Operesheni KuKu (kufa kupona). riwaya ya kijasusi

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,809
6,081
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660


VITABU VILIVYOTANGULIA
• KIKOSI CHA PILI
• MPANGO WA CONGO
• URITHI WA GAIDI
• SAUTI YA MTUTU
• DAKIKA ZA MWISHO
• OPERESHENI JICHO LA PAKA
• BAHARIA
• CHUMBA CHA SABA.


Soma

----Beni; Kivu kaskazini Congo.-


Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa (UN) vilikuwa vinatoka kijiji cha Kubuhe na kuelekea mjini Beni ikiwa ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia wa maeneo hayo. Vikosi hivi vilikuwa kwenye mizunguko yake ya kawaida na kila siku.
Vikosi hivi vilikuwa na wanajeshi zaidi ya kumi na mbili huku magari ya kijeshi yenye nembo za UN yakiwa mawili na gari moja la kawaida ila nalo likiwa na chapa ya UN lakini pia kulikuwa kuna gari moja la msalaba mwekundu na magari haya yalikuwa yametanguliwa na vifaru viwili huku kimoja kikiwa nyuma na kingine mbele kuhakikisha usalama wa msafara ule.

Katika gari lile la kawaida aina ya Ford; kulikuwa kuna mwanajeshi mmoja na watu wengine wawili ambao walikuwa ni mwanamke na mwanaume huku vifuani mwao kukining’inia vitambulisho vyao ambavyo viliwatambulisha wao ni waandishi wa habari kutoka shirika la habari la umoja wa mataifa ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kuhabarisha ulimwengu yale yaliokuwa yakiendelea katika uwanja wa kulinda amani katika jimbo la Beni ndani ya Kivu ya kaskazini.

Na katika yale magari mawili ya kijeshi pia kulikuwa kuna wanajeshi ambao walikuwa wamebeba silaha zao vyema kabisa huku macho yao yakiwa makini kuhakikisha wanavuka salama katika msitu ule uliokuwa unatenganisha kijiji cha Butuhe na Kabasha kilomita kumi kutoka mjini Beni Kivu ya kaskazini.

Mara nyingi katika misafara hii ya patrol mawasiliano makubwa huwa yanatokana na simu za upepo baina ya msafara na wakuu wa kamandi ya ulinzi na usalama.
Na ndivyo ilivyokuwa hata wakati msafara huu ulipokuwa njiani mawasiliano yalikuwa yanafanyika ili kuhakikisha usalama unazingatiwa kwa wanajeshi wote na matabibu waliokuwa katika msafara ule.

Kwenye gari lile la ford wale waandishi wa habari walikuwa kimya kwa muda mrefu huku kila mmoja akitafakari lake.
Mara mwanaume akawa kama kazinduka kutoka usingizini na akamtazama mwenzake wa kike ambae alikuwa amegemea kiti na dhahiri akiwa mbali kifikira.

Mwandishi wa kiume akajipapasa hapa na pale, kisha akachukua mkoba wake uliokuwa na kamera na kompyuta mpakato.
Alitoa kamera yake na kuitazama kisha akatoa betri zake na kwenye kiunga betri alinyofoa kadi ndogo ya kuhifadhi kumbukumbu.
Kadi ile akaipachika kwenye diski mweko kisha akapichika kwenye kipakatarishi (kompyuta mpakato) na akaaza kuhamisha mafaili kadhaa ambayo ni yeye tu aliejua yana umuhimu gani kwake kisha alipomaliza akatoa na diski mweko na kutoa ile kadi na akarejea tena kwenye kipakatarishi na kufuta yale alioona yanafaa kufutwa.

Wakati akifanya hayo yote kwa kasi ya ajabu; muda wote mwandishi wa kike alikuwa akimtizama tu bila kusema neno.

Bwana yule hakujali macho ya mwenzake bali akajishika kwenye mkanda wake wa suruali na kutoka na kiwembe kikali ambacho mara nyingi hutumika kutahiri watoto.
Akavua shati lake.

“Unataka kufanya nini wewe!!” mwanamke alihoji huku akiwa ametumbua macho kama malaya alieona pochi ya mzungu.

“Tulia kidogo mama” mwanaume alijibu.

Bwana yule akajishika Kifua chake kilichonona minofu imara kwa mazoezi.

Akashika ziwa lake la upande wa kushoto, akagusagusa kidogo kisha akahamia upande kulia akagusa gusa kidogo na aliporidhika akashika kiwembe kwa mkono wa kushoto na kwa utaratibu sana akachana chini kidogo ya mtuno wa ziwa lake la kushoto na akarudia tena kwa kudidimiza zaidi kiwembe na aliporidhika akachukua ile kadi ndogo aliotoa kwenye diski mweko na kuididimiza pale kwenye lile jeraha alilochana.
Aliporidhika akachukua kitambaa laini na kukimwagia unga mweupe na kupaka jeraha lile ambalo lilikuwa linatoa damu na punde damu ikakatika; akachukua tena unga mwingine na kupaka kwenye hilo jeraha lake na kukakauka kabisa kama vile lilikuwa ni jeraha la siku nyingi.

Muda wote mwanamke alikuwa akimtizama bila kutia neno.

Mwanamke akapumua kwa nguvu baada ya jamaa kuvaa shati lake na kupachika kitambulisho chake kifuani.

“Sikwelewi kabisa ujue!!” mwanamke alisema.

“Hisia zangu zimeenda mbali sana kwenye msafara huu hivyo hii ni tahadhari tu” Jamaa alijibu.

“Zedi una….” Akataka kuropoka kitu yule mwanamke na jamaa akawahi kumzuia huku akimkata jicho kali sana.

“Sikia inabidi uzoee kabisa kutokuniita Zedi Wimba na badala yake uendelee kuniita jina hili la Sami Kinyozi na wewe sio Mina ni Kakere Masuti. Sawa bi Kakere?” Zedi akamwonya Mina na kisha hakutaka maelezo zaidi akajilaza kwenye kiti kama vile hakuwa ana maongezi na yule binti.

Msafara uliendelea kwa utulivu wa hali ya juu huku bado wakiwa wanacheza katikati ya msitu mnene wa Bwanga na kwa ubovu wa barabara basi iliwawia ugumu kuwa na kasi zaidi ya mwendo wa aste aste tu.

Zilikuwa zimebaki kilomita mbili kufika mji wa Kabasha ambao upo kilomita saba kutoka mjini Beni Kivu ya Kaskazini.

Kifaru kilichokuwa mbele kikasimama gafla na kufanya magari mengine nayo yasimame gafla huku vumbi likitimka kwa breki kali za gari zile.

Haraka haraka wanajeshi wakashuka na kujipanga kimakabiliano huku mtu wa mwisho kushuka akiwa ni patrol commander.
Wanajeshi wote walikuwa tayari kwa lolote hasa baada ya kuona mazingira yakiwa hayaeleweki na kilichosababisha msafara kusimama hakikuonekana kwa wakati huo.

Patrol commander akapiga hatua kusonga mbele kulikokuwa na kifaru na nyuma yake walifuata wanajeshi wengine wawili ili kumlinda na shambulizi lolote.

Hatimae kilichosimamisha msafara kikaonekaa.

Mbele hatua kama ishirini hivi kutoka kilipokuwa kifaru; kulikuwa kuna gari moja aina ya Land Rover ya wazi bila mambomba ikiwa imesimama huku bunduki kubwa ya msaada (Light machine gun) ikiwa imechungulia kwa mbele na nyuma yake kukiwa kuna mtu alievaa mavazi ambayo yalifanania na ya kijeshi huku suruali yake ikiwa ni ya kawaida tofauti na shati na kichwani alikuwa amefunga kitambaa na mikono yake ikiwa kwenye bunduki ile kubwa iliobeba mkanda wa risasi.
Mbali na mtu yule pia kulikuwa kuna dereva wa land Rover ile.

Patrol commander alinyoosha mkono wake wa kushoto na kuwapa ishara wanajeshi waliokuwa nyuma yake na ishara ile waliitambua mara moja ya kuwa mbele kulikuwa kuna kundi la waasi, hivyo kila mmoja alitakiwa kukaa sawia huku amri ya kushambulia ikiwa ni chaguo la mwisho endapo kutakuwa hakuna maelewano baina ya watu wale na wao.

Kwa kawaida vikosi vya kulinda amani huwa wanashauriwa kutokushambulia kiholela endapo kundi la waasi litakuwa limehitaji mazungumzo mana mazungumzo yanaeza kuwa na tija kwao.

Wakiwa bado wanatazama gari lile, mara watu wengine wenye silaha walijitokeza katikati ya nyasi ndefu huku wakiwa wanabunduki za kivita na vichwani mwao wakiwa wamevaa majani ili waweze kufanana na nyasi, hii ilikuwa ni mbinu moja wapo ya kujificha katika medani ya kivita (camouflage).

Walinda amani wakajikuta wakiwa wamezungukwa na kundi kubwa la waasi wa msituni huku hakuna ambae alikuwa anajua dhumuni la kuzungukwa kule.

Kiongozi wa doria ambae alikuwa ni raia wa Kenya hakuwa na namna zaidi ya kuwataka wanajeshi wake wawe makini kwa lolote.

Hakuna aliemsemesha mwenzake si walinda amani wala waasi na hakuna aliepiga hatua kumfuata mwenzie.

Ukimya ule ulidumu kwa dakika kama tano hivi huku kila jicho likiwa makini na jicho la mwenzake ili kuwahiana kwa hila yoyote ile.

Wakiwa wamedumu kwenye ukimya ule mara kuna gari jingine lililokuwa wazi likatokea porini huku likiwa na wapiganaji wanne wenye silaha na kila waliokuwa wamesimama nyuma ya gari ile na mtu mmoja akiwa amekaa mbele huku nae akiwa amepakata silaha yake.

Gari lile likanyoosha moja kwa moja hadi alipokuwa kiongozi wa msafara wa walinda amani.

Gari ilisimama kisha akashuka yule jamaa ambae alikuwa amekaa mbele, akamsogelea patrol Commander na kumpa mkono kuashiria wapo pale kwa heri na si shari.

“Sisi bwana tumetumwa tuwapelekeni kambini kwetu kistarabu tu” Jamaa alieshuka kwenye gari alisema huku akijitambulisha jina lake kuwa yeye anaitwa Sajini Lolo. Cheo alipokipata hakuna aliejua labda ni huko kambini kwao.

“Huko kwenu tukafuate nini wakati leo hatukuwa na ratiba ya kudoria hadi huko ?” Patrol Commander ambae kicheo alikuwa ni Luteni na jina aliitwa Njeremi; alimwambia Sajini Lolo.

“Ni mazungumzo ya amani tu wala si kwa ubaya ila ni endapo mkitii amri bila shuruti” Sajini Lolo alimwambia Luteni Njeremi.


“Ni itakuwaje tusipoandamana nanyi Sajini!” Luteni Njeremi alimwambia Sajini Lolo.

Sajini Lolo akacheka kwa sauti kisha akachukua sigara yake na kuwasha akapiga fumba kadhaa na kutoa moshi mwingi juu na kusema

“Hivi wewe ni Luteni gani ambae hujui kuwa hadi sasa umetekwa na kikosi chako? Au huoni umezingirwa?”

Luteni akageuza macho pande zote na kuona waasi wengi wakiwa wamewazunguka kila pande.

“Na kisheria mateka ndie anaefuata mashariti ya mtekaji Luteni au nalo hujui?” Sajini aliuliza kimzaha.

“anyway usiogope hakuna baya ni mazungumzo tu ya kawaida komredi” Sajini Lolo alizidi kusema.

Luteni akachumua simu yake ya upepo na kuwasiliana makao makuu na kuwapa taarifa jinsi ilivyo hali yao huko njiani na makao makuu wakamuomba ashushe silaha na awafuate waasi hao huku wao wakiwa njiani kuelekea huko kutoa msaada kama utahitajika.

Ilikuwa ni kitendo ambacho hakuna aliekitegemea hasa kutoka kwenye kundi la walinda amani, pale ambapo kiongozi wao aliwataka wawafuate waasi wale.

Kutoka kwenye gari la wale waadishi; Zedi p.a.k Sami kinyozi alimgusa begani mwandishi Mina p.a.k Kakere Masuti.

“Usihofu ni moja ya kazi iliotuleta huku” Sami alimwambia Kakere.

Lakini kamwe hawakujua usiku mnene aujua ni mlevi Komba. Wao hawakujua kabisa kitatokea nini huko na kama walihisi ni amani basi walikosea sana lakini hayo ni maisha ya mwanajeshi siku zote kifo ni ushujaa kwake.
Na hii ilikuwa ni mwanzo wa operesheni kufa kupona; operesheni KuKu.
 
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660


SEHEMU YA PILI




Luteni akachumua simu yake ya upepo na kuwasiliana makao makuu na kuwapa taarifa jinsi ilivyo hali yao huko njiani na makao makuu wakamuomba ashushe silaha na awafuate waasi hao huku wao wakiwa njiani kuelekea huko kutoa msaada kama utahitajika.

Ilikuwa ni kitendo ambacho hakuna aliekitegemea hasa kutoka kwenye kundi la walinda amani, pale ambapo kiongozi wao aliwataka wawafuate waasi wale.

Kutoka kwenye gari la wale waadishi; Zedi p.a.k Sami kinyozi alimgusa begani mwandishi Mina p.a.k Kakere Masuti.

“Usihofu ni moja ya kazi iliotuleta huku” Sami alimwambia Kakere.

Lakini kamwe hawakujua usiku mnene aujuae ni mlevi Komba. Wao hawakujua kabisa kitatokea nini huko na kama walihisi ni amani basi walikosea sana lakini hayo ni maisha ya mwanajeshi siku zote kifo ni ushujaa kwake.
Na hii ilikuwa ni mwanzo wa operesheni kufa kupona; operesheni KuKu.


Msafara wa magari ya walinda amani kaskazini mwa nchi ya Congo ulikuwa umeacha njia yake ya kila siku na kuelekea msituni mbali zaidi na vijiji vya Kabasha na Buheta.

Bado hakuna aliejua dhumuni la waasi wale kuwateka walinda amani wale.

Safari ilikuwa ya kimya kimya huku kila mwanajeshi akiwaza jambo lake huku wengine wakisali sala zao kusitokee machafuko yoyote huko waendako na wengine tayari walianza kulia kimyakimya huku wakiomba walau wakutanishwe na familia zao kwa mara ya mwisho.

Lakini yote hayo ilikuwa ni kama dua la kuku tu na hakuna ambae angejua lifuatalo na hata kama lingetokea lile wanalowaza basi familia zao ingekuwa ni ndoto kuziona na badala yake wangerejeshwa majumbani mwao wakiwa ni maiti kabisa na hawasemi wala hawasikii.

Hakika nafsi zao zilijawa na fadhaa sana hasa wakiona idadi yao ni wachache sana kuliko idadi ya waasi wale.

Kwenye gari ya Ford walimokuwamo waandishi wa habari bwana Sami Kinyozi na bibi Kakere Masuti; na wao walikuwa na kazi nyingine tofauti wala hawakujishugulisha na kuwaza kiyama chao bali walikuwa wapo bize kuhakikisha wanapata picha nzuri za kila eneo walilokuwa wanapita na lengo lao lilikuwa ni kupata picha kamili ya kuweza kuwafikisha kwenye kambi ya waasi ambao hadi wakati huo hakuna aliekuwa na uhakika hasa ni waasi wapi;ni boko haramu ambao walikuwa wanazidi kuingia nchini Congo wakitokea Nigeria na Cameroon ama walikuwa ni waasi wa Allied Democratic Force(ADF) kutoka Uganda ama ni waasi gani hao, je ni wale M23 waliosambaratishwa na vikosi imara kutoka nchini Tanzania? Na kama ni M23 ni nani yupo nyuma yao na ni kina nani na mana viongozi wa kwanza wote walishajiuzulu na kukimbia na wengine kujisalimisha mikononi mwa serikali na wengine walikufa katika uwanja wa mapambano.

Hakika yalihitajika majibu ya kina na viongoziuwaafrika waliamua kulivalia njuga suala hilo kwa kuwa vikosi hivyo vya waasi vimekuwa vivamia sana vikosi vya kulinda amani na kuuawa wanajeshi wao,lilikuwa ni jambo gumu sana kukubaliwa kirahisi kupoteza nguvu kazi zao kila mara na ndipo sasa majadiliano yakaanza,lakini wakati yanaanza tayari wasaliti walishaanza kutia figisu na Tanzania ikaamua kuingia kivyake bila taarifa na lengo ni kujua ni waasi wapi na ni nani yupo nyuma yao.

Sami alizidi kuchukua picha kwa kamera yake ndogo ya kiuandishi huku Kakere yeye akiwa bize kuchora ramani kila eneo walilopita bila kuacha alama yoyote.

Kila kitu kiliwekwa kifasaha kabisa.

“Sikia; ukiona tu msafara unasimama hakikisha unaskani haraka hiyo ramani na kuituma Eagle wing house mara moja bila kuchelewa.” Sami alimwambia Kakere huku yeye akiendelea kupiga picha licha ya magari kuwa katika mwendo mkali kidogo.

Hatimae walianza kuingia kwenye milima Meko na kwa ubovu wa barabara ilibidi magari yapunguze mwendo na ndipo ambapo Sami Kinyozi alianza kuona kile ambacho hawakukitarajia.

Walianza kuona vidungu (sehemu za juu wanazokaa walinzi kambini). Vidungu vilikuwa vitatu kwenye kilima kimoja na kwa haraka akakuza picha na kuona kila kidungu kilikuwa na wapiganaji wawili na kwenye kidungu kimojawapo kulikuwa kuna taa kubwa ambayo haraka Sami Kinyozi alijua ilitumika nyakati za usiku kuangaza maeneo ya vilima vile.

Sami aliendelea kumwelekeza Kakere kile anachokiona na mikono ya Kakere iliendelea kufanya kazi ya uchoraji kwa kasi sana bila kupitwa na neno hata moja.

Waliendelea kuona vidungu vingine pia kwenye maeneo mengine yaliokuwa yanazunguka vilima vile na wapiganaji wakiwa makini sana.

“Lakini sioni kama vidungu hivi vinakaliwa mara kwa mara ni kama sehemu zao za kupumzikia tu hawa jamaa” Sami alimwambia Kakere.

Msafara wa magari ukasimama na haraka Kakere akafanya kile alichoelekezwa na kutuma ramani ile makao makuu ambapo wao walipaita Eagle Wing House.

Kakere alipohakikisha amekamilisha kazi yake, haraka akachanachana ramani ile na vipande vile akavitupa nyuma ya siti na kisha wakatulia tuli kama vile hawakuwa wanajua kinachoendelea.

Mkuu wa doria wa vikosi vya kulinda amani Luteni Njeremi alikuwa wa mwisho kushuka huku tayari wanajeshi wake wakiwa wamemzingira kuhakikisha usalama wake.

Walikuwa katikati ya milima Meko na kwa haraka yalionekana kuwa ni makazi ya waasi wale .

Tofauti na kambi nyingi za waasi kuwa na bendera zao, kambi hii haikuwa na bendera yoyote ile.

Macho ya wanajeshi yaliona wapiganaji wengi wakiwa juu ya milima huku wakiwa wamewanyooshea mitutu ya bunduki.

Hakika ilitisha kukaa eneo kama lile; nyuso za wapiganaji zilikuwa zimetawaliwa na ukatili wa kutisha huku baadhi wakionekana kusota kwa njaa na hali zao zikiwa ni dhoofu.

Eneo lile lilikuwa limezingirwa na magari mengi ya wazi huku bunduki za msaada zikiwa zinatazama tu bila kutoa cheche na magari yale mengi yalikuwa ni Land Rover za kale na zilionekana kuchoka sana.

Kwenye kilima kimoja kulikuwa kuna tundu kubwa kama mlango wa pango na kimlango kile kilikuwa kina walinzi wenye miili mikubwa kuashiria walikuwa ni makomando waliokuwa wamefuzu kila idara na hawakuwa na nyuso za tabasamu kama vile walinzi wa rais.

Mkuu wa doria alibaki akiyasoma mazingira ya pale na huku akisubiri amri ya Sajini Lolo ambae alikuwa anashuka kwenye gari lake na kupiga hatua kuelekea kule kwenye kile kimlango cha pango.

Sajini Lolo alipotelea kwenye kimlango kile na alikaa huko kwa dakika kama nne hivi kisha akatoka akiwa ameongozana na mtu mmoja ambae alikuwa amevaa mavazi ya kijeshi na nyota moja begani yani alikuwa ni luteni usu.

Yule jamaa aliekuja na Sajini Lolo alimshika bega sajini aliekuwa ametangulia na kuzungumza nae kidogo kisha akasogea hadi walipokuwa wamesimama wanajeshi wa vikosi vya kulinda amani wakiwa wamemzunguka mkuu wa doria Luteni Njeremi.

Mtu yule alisabahi kisha akamuita pembeni Luteni Njeremi.

“Sikia bwana sisi hapa tumeishiwa chakula na tunahitaji chakula kama unavyoona vijana hawajala kabisa!” Luteni usu alizungumza huku akijitambulisha kwa jina Amolo.

“Sasa sisi tunahusikaje labda na kuwapeni chakula ninyi na kama mjuavyo sisi nao tunalishwa tu!” Luteni Njeremi alimwambia Amolo.

“Sikia bwana, unaweza kupiga simu na kuomba tuletewe chakula kisha tuwaacheni mwende mana tunajua kabisa ninyi ni walinda amani na mnahudumia misaada ya chakula na sisi tunahitaji msaada huo!” Amolo alimwambia Njeremi.

“Duh! Ni ngumu sana hii kitu na bahati mbaya sana chakula chote tumegawa huko tulikotoka bwana Amolo.” Njeremi alimwambia Amolo.

“Wala usiwe na wasiwasi kabisa mana chakula kitaletwa tayari mkiwa kama mateka wetu na mabadilishano ni chakula ambacho kitawakomboeni ninyi hapo!” Amolo alimwambia Luteni Njeremi.

Njeremi akastuka kidogo.

“Ina maana sisi ni mateka tayari sio?” Aliuliza.

“Siwezi kusema ni mateka moja kwa moja ila mkikaidi basi mtakuwa ni mateka Luteni” Amolo alimwambia tena Njeremi.

Njeremi ubaridi ulimwingia hadi miguuni.

“Sasa tuokoe muda Luteni; piga simu kwenye kamandi yenu tafadhali” Amolo alimsisitiza Njeremi.

Njeremi hakuwa na namna ilibidi achukue simu ya upepo na kuomba kijana wa mawasiliano waliekuwa nae pale ajaribu mawimbi mapya kwa kuwa walikuwa wamebadili uelekeo wa awali.

Kijana fundi wa mitambo akafanya kazi yake na mawimbi yakanasa na kilichofuata na simu kuanza kukoroma.

“01Alfa.. 01Alfa….” Luteni Njeremi alianza kuita kwa utambulisho wa kikosi chao.

Punde upande wa pili ukaitikia na kilichofuata ni maombi ya chakula ili wao watoke kizuizini haraka sana.

Tofauti na matarajio ya Amolo na wenzake; upande wa pili ulijibu ya kuwa kulikuwa hakuna akiba ya chakula kwenye stoo na labda kama wanataka kingine wanaweza kusaidiwa.

Amolo akatikisa kichwa kwa masikitiko kisha akaondoka pale na kurudi ndani ya pango.

Huko hakukaa sana, akatoka akiwa na haraka kubwa sana kama vile mtu alieanika uwele nje anawahi mvua.

“Kwani wakati mnakuja huku mlitoa taarifa makaoni mwenu?” Amolo alihoji.

“Kila tunakoenda lazima tutoe taarifa!” Luteni alijibu.

Amolo akakuna kichwa kama aliemwagiwa mchanga.

“Ok sawa!! Sasa hatuna muda mrefu hapa inabidi jambo lingine lifuate ikiwa tu mtakubali kutuachia silaha zenu hizo!” Amolo alimwambia Luteni Njeremi.

Ebana ee ikawa kama mmarekani kumyoa kiduku rais wa Korea.

Luteni aling’aka kwa gadhabu, mwanajeshi haachi silaha kwa adui labda awe amekufa na kuacha silaha ni kujisalimisha, sasa wao wanaambiwa waweke silaha chini kisha waondoke.

Hilo halijwahi kutimizwa na mwanajeshi aliekula kiapo hata siku moja.

Waliamua kukoki silaha zao baada ya kuambiwa na kiongozi wao wa doria.

“Bora mtuue tu kisha mchukue silaha ila sisi hatuwezi kukabidhi silaha hivyo hata siku moja!!” Luteni alimwambia Amolo.

Amolo nae akaamuru vijana wake waweke sawa bunduki zao kwa lolote..

Roho zikawa mikononi kila mmoja akitarajia kuchakazwa risasi nyingi kutoka kila kona ya vilima vile ambavyo wao walikuwa katikati yake bondeni.

Wakiwa wametulia kungoja amri zaidi kutoka kwa Amolo ama Luteni Njeremi; kwenye kile kilango cha pango akatokea mtu mmoja ambae alikuwa ni mrefu wa umbo na weusi wa kutisha huku sura yake mbaya ikiwa zaidi ya sura ya mamba.

Mtu yule alikuwa na jicho moja huku jicho lingine likiwa limezibwa na kipande cha ngozi “eye patch” na kushikizwa na ngozi maalumu kukizunguka kichwa chake.

Mtu yule alivyochomoza tu kila mpiganaji alitoa salamu kwa kugongesha kiganja chake na mgongo wa bunduki kiasi kila kona kukasikika mlio mkali kama vile kuna mvunjiko wa mti mkubwa.

Mtu yule alizungusha macho yake kila pembe na hatimae jicho lake moja likagota kwenye gari nzuri ya ford.

Akatazama pale kwa dakika moja zaidi kisha akasema

“Luteni mbona watu wengine wamejificha kwenye magari yako?” Alihoji bwana yule.

Luteni akageuka kutazama nyuma yake na kuona gari la waandishi wa habari na lile la msalaba mwekundu.

“Hao ni waadishi wa habari na watu wa huduma ya kwanza hawana neno!” Njeremi akajibu.

“Umesema wewe hawana neno, lakini lazima kuna wenye neno hasa hao walioko kwenye hiyo ford, washushwe tafadhali” Yule bwana alisema na neno lake ni sheria haraka wapiganaji wake wakalizingira lile gari na kuifungua milango kwa kasi na kuwaamuru dereva na wale waadishi wawili washuke.

Nao wakatii na kushuka.

Haraka haraka mizigo yao ikashushwa na wakaamuliwa kusogea mbele zaidi.

“Hao una hakika ni waandishi?” Aliuliza mtu yule.

Luteni akakubali na kutetea kabisa.

“Sawa!! Sisi tunakazi nao, hivyo wengine nendeni hawa mali yetu na tutawarejesha muda ukifika” Alizungumza bwana yule mwenye sura mbaya kugeuka kisha akaondoka.

Haraka Luteni akapiga simu makao makuu na kueleza hali ilivyo.

Uongozi ukawaamuru watoke huko haraka na wao watajua cha kufanya kuwaokoa.

Luteni Njeremi akaamuru vikosi virudi nyuma haraka sana kisha wakaondoka pale huku wakiona waandishi wao wakisukwasukwa kuingizwa ndani ya pango.

Ilikuwa hali tete kwa bwana Sami Kinyozi na bi Kakere Masuti.

Lakini Sami alijiuliza yule bwana amejuaje ya kuwa yeye si mwandishi na inaonekana ana hakika kabisa.

Subira yavuta heri ila kwao ikageuka shubiri huku wasijue hatima yao mikononi mwa waasi wasio na huruma kabisa.

Ilikuwa ni kufa ama kupona ndilo jambo walojiwekea waandishi wa habari wale.
 
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660


SEHEMU YA TATU




Luteni Njeremi akaamuru vikosi virudi nyuma haraka sana kisha wakaondoka pale huku wakiona waandishi wao wakisukwasukwa kuingizwa ndani ya pango.

Ilikuwa hali tete kwa bwana Sami Kinyozi na bi Kakere Masuti.

Lakini Sami alijiuliza yule bwana amejuaje ya kuwa yeye si mwandishi na inaonekana ana hakika kabisa.

Subira yavuta heri ila kwao ikageuka shubiri huku wasijue hatima yao mikononi mwa waasi wasio na huruma kabisa.

Ilikuwa ni kufa ama kupona ndilo jambo walojiwekea waandishi wa habari wale.

*****
Baada ya kuingizwa ndani ya pango lile; walipelekwa kwenye kona moja ya lile pango na kuamriwa kuvua nguo zao zote.

Lilikuwa ni jambo gumu kukubalika kwa kuwa wote mle walikuwa ni wanaume na ni bi Kakere peke yake aliekuwa mwanamke.

Kakere aliamua kujitetea kwa kuwasihi wasimdhalilishe kiasi hicho, lakini ilikuwa ni kama kumuuliza mbuzi tarehe..
Hatimae walimvua nguo zote kwa lazima.

Licha ya kuwa uchi lakini hakuna muasi ambae alionesha hata matamanio kwake.

Waliingizwa kwenye kona nyingine ya lile pango na huko wakapewa mavazi mengine na kisha wakaongozwa kuingizwa kwenye kona moja ambayo ilikuwa ni tofauti na kona zingine zote kwa kuwa kona hii ilikuwa ni nzuri na pia kwenye kuta zake kulikuwa kunawaka mishumaa na kwenye njia zake kulikuwa kumesimama walinzi waliokuwa kimya bila hata kujitikisa.

Sami Kinyozi na Kakere Masuti walikalizwa kwenye viti viwili upande mmoja na kisha wakawekewa meza mbele yao huku wakiwa na mavazi yanayonuka jasho na hayakuwa mavazi ya miili yao kwa kuwa zilikuwa kubwa kuliko Miili yao.

Waliachwa peke yao kwenye kile chumba bila kuambiwa lolote lile.


Walipoachwa kila mmoja alibaki na lake kichwani, huku wakiwa hawajui kabisa hatima ya maisha yao katikati ya mikono ya watu wale WA ambao hawakuonekana kuwa wema hata kidogo.

Kila alijikuta akiwa na mashaka kuhusu hatima yake kwa kuwa yule bwana mwenye jicho moja alionekana dhahiri kuwafahamu vyema wao kuliko wao wanavyomfahamu na pia walibaki wakijiuliza ni wapi hasa alipopata taarifa zao ikiwa hata kambini walipo hakuna anaejua hasa wao ni kina nani wapo hapo kwa ajili gani?

Lilikuwa ni swali gumu kujibika na hakuna alienyanyua kinywa chake kumjibu mwenzie.

Walibaki na yao moyoni huku hakuna aliejua ni nini kitafuata.

Ilikuwa ni baada kama ya dakika kumi hivi tangu waachwe pale peke yao, ndipo masikio yao yalinasa harakati za miguu ya watu zaidi ya wawili wakiingia kwenye kile chumba walichokuwa ndani ya pango lililoko kwenye mlima na kwa haraka haraka Zedi Wimba p.a.k Sami kinyozi aligundua pango lile lilikuwa ni moja ya kazi za wachimbaji madini wa kienyeji bila kufuata taaluma kwa kuwa lilikuwa halina mpangilio maalumu yani ni kama vile walichimba kwa majaribio.

Harakati za miguu zilizidi kukaribia na punde likatangulia kundi kubwa la walinzi ambao haikuhitaji lau elimu ya kidato cha sita kujua wale walikuwa ni makomando waliokuwa wamefuzu medani zote za kivita na makabiliano ya ana kwa ana.

Walitangulia makomando kama sita wakiwa na silaha kubwa na za kisasa kabisa zinazotumiwa na mataifa makubwa kwenye anga la vita.

Nyuma ya makomando wale kulifuata mwanamke mmoja aliekuwa amevaa kihasara hasara na nyuma yake alikuwepo mwanaume mrefu na mweusi kuliko neno weusi wenyewe.

Mtu yule alikuwa anatembea taratibu kama vile hakuwa na haraka yoyote ile na jicho lake moja alikuwa akilizungusha kushoto na kulia kama vile kinyonga.

Alikuwa ni yule bwana aliekuwa amevaa eye patch kwenye jicho moja na kuzungushiwa kamba kichwani ili kushika patch ile.

Jicho la Sami lilitalii vyema kwenye mwili wa yule jamaa na kuona namna mwili wake mweusi ulivyokuwa unaonesha ukomavu wa hali ya juu na pia ulionesha namna alivyopitia vikwazo vingi vilivyomwachia makovu kila mahali.

Lakini kuna kitu pia ambacho aliona kwenye ukosi wa shati alilokuwa amevaa jamaa yule na ilihitaji umakini wa hali ya juu kutambua alichokuwa amebeba yule mtu kwenye ukosi wake.

Alikuwa amepachika kifaa kinachotumiwa sana na majasusi kunasa sauti za mtu alanaeongea mita mia mbali nae.

Lakini kifaa hiki kilionekana dhahiri kupeleka pia sauti sehemu fulani mbali na pale wao walipokuwa.

Bwana yule ukosi wake ulikuwa umebeba UVH-Transmiter.

Sami alijiuliza swali moja tu kichwani

“sauti ile ilikuwa inapokelewa wapi na ni nani aliekuwa anatarajia kusikiliza maongezi yao na yuko umbali gani kutoka hapo wao walipo?” lakini hilo swali kulikuwa hakuna wa kumjibu bali alingoja muda utampa majibu licha ya kutokuwa na hakika kabisa juu ya uhai wake huko mbeleni.

Mtu yule alikaa na nyuma yake akasimama yule mwanamke alieingia nae na moja kwa moja akaanza kumsugua sugua mwili mwake hasa sehemu za mabega.

Mtu yule alikuwa ameshika sigara kubwa aina ya Siga na kuivuta taratibu kama vile mtu anaehofia kuunguza mapafu yake kwa moshi wa sigara ile.

“Naitwa Chepe! Sijui mwaitwa nani vile!” mtu yule alijitambulisha kwa sauti ya chini sana tofauti na umbo lake lilivyo.

“Naitwa Sami Kinyozi na huyu mwenzangu anaitwa Kakere Masuti” Sami alijitambulisha yeye na mwenzake.
Chepe alicheka kidogo kisha akavuta fumba moja la moshi na kuuacha upepe juu hewani baada ya kutoka tumboni kwa kupitia puani.

“Hapa Beni mpo kwa kazi gani bwana Sami” Chepe alihoji huku akijiandaa kupiga fumba lingine tena.

“Sisi ni waandishi wa habari tunaofanya kazi na makao makuu ya UN” Sami alijibu.

Chepe akaguna kidogo na kumtazama Kakere na kumuuliza

“Eti bibie ni ya kweli hayo?”

Kakere alitikisa kichwa kukubali.

Chepe akacheka kidogo kisha akasema tena.

“Na ni vipi nikiwaambia kwamba ninyi mwanidanganya?”

Kakere na Sami walitazamana kwa zamu kisha mmoja akasema

“Hatuna haja ya kudanganya wakati vitambulisho vyetu vipo na vinaonesha kazi zetu”

“Vitambulisho? Mh! Si hata mimi naweza kwenda hapo nikatengeneza tu bwana mdogo!” Mara hii Chepe aliongea kwa sauti kidogo huku akitupa chini siga yake iliokuwa imeisha na kuifumbata mikono yake pamoja na kuiweka juu ya meza.

“Unajua mimi nimezaliwa Tanzania na kukulia mitaani baada ya kukosa malezi ya wazazi; nilizaliwa na mateja wa pale mwananyamala kisiwani, kisha nikatelekezwa na kukulia kitaani, nilikuja kupata udhamini wa kushiriki mbio za kili marathon na huko nikaendelezwa kwa kupelekwa jeshini, nikafundishwa na wakufunzi mahiri sana akiwemo bi Hawa Maiga kisha nikaletwa huku Congo kulinda amani kama nuke see ila ndo hivyo sijarudi tena kupewa amri na mimi sasa natoa amri tu!” Chepe aliwapa simulizi yake kwa kifupi sana.

Kakere na Sami Kinyozi walitazamana kwa kutoamini masikio yao hasa kutajwa kwa jina la Bi Hawa Maiga; wao walimjua vyema sana mwanamama yule na ilikuwa ni ajabu kukutana na mtu aliefunzwa na mwanamama yule tena akiwa ni muasi wa jeshi la Tanzania na nchi ya Congo.

Ilikuwa ni ngumu kumeza ila ndivyo ilivyokuwa.

“Najua mnajiuliza kwa nini nimewapa simulizi ya maisha yangu!!” Chepe alisema huku akitoa eye patch kwenye jicho lake na kubaki na tobo kubwa lililokuwa linaogopesha kutazama.

Kakere alishindwa kurudia kutazama, akainamisha uso chini.

“Nimewambia ili mjua nawajua watanzania na ujanja wao, nawajua mbinu zao katika ulingo wa ujasusi na medani za mapigano hivyo msijaribu kunidanganya na hata mkinidanganya mjue mimi naujua ukweli kuhusu nyinyi!” Chepe aliwambia kisha akachukua eye patch na kuiweka tena usoni na kutoa mkebe sigara kali na kuanza kuvuta.

“Narudia tena kukwambia kwamba hatuna sababu za kukudanganya na kama nilivyojitambulisha ndivyo ilivyo na hakuna la zaidi!” Sami nae aliendelea kujipa ukiburi mbele ya Chepe.

Chepe akacheka kidogo na kuvuta fumba la sigara kali kisha akakohoa kidogo kwa ukali wake.

“Umesema unaitwa Sami Kinyozi sio!” Chepe alimhoji Sami.

Sami akaitikia!!

“Unaonaje nikikuita Zedi Wimba?” Chepe alihoji huku jicho lake kali likiwa usoni mwa Sami.

Sami alijua kwa nini yule bwana alikuwa akimtizama namna ile.
Alijua yule bwana anataka aone msituko wake ili ajiridhishe na taarifa yake..

Sami au Zedi Wimba hakuwa kuhadaika kizembe namna hiyo.

Nae akamtazama Chepe usoni tena akiweka uso wa msahangao kabisa kuonesha Chepe anakosea kumnasibisha na Zedi Wimba.

“Hapana!! Jina langu ni Sami Kinyozi mkuu wala huyo mtu hana mahusiano kabisa na mimi!!” Sami alizidi kukataa jina la Zedi Wimba.

Chepe akatabasamu kiupande na kumtazama Kakere kisha akasema

“Na wewe una kataa huitwi Minata Daudi au Mina kwa kifupi?” Chepe alimhoji Kakere.

Kakere nae akamkazia macho na kukataa kabisa hilo jina na tena hawajawahi kulijua kabisa.

“Unajua wakati natoa Patch yangu usoni nilitaka muone uso wangu ulivyoharibiwa; kipindi hicho nilikuwa double agent kama nyie na tena nyie ni spy tu wala hamna taaluma ya kufuatulia counter terrorism na ndo mana mmefahamika kirahisi” Chepe alizidi kuwanyumbua wageni wake huku akizidi kuvuta sigara yake.

“Nilitolewa jicho katika harakati zenu hizi na niliahidi kumtoa jasusi yeyote kutoka Tanzania endapo ningekutana nae anga zangu, najua mnajiuliza kwa nini!” Chepe aliendelea kusema bila wasiwasi na chumba chote ilikuwa inasikika sauti yake tu huku walinzi wake wakiwa kimya na kufuatilia kila alichokuwa anafanya Sami mana taarifa zake walikuwa nazo hivyo hawakutaka kuzidiwa ujanja nae.

“Nimewambia hivyo kwa sababu nilitolewa jicho wakati naipogania nchi yangu ila niliporudi wakanitenga na kuniweka kwenye kundi la walemavu huku wakinipa misaada kidogo sana na nilipowaomba wanirudishie japo jicho la kondoo walinikatalia kabisa na tena wakanileta huku msituni kulinda amani nikiwa hivi….” Chepe alizidi kuwambia wageni wake wale..

“Hivyo epukaneni na adhabu hii, nambieni ukweli ninyi ni kina nani hasa na hapa Beni mnafanya nini!’ Chepe aliwahoji tena.

Walikaa kimya!!.


“Ninyi ni watanzania wenzangu ndo mana sijataka kuwaacha mhojiwe na vijana wangu, hivyo nilipeni fadhila tafadhali!!” Chepe alizidi kuwasihi.

Wakati Chepe anangojea majibu ya Sami na Kakere mara akaingia Sajini Lolo akiwa na haraka kubwa na kwenda kuteta jambo na Chepe kisha akaondoka na Chepe nae akatikisa kichwa mara mbili tu na kusimama.

Hapo ndipo ikazuka tafrani kubwa na hekaheka za kutosha..

Wapiganaji walifanya hima kumsindikiza Chepe huku wengine wakiwasomba mzobe mzobe Sami na Kakere na wengine walishugulika kuwafunga sura zao ili wasione.

Hakuna kati ya Sami ama Kakere aliejua ni wapi wanapelekwa na ni kitu gani kilikuwa kimetokea hadi kuondoka haraka namna ile japo walihisi tu watakuwa walipata taarifa ya kuonekana vikosi vya kulinda amani vikielekea eneo hilo kufanya uokozi wa waandishi wao wa habari.

Sami na Kakere walitupwa kwenye gari kama vifurushi vya viatu vya bondo alimaarufu saa sita utanikoma.
H
Hawakujua wanapopelekwa na ni nini kitatokea huko.

Ila kuondoshwa kwao katika mapango ya milima Meko ndio kukazua kizaazaa na ikawa ni kufa kupona katikati ya Mji wa Beni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom