundi lile la uasi ni moja ya kundi lenye nidhamu sana na ndivyo ililivyokuwa; kundi lile lilikuwa ni kundi lenye nidhamu sana kwa viongozi wao ila ni kundi la kihuni sana kama usipoenda vile watakavyo.

Zilipita zaidi ya dakika kumi ndipo tena harakati zikasikika na kisha ukafuata msafara wa walinzi kadhaa wakifuatiwa na Chepe ambae alikuwa amevaa kanzu safi tofauti na wakati ule aliokuwa amevaa mavazi ya kijeshi na na safari hii alikuwa amebadili hadi kiziba jicho (eye patch) badala ya nyeusi akawa amevaa nyeupe na pia hakuwa ameongozana na mwanamke.

Chepe alikaa kwenye kiti kile kimoja huku akiwatizama mateka wake kwa zamu.

“Tumekutana tena ndugu zangu ila wakati huu inaweza kuwa ni kwa hatua nyingine ikiwa mtazidi kukomalia msimamo wenu!” Chepe aliwambia huku akipokea Siga kutoka kwa mlinzi wake aliekuwa na mkebe wake.

“Naomba mnambie nyie ni kina nani na mpo hapa kwa ajili ya nini!!” Chepe aliwahoji huku akiwasha siga yake.

“Sisi ni waandishi wa habari na ndio kazi iliotuleta hapa mjini Beni hakuna zaidi ya hilo Mr. Chepe!” Kakere alizungumza.

Chepe akatabasamu kidogo

“Kwa hiyo hata yale majina niliowatajia si ya kwenu, inamaana wewe huitwi Mina na huyu mwamba haitwi Zedi Wimba?” Chepe alihoji huku safari hii jicho lake moja likiwa lipo makini bila kupepesa sehemu yoyote ile.

“Upande wangu mimi sina jina lingine zaidi ya hili la Kakere Masuti na sijui hilo jina la Mina kiukweli!!” Kakere alizidi kujitetea mbele ya Chepe na walinzi wake.

“Unajua huwa sipendi masihara kabisa na kitu kimoja yawezekana hamnijui vizuri nyinyi!” Chepe alisema huku akizima siga yake kwa kuisigina juu ya meza kwa mkono wa kushoto.

“Sikilizeni nyie mapimbi; kuna aina zaidi ya tano za mashushu ambazo ni
Local spies; Moles/inward spies; double agent/covert spies; doomed spies na surviving spies.” Chepe aliwatizama tena waandishi wale huku akihamisha jicho lake kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine kisha akaendelea…
“Na bahati mbaya kwenu ni kwamba mimi nimepitia levo zote hizo nikiwa chini ya MI(military Intelligence) na nimefanya kwa mafanikio makubwa hadi wakati ambao nilipoteza jicho langu na badala ya kupandishwa cheo nikaambiwa mi mlemavu na kuletwa Congo kulinda amani huku utu wangu wa kupigania nchi yangu ukionekana ni kazi bure kabisa!” Chepe akawatazama na kuendelea tena kuzungumza

“Msidhani sijui mbinu za kukomaa ili usitoe taarifa kwa mwingine, hivyo nyinyi hata nikiwalamba miguu itakuwa kazi bure, hamtaniambia ninachotaka, lakini tambueni hakuna jasusi aliepona kwenye modified torture!” Chepe aliwachimba mkwara waandishi wale..

Wakati kila mmoja akiwaza lake mara akaingia Sajini Lolo akiwa ameshika kipakatarishi na kwenda pale alipokuwa Chepe na kumnong’oneza kitu kisha akaweka kipakatarishi kile mezani.

Pakatarishi ile ilikuwa ni ya Mina p.a.k Kakere Masuti.

Kakere alianza kuingiwa na hofu baada ya kuona mikono ya Chepe ikichezea kiparaza.

Chepe aligusa hapa na pale kwenye parakatarishi ile kisha akawatazama mateka wake!.

“Ni nani mmliki wa kompyuta hii?” Chepe aliuliza

Kakere akaitika kuwa ni ya kwake.

“Ok naomba nywila yake tafadhali!!” Chepe alimwambia Kakere.

Kakere akafikiria kidogo kisha akamtazama Sami.

Sami alimeza mate na kutanua shingo kwenda juu ili Kakere aone mate yanavyoteleza kooni.

Ilikuwa ni ishara iliotembea kwa ufupi wa sekunde mbili tu Chepe au walinzi wake kujua kilichoendelea.

Kwa nini hawakujua!

Kwa sababu wakati Kakere anamgeukia Sami; Sami yeye hakuhangaika kumtazama japo alijua Kakere alihitaji nini kwake hivyo akafanya kile ambacho si rahisi mtu yoyote kugundua isipokuwa wao tu.

Na kama Sami nae angegeuza uso kutazamana na Kakere basi ilikuwa rahisi wao kugundulika.

Kakere akafikiria maamuzi ambayo ameelekezwa na Sami kuyachukua kama yalikuwa na tija wakati mgumu kama ule zaidi alihofia kuwa maamuzi yale yalikuwa ni sahihi kwa wakati sahihi hasa alipoifikiria Eagle wing house na umuhimu wa kile alichopaswa kufanya.

Heri wao waumie ila makao makuu wapate kile walichostahili kukipata kupitia parakatashi.

“00000” Kakere alitaja nywila za kufungulia mafaili ya pakatarishi yake.

Chepe akapinda mgongo na kuingiza maneno yale.

Ikafunguka na taratibu akaanza kupekua hili na lile.

Hazikupita dakika tatu ikazima, harakaharaka Sajini Lolo akachomeka waya wa kuingiza moto ili kuiwasha tena na zoezi halikufanikiwa na iligoma kuwaka tena.

Waliihangaikia kwa zaidi ya dakika kumi lakini haikuwaka tena.

Wakiwa katika harakati za kuhakikisha inawaka, mara akaingia jamaa mmoja ambae alikuwa ameshika kifaa kidogo mithili ya simu za upepo na kwenda kumuonesha Chepe.

Chepe akatupa chini pakatarishi iliokuwa mkononi huku tusi kubwa kwa lugha ya kifaransa likimtoka na kwa wepesi wa hali ya juu akamnasa kofi zito Kakere ambae alienda kutua chini kama mzigo wa makohozi.

Sami akasimama kwa pupa nae akajikuta akienda chini kwa pigo safi kutoka kwa Chepe lililotua sawia kifuani kwake.

Wakati wanataka kujiinua kutoka walipokuwa wameangukia wakajikuta wakirudishwa tena kwa mateke mawili ya mzunguko kutoka kwa Chepe huku Chepe akiunguruma kama gari bovu kilimani.

Walinzi wake wakaingilia na kumpokea kisha wakaanza kushusha kipigo kizito kwa Sami na Kakere ambao kwa dakika moja tu hakuna aliemtambua mwenzie kwa jinsi nyuso zao zilivyokuwa zimeumuka kama maandazi ya Azam.

“Idiots they set us on poison trap!!” Chepe alisema huku akichukua kile kifaa kidogo na kukizima.

“Zimeni mitambo yote na hawa ngedere wapelekeni shimoni!” Chepe alisema huku akianza kupiga hatua kutoka ndani ya chumba kile na Kakere na Sami waliburutwa chini kuelekezwa shimoni ambapo hakuna aliejua kuna nini huko shimoni.

Waliburuzwa chini kwa zaidi ya dakika kumi kisha wakaingizwa kwenye chumba kilichokuwa na giza ila kile chumba kina mashimo mawili.

Wakafungwa minyororo kisha wakaanza kushushwa kila mtu kwenye shimo lake.

Kadri walivyokuwa wanashuka ndivyo joto lilizidi kutesa majeraha yao na jasho lilianza kuwatoka kila mmoja kivyake kwa kuwa kulikuwa kuna joto kali na uvundo wa harufu kali sana.

Sami alikadiria urefu ule ni zaidi ya futi kumi kwenda chini huku akishindwa kuelewa joto lile kubwa lilisababishwa na nini mana ilikuwa ni kama wamewekwa kwenye pipa ambalo lilikuwa linaanza kuchochewa moto.

Kwa joto ile, jasho lilianza kushuka mwilini kama maji huku ikeleta adha kwenye majeraha mabichi ya kipigo walichopewa.

Hatimae waligota chini huku mikono ikibaki ikining’inia juu kwa kuwa ilikuwa imefungwa na minyoyoro iliokuwa juu.

Kakere nae aligota chini na kubaki mikono juu, lakini alihisi hali ya tofauti mbali na uvundo uliokuwamo mle lakini pia kulikuwa kuna sauti ya vitu viwili tofauti.

Kulikuwa na sauti kali ya mbu wengi huku wakitoa sauti za mlio mkali kama vilio msibani. Lakini pia kulikuwa kuna sauti nyingine ilianzia chini,kisha akaanza kuhisi miguu yake ikitambaliwa na vitu.

Walikuwa ni mende wa kufugwa na mbu nao wakaanza kumshambulia huku mende nao wakionja ladha ya jasho la mtu.

Adha kwake ilikuwa ni hawezi kujipangusa kwa kuwa mikono ilifungwa.

Lakini ilikuwa ni mara mia zaidi usumbufu wa mende na mbu kuliko alichokutana nacho Sami.

Sami alikutana na kundi kubwa la nge na walianza kushambulia miguu yake huku wengine wakipanda kuwahi nafasi kwenye kwapa na sehemu zingine za mwili.

Sami alipiga kelele za maumivu huku kelele zile tena zikigeuka kuwa kero kwake mwenyewe kwa kuwa hazikwenda mbali kwa ufinyu wa shimo alilokuwamo.

Angefanya nini wakati mikono imefungwa!!!

***
 
Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,666
Points
2,000

Kudo

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,666 2,000
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA TANO

Adha kwake ilikuwa ni hawezi kujipangusa kwa kuwa mikono ilifungwa.

Lakini ilikuwa ni mara mia zaidi usumbufu wa mende na mbu kuliko alichokutana nacho Sami.

Sami alikutana na kundi kubwa la nge na walianza kushambulia miguu yake huku wengine wakipanda kuwahi nafasi kwenye kwapa na sehemu zingine za mwili.

Sami alipiga kelele za maumivu huku kelele zile tena zikigeuka kuwa kero kwake mwenyewe kwa kuwa hazikwenda mbali kwa ufinyu wa shimo alilokuwamo.

Angefanya nini wakati mikono imefungwa!!!

***
Kila mmoja alipiga kelele kwa uweza wake huku kila mmoja akijitahidi kujizuia kwa kujitikisa tikisa ili lau aweze kuondoa wadudu wale waliokuwa wametumwa kufanya yale waliokuwa wanayafanya.

Bado ilikuwa heri kwa Kakere kuliko kwa Sami ambae sumu ya nge na maumivu yake vilizidi uwezo wa ubongo na kujikuta akianza taratibu kupoteza fahamu bila kupenda huku maumivu yakiwa kedekede mwilini mwake.

Kakere yeye alizidi kupata adha ya kuliwa na mbu huku mende wakijaribu kunyonya ngozi iliokuwa imegandiwa na jasho lenye chumvi chumvi na kumwachia maumivu yasiosemekana.

Ilikuwa ni kulia hawezi Kia sababu sauti yake ilirudi kuwa kero masikioni mwake bila kupenda!

Ilikuwa ni lazima aishie kukugumia tu kama fisi anaefika mshindo.

Kitu kimoja pia alifikiria namna ambavyo mbu walikuwa wanamshambulia kwa kupokezana na ni kama vile walikuwa wanafundishwa kazi ile ya kumla mtu ngozi yake.

Mende na mbu walianza kummaliza nguvu za mwili kwa kazi waliomfanyia lakini pia kutokwa na jasho jingi kulimpunguzia ufanisi wa mwili kufanya kazi na akabaki kama mlevi aliepigwa denda na mtoto mchanga.

Hakujua itachukua muda gani kuondolewa kwenye shimo lile na hakuwa na hakika kama Sami nae alikuwa anapitia adha kama ya kwake kwa kuwa alijua kabisa Sami ni lazima atapewa mateso zaidi yake kwa kuwa yeye ni mwanaume na mbali ya hivyo pia alikuwa ni mwenye jina kubwa katika medani za ushushu hivyo jicho kubwa litakuwa kwake kuliko yeye.

-------
Chepe alikuwa anakuna kidevu chake kwa ncha ya kidole cha shahada huku macho yake yakiwa makini kutazama vijana watatu waliokuwa wapo makini kufanya jambo fulani kwenye mitambo ya mawimbi ya umeme yaliokuwa yanawasaidia kupiga simu za satellite na pia kujua mienendo ya mawimbi ya umeme yaliokuwa yanasogelea kwenye maeneo yao.

Mitambo hii ndio ilifanikiwa kujua kuna mawimbi ya ajabu yanatoka kwenye pakatarishi iliokuwa inawahangaisha Chepe na Sajini Lolo baada ya kupewa nywila zake na Kakere.

“Poison trap!! Hawa wajinga sana!” Chepe alijisemea huku akiendelea kufuatilia kwa makini kile kilichokuwa kinafanywa pale.

Kijana mmoja akamgeukia Chepe baada ya kompyuta yake kutoa mlio wa bip mara tatu huku alama nyekundu ikisoma kwenye ramani kuonesha pahali fulani ndani ya Afrika mashariki.

“Kamanda mawimbi yamesafiri hadi Dar es Laam Tanzania!” Alimwambia huku akigeuka tena na kuendelea kucheza na kicharazio cha kompyuta yake.

Chepe alipiga ngumi ukutani huku akitoa tusi zito la nguoni na kutupa baragashia yake ya thamani.

“Aisee sasa hii ni vita mpya inaanza na Tanzania haijawahi kufeli ila hii nitawafelisha nawajua nje ndani hawatanisumbua tena naanza na hawa vikaragosi wao waliowatuma” Alijiwazia peke yake huku macho yake yakiwa bado kwenye vioo vya kompyuta.

Mara akaingia Luteni daraja la kwanza bwana Amolo akiwa ameshika simu.

“Kamandi ya sita kule Beni juu wanataka kuzungumza na wewe!!” Amolo alimwambia Chepe .

“Unadhani wanataka kusema nini labda labda!” Chepe badala ya kupokea alimuuliza Amolo.

“Ni kuhusu wandishi wa habari tuliowazuia hapa!!” Amolo alijibu.

Chepe alitabasamu kisha akamwambia Amolo.

“Wambie sihitaji kwa sasa nitawatafuta mwenyewe!” Chepe akamwambia Amolo na Amolo nae haraka akaondoka mle ndani.

“Tanzania…… Tanzania mh!!” Chepe alijiwazia huku akitoa simu yake mfukoni iliokuwa na mkonga na nyuma ikiwa imetuna kama mgongjwa wa fufu.

Ilikuwa ni simu ya satellite.

Akachangua namba kadhaa kisha akaipata alioihitaji akapiga.

“Tap on the top, tunahitaji kuweka ukuta kila sehemu miguu ya mamba imeonekana huku na harufu imefika kiotani!!” Chepe alizumgumza na mtu aliepokea simu upande wa pili.
Na alitumia lugha ya kijasusi, lugha ya mafumbo akiwa na maana kumekuwa na vihatarishi kwenye maeneo yao na bado tarifa za vihatarishi imefika mbali na itakuwa shida kwao.

Mtu wa upande wa pili alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema

“Ina maana umewadaka nzi wao!?” Alihoji yule jamaa kwa kiswahili safi kabisa.

Akimaanisha nzi ni mashushu au majasusi wa kitanzania.

“Yes!! Wapo shimoni hadi sasa!!”Chepe alijibu.

“Umekosea sana!! Na umetangaza vita mbaya sana na hao jamaa, lakini kama ulijua wapo ulishindwa kuwapangusa bila kuwanasa?” Alihoji jamaa huku akionekana dhahiri kuogopa kitu kilichofanywa na Chepe.

“Usiogope najua cha kufanya!” Chepe alijibu.

“Kama kipi?” Jamaa alihoji.

“Naomba unitumie picha za watu wote wanaofanya kazi kwenye kitengo cha special operation chini ya Kamishina Zenge wa Zenge na Hawa Maiga kisha anza kutega huko na wakifanikiwa huku basi sisi tunamaliza!” Chepe alimwambia jamaa.

“Watanzania wajanja aisee wanaweza kukuleta operative ama considered spy ohoo!!” Jamaa alimtahadharisha Chepe.

“Huku watakuja madeep spy tu trust me!!” Chepe nae aliendelea kutetea hoja yake.

“Sawa ngoja nitege mingo na picha utapata hivi punde!” Jamaa alisema na kukata simu.

Chepe alitabasamu.

“Wajinga wametaka mchezo sasa mimi nawafungia kibwebwe tuserebuke wote na ndo watajua pombe ya ngoma haikeshi mana watainywa hadi vilembwe!” Chepe alijisemea huku akiandika ujumbe wa kikao cha dharura kwa watu fulani na kuutuma kwa wakati mmoja kisha akatoka kwenye kile chumba na kuelekea kule kwenye chumba cha shimo na kuamuru Kakere na Sami watolewe shimoni.

Agizo lilitekelezwa mara moja na waadishi wale wakaibuliwa na Kakere alikuwa hoi taabani lakini Sami yeye hakuwa na fahamu kabisa huku mwili wake ukiwa umekuwa mweusi kwa sababu ya sumu ya nge waliomshambulia mwili mzima.

“Wapelekeni rest in peace wapeni huduma wazinduke nitakuja badae!” Chepe alitoa maagizo na kisha akatoka na hakuna aliejua safari yake ilikuwa ni wapi.

--EAGLE WING HOUSE-DAR—

Mwanamke aliependeza kwenye sare zake za jeshi alishusha mkonga wa simu ya mezani huku uso wake ukiwa umejikunja na mdomo wake akiwa ameupeleka mbele kama kalambishwa konyagi.

Akakalia kiti chake cha kuzunguka na kuweka miguu juu ya meza iliokuwa mbele yake huku mikono yake akiufumbata pamoja na kuilaza juu kidogo ya kinena kisha macho yake yakatua juu ya ukuta na kukutana na picha ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mwanamama yule mabegani mwake alikuw na kola yenye ngao (bibi na bwana) kisha nyota tatu kumaanisha cheo chake kilikuwa Brigedia Jeneral na juu kidogo ya mfuko wa vazi lake la juu kulikuwa kuna jina lake.

Alikuwa ni Brigedia Jeneral Hawa Maiga.

Muda huo alikuwa ametoka kuwasiliana na simu mbili huku simu ya kwanza ikiwa ni kutoka nchini Congo kwenye vikosi vya umoja wa mataifa na kuarifiwa kuwa mkubwa wa waasi Chepe alikuwa amegoma kuzungumza nao hivyo walikuwa hawajui ni nini shida yake kwa waandishi wale.

Bi Hawa Maiga alishindwa kuelewa kama Chepe alishindwa kuzungumza ni kwa kuwa amejua aina ya watu aliowateka ama anahisi tu.

Bi. Hawa Maiga alimtambua vyema Chepe kuliko mtu yeyote na alijua ni lazima Chepe atakuwa amejua wale ni Zedi na Mina kutoka kwenye kitengo chake cha MI chini ya mwamvuli wa special operations..

“Lakini nimekutengeneza mimi Chepe na huwezi kushindana na mimi hata kidogo, uliowaua wanatosha, familia zao zimelia vya kutosha nisingependa tena damu imwagike ni lazima nikutie mikononi hata kwa kuingia mi mwenyewe” Brigedia Jeneral Hawa Maiga alijisemea huku akitikisa mguu wake wa kulia na kwa waliomfahamu hapo walijua yupo kwenye kiwango cha mwisho cha hasira na hata ukimzingua unaweza kuchezea risasi ama mbata za kutosha.

Bi Hawa pia alikuwa amepiga Simu kwa Kamishina Zenge wa Zenge ambae nae alikuwa ni msimamizi wa operesheni maalumu upande wa jeshi la polisi huku yeye akiwa ni msimamizi wa operesheni maalumu upande wa jeshi yani Military intelligence (MI).

Kwa nini walishirikiana?

Kwa sababu vijana wa special operations walikuwa ni wale wale huku wakijigawa kimajukumu kulingana na uzito wa kazi kila pande hivyo wakiwa chini ya Zenge wa Zenge walipaswa kufanya kazi za kipolisi na wakiwa chini ya Hawa Maiga wanafanya kazi za jeshi kikamilifu kwa kuwa wote walikuwa ni makomando waliofuzu kila idara na pia walikuwa wameiva kwenye mafunzo ya ujasusi na upelelezi.

Simu aliopiga ilimhitaji Kamishina afike makao makuu yao wote kwa kikao chao cha dharura kuhusu jambo lile.

Na kikao kile ndicho kilizaaa balaa na kizaaa zaa kikubwa ndani ya Dar na nchini Congo na ikawa ni operesheni kufa kupona iwe jua iwe mvua.
 
dvj nasmiletz

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Messages
431
Points
500

dvj nasmiletz

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2018
431 500

Saafi...endelea mkuu
 
Forum statistics

Threads 1,345,287
Members 516,220
Posts 32,852,294
Top