Operation Sangara: Chadema yajipanga Upya

Kwangu mimi hawa Mwaipopo et al ni njaa tu.

Na kwa JF imepatikana platform nyingine ya kutukana waislam kwa ujumla wake kutokana na matamshi ya so called BAHA wot-eva!
 
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kauli iliyotolewa juzi na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupinga oparesheni Sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), si kauli ya waislamu wote.

Akizungumza mjini Morogoro kwa niaba ya Kaimu Mufti wa Tanzania, Shekhe Suleiman Gorogosi, mratibu wa habari wa Bakwata, ustadhi Issa Mkalinga alisema kauli hiyo ni ya waislamu wachache ambao wamekuwa wakitumiwa na
viongozi wa kisiasa kwa manufaa binafsi.

Ustadhi Mkalinga pamoja na Mkurugenzi wa Utawala, ustadhi Karim Mataliwa, aakizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kaimu mufti huyo ya kutembelea mikoani kuhamasisha uhai wa baraza, alisema baraza halitambui kauli hiyo na wala halijihusishi na mambo ya siasa.

"Ujue tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani, hivyo wako baadhi ya wanasiasa wanatumia mwanya wa majukwaa ya dini kupeleka ujumbe wao," alisema. Akizungumzia ziara ya kaimu mufti mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Utawala alisema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu aliyojiwekea kaimu mufti ya kutembelea baraza katika mikoa yote Tanzania na kwamba kaimu mufti ametembelea Dodoma na Morogoro na atatembelea mikoa mingine.

Ustadhi Mataliwa alisema lengo la ziara hizo ni kutaka kujua uhai wa baraza na matatizo yanayolikabili baraza katika ngazi hizo ikiwa ni pamoja na kuhimiza kufanya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi kuanzia ngazi ya msikiti hadi taifa utakaoanza kufanyika mwezi April mwaka huu.

Wakati huo huo, katika mahojiano na baadhi ya waumini wa dhehebu hilo,
mkoani Morogoro wameunga mkono kauli ya Bakwata na kudai kuwa viongozi wa dini ni vema wakafanya shughuli zao za kiroho na kuwaacha wanasiasa kufanya kazi zao za siasa.


Mmoja wa waumini hao, Ismael Rashid, alisema tamko lililotolewa na waislamu katika kongamano la jijini Dar es Salaam la kudai kuwa Chadema haina manufaa na msaada wowote kwa uislamu si maneno ya kiungwaana na si vema kukipakazia chama hicho kwamba ni kikabila na cha kibinafsi.

Rashid ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Jahazi asilia mkoani Morogoro alisema hatua iliyochukuliwa na Chadema ya kuacha kuunga mkono vyama vya CUF na Sauti ya Umma (SAU) ilikuwa ni sahihi kwa sababu chadema walisimamisha mgombea ubunge katika jimbo la Mbeya vijijini lakini vyama hivyo vilimwekea pingamizi mgombea huyo na kuenguliwa.

"Pingamizi hilo lilisababisha mgombea ubunge wa Chadema akaenguliwa kugombea nafasi hiyo, sasa iweje chadema iwaunge mkono?" alihoji Rashid

Alisema chama cha Chadema hakiungi mkono kampeni za mgombea wa CUF kwa mdai kuwa chama hicho, mwakani inakusudia kusimamisha mgombea wake katika jimbo hilo kwa hiyo kama Chadema ikiunga mkono CUF itashindwa kusimamisha mgombea wake hapo mwakani.

SOURCE:http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=9217
 
Waislam 35% ya population ya Tanzania, wakristo 30%, imani za kienyeji 35%; sasa ukiigawa nchi kwa waislam na wakristo wale wengine inakuwaje? Acha uzushi!
Wewe nae kwenye huu ulimwengu wa siku hizi mpaka utafuniwe! Utakuwa ulikuwa mtu wa mkoba aka desa sana chuoni kwako! Jaribu CIA factsheet au Wikipedia Tanzania kabla ya kuja na maswali kama haya ili uwe na mwanga kidogo tu, au njoo na alternative statistics!

Buy By.
 
Waislam 35% ya population ya Tanzania, wakristo 30%, imani za kienyeji 35%; sasa ukiigawa nchi kwa waislam na wakristo wale wengine inakuwaje? Acha uzushi!


Mkuu hiyo sensa alifanya nani na alifanya mwaka gani? au ndio unatumia estimates za CIA ambazo hazina msingi. sio uzushi kuna watu wengi sana wanaojiiita waislamu wanafanya mambo ya kijinga kwa kutumia kivuli cha kiislamu. Kuna mamia ya watu wanasema Tanzania ni nchi ya kikristo eti kisa inafuata sheria za kiingereza ambazo ni za kikristo. Kuna wengine wanaosema serikali inawanyanyasa waislamu, hata Zanzibar kuna wanaosema hivyo kuwa serkali ya Visiwani inawanyanyasa waislamu. Kuna wajinga wengi wanaupaka matope uislamu kwa kisingizio cha maslahi ya waislamu lakini ukweli ni njaa yao tu.
 
"Ujue tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani, hivyo wako baadhi ya wanasiasa wanatumia mwanya wa majukwaa ya dini kupeleka ujumbe wao," alisema. [/url]

Wanasiasa gani hao, tunaweza kutajiwa majinan yao ili tujue jinsi ya kuwakemea na kuwaepuka
 


Mkuu umenena sawa. Lakini ukiangalia uhalisi wa mambo utaona kuwa ni rahisi sana kwa dini ya kiislamu kuwa hijacked na kutumika vibaya. Na watu wanatumia weakness za dini hiyo kuradicalize watu na kufanya ujinga wao. So far ukiangalia utaona kuwa wasilamu hawajaungana, na sababu ni kuwa waislamu wa kweli hawapendi ujinga, wanafuata dini tu hawataki kutumika na kuchafua dini.

Umewahi kusikia kuwa wakristo waeandamana kudai kitu fulani? au wameandamana kuunga mkono kitu fulani? au kuilaani serikali au kukilaani chama fulani kuwa hakiwatendei haki wakristo? Mimi sina kumbukumbuku, lakini nina kumbukumbu kuwa serikali hasa ya mwalimu ilifanya injustice kubwa dhidi ya wakristo na kupora shule karibu zote zilizokuwa zinaitwa shule za mission na kuziharibu, leo shule hizo na nuu magofu na perfomance zimeshuka sana. Lakini hayajawahi kutokea maandamano, labda hao waikristo ni wajinga.
 

- Mkuu haya maneno yako ndio uzushi wenyewe wa kidini na yanashusha heshima yetu hapa JF kwa sababu huwezi kuonyesha ushahidi wake, acheni machochezi ya kidini hapa JF, Mods it is about time mkaifunga hii thread sasa maana this is beyond ustaarabu!

This is a pure nonesense tena ni sad kwamba inaweza kutolewa na a man of your academic status, aibu tupu kwani huwezi toa ushahidi mzito wa hizi empty claims!
 

Well Mkuu mimi hii sishangai, kuna maprofesa, Ma-Dotor na hata graduates wengi line zao za argument inapofika kwenye suala la dini inakuwa kama wanapteza akili zao. I wonder tatizo ni nini, lakini ukweli ni kuwa it is nonsense, unaweza kushangaa akili za hawa wasomi huwa zinaenda wapi inapofikia. Jaribu kufuatilia habari kuhusu msikiti wa Arusha na uone comments za "wasomi" unaweza kucheka sana.
 
Sioni connection ya operation Sangara na Dini?
Aliyeongea hayo sishangai bse tumezoea mengi ya ajabu toka kwao.
Sijui tatizo shule au jazba!
That being the case wakristu nao wataanza sema CUF ni ya WAISLAMU?
Tunakwenda wapi jamani?
Habari kama izo hazifai ata kuandikwa kwa gazeti since zinawakilisha kuishiwa sela kwa msemaji au usikute ni mamluki wa chama.
Walai wale wa EPA wote wangekuwa waislamu ungesikia tuu,thank God hawakua.
Nimegundua shule ni muhimu kuundoa ujinga
 
bwana Njowepo tatizo sio shule Tatizo ni kuelimika, Wakati nchi ilipokuwa inapata uhuru hatukuwa na wasomi wengi lakini watu walikuwa na uelewa na walikuwa wanajiachia kuelimika
 
Hayo aliyoyasema sheikh Said Mwaipopo yana baraka ya viongozi wengine wa dini yake,wafanyabiashara maarufu na wanasiasa.Hajakurupuka.Amekuwa katika movement ya kuueneza uislamu kwa kuzikasifu dini nyingine haswa ya kikristo kwa kipindi kirefu.Amefanaya mihadhara ya kukashifu Ukristo na kuyaponda maandiko yaliyomo ndani ya Biblia.Ni mhadhiri wakutegemewa haswa.Nenda Dar es salaam,pale shule ya Uhuru karibu na kituo cha mabasi yanayokwenda Tandika utapata habari zake/zao.
Kwa wataokumbuka(walioangalia CD za mdahalo wa wakristo na waislamu uliofanyika pale Diamond Jubilee mwaka jana) aliposimama alishangiliwa sana.Maana yake anakubalika katika jamii hiyo kwa kazi kupinga imani nyingine.
Hawa watu(yeye na wahadhiri wenzake) hawana pesa wala kazi rasmi(ya kudumu) ya kuwapatia kipato.wanachofanya ni kupanga wapi wakafanye mhadharak, kisha huenda kuomba fedha kwa hawa matajiri HASA wa mafuta.Mara nyingine huwekewa dau na waislamu wenzao kisha huangalia lipi ni kubwa na kisha huenda huko.Pia walipata msaada toka DIC (Dar es salaam islamic Club); ambayo hii imetoa mawaziri kadhaa ktk baraza la mawaziri lililopo.
Kwa wanaomfahamu itakumbukwa huko ktk miaka 2005-07 kuna kipindi kirefu amekuwa akitembea na kufanya shughuli akiwa DAR na bwana mmoja ambaye kwa wakati huo alikuwa msemaji wa CUF.
Hapa, sina uhakika, kama msukumo huo unatoka CCM au CUF.Toka CCM ikiwana maana ya kuwagonganisha wapinzani(kwani CCM wanakihofu CHADEMA sana kwasasa na strategies zake) ili wao wawezeshinda.Ama toka CUF baada ya ule ushirikiano kuvunjika(waCUF na CHADEMA, na vyama vya upinzani kwa ujumla).WAMEPIGWA KIBUTI MBEYA.Kwa mwendo wa siasa zinavyokwenda CHADEMA inaonyesha inaweza simama vizuri.Wali-prove pale waliposhambuliwa na kuzushiwa na vyama karibu vyote vya siasa, na mwisho kushinda kule Tarime.
Mkuu mmmoja ameuliza humu janmvini kwanini watu wanakuwa sensitive sana na mada za kidini/element za udini.Ukweli ni huu,SIASA ZA UDINI NI HATARI. Chama chochote cha siasa kisitake kupata support kwa kuegemea udini.HAKUNA NCHI ILIYOINGIA KWENYE MGOGORO WA KIDINI IKAWA SALAMA.
Mwaipopo na wenzake wanasema CHADEMA haina mwelekeo wa kuwasaidia waislamu,sawa.Je wamethibitisha haina uwezo wa kuwasaidia watanzania bila kujali dini zao? Siasa hizi za UDINI,MIMI SIZIKUBALI. naamini wote wanaiwazia mema Tz wanazichukia.
Tusubiri yatakayojiri ilihali tunaikemea tabia hii.
 
Mara nyingine huwekewa dau na waislamu wenzao kisha huangalia lipi ni kubwa na kisha huenda huko.Pia walipata msaada toka DIC (Dar es salaam islamic Club); ambayo hii imetoa mawaziri kadhaa ktk baraza la mawaziri lililopo.

fafanua imetoaje mawaziri?!
 
haya yote yameletwa na Rais wetu. Kwa wale muliosikiliza idhaa ya kingereza ya BBC asubuhi, hawa ndugu wanadai wanaipongeza serikali ya awamu ya nne na rais kwa sababu amewapa uhuru wa kufanya mihadhara waliyozuiwa na serikali iliyopita. Mihadhara yenyewe nadhani munajua inazungumzaga mambo gani. Kukashifu Biblia na kutukana wakristo. Kwa nini waruhusiwe. wenzetu kufanya vurugu kutetea dini sio issue, tena ni thawabu. sisi wengine hatuhubiri kwa msuli na jambia mkononi, wenzetu wamefunzwa hivyo. sasa wanataka kutawala nchi

Rais anaonesha wazi upendeleo wa kidini katika serikali yake. anajaribu sana kuweka watu wengi wa dini yake kwenye serikali for future purpose. wengine uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana. analazimisha dini na wanawake na sio uwezo wa mtu. hii ni hatari na ndio inawapa kiburi waislam. wewe umewahi kuona katika tanzania waislam wanatetea serikali? kila mara wamekua wakilalamika kuwa serikali inawaonea. Cha ajabu kipindi hiki wanaishabikia na wa wanasema wanasikiliza na wanangoja maamuzi yake juu ya OIC na Kadhi court. Wanajua wanachokisema na kukifanya.

Kati ya kosa atakalolijutia Kikwete ni hili la udini. Mimi nadhani viongozi wetu wanaapa kuwatumikia wananchi na sio dini zao. zaidi sana tunategemea dini zao ziwasaidie kuwa watu wema na waaminifu na sio kuweka misingi ya dini. itakuwaje kesho tukiwa na rais wa kikristo naye akaamua kulipiza kisasi? je huku tunapokwenda hatutachagua viongozi kwa dini zao? Mungu atuepushe maana hii ni hatari kubwa sana kwa taifa letu.
 

Swadakta Bro YournameisMINE! Ni kweli uyasemayo... na ni mara nyingi huwa ninasema na nitaendelea kusema kuwa JF imejaa udini, kiasi inatia kinyaa kinacho sababisha kichefu chefu...! Sishangai na wala sitashangaa thread kama hii na nyingine zenye kugusa iman za Waislam zikabakishwa kwenye kumbi tofauti ya ukumbi wa Dini/Iman.

Leo nimesoma thread inayosema "...Mchungaji Dakta Herry Mhando kuanzisha kanisa lake la 'Wasabato Wapentekoste' " Haikuchukuwa hata saa tangia thread ibandikwe Moderator (s) wamaeihamisha kwa speed ya ajabu. Wakati nipo online nasoma na kuandika nilicho andika nikajikuta naibukia kwenye jukwaa la wakereketwa (Dini/Iman). Nikabaki Aaaah!

Wenye JF hawatakaa na kuwa fear hata siku moja...!?
 
Binadamu wote sisi ni wadini! Kila mtu anatetea anachokiamini.

Waislamu ndugu zangu..inabidi wakubali positive criticism.

Mimi naamini and I say it again, waislamu especially Tanzania..inabidi waamke..waweke msisitizo kwenye elimu dunia!....dunia ya leo huwezi kwenda darasani ukaweka mkazo kwenye quran baadala ya Chemistry au Physics.. (By the way I have seen this not only in TANZANIA BUT ALSO IN SOME OTHER ISLAMIC COUNTRIES I HAVE WORKED IN) Nimeona malalamiko mengi sana ya wenzetu wakisema kwamba wanaonewa epecially na wakristo. What I can say: invest in education. kama ni seminary za waislamu support wanafunzi wakate nondo..washindane na akina URU, MAUA, KATOKE, MAKOKO etc.... Otherwise..hali ikiendelea hivi, malalamiko ya marginalization hayataisha. Dunia ya leo imebadilika sana... Hivi tujiulize ni shule ngapi za waislamu ambazo zinapaform vizuri Tanzania? I bet zitakuwepo ila siyo nyingi. How about kile chuo cha Morogoro? Hope kinafanya vizuri. This is historical but also its because its perpetrated by some of the so called viongozi wa hizi dini..who believe to be custodians of ethics and morals. Na ofcourse they have answers on who is to blame for all these problems.

Friends accept this as a positive criticism. Hizi dini..uwe ukristo, uislamu, uyahudi ni imani tuu..hazitupeleki popote-ni imani yako tuu. Taasisi za dini Tanzania kama RC, NA WALUTHERI nadhani sasa wanaongoza kwa mwamko wa elimu kwa kuwa na vyuo vikuu vingi..hata Anglican nao sasa wameamka wana St. John University Dodoma! Hata wasabato... are catching up!

Kwa Tanzania, I would advise waislamu (baadhi ya viongozi wao) waachane na hizi short term planning za kugombana na Chadema au CCM..these are politicians..they will use you and they will damp you when you are of no use to them. Period. Mfano hawa mashekh wangewafuata hawa matajiri akina Manji et al..wakatoa hela ya kuleweka kujenga vyuo na shule! This is the only route towards true liberation ya waislamu..Progress is about lobbying...play your cards well.

Hizi sentiments ..oohhh.. Fundi, YN, Mkandara nk...ni mdini..nani mdini...will always be there....Ila tukiendelea na haya malumbano ya nani mdini..tutashindwa kufanya yale tunayotakiwa kufanya...in the process waislamu wataona kwamba kila mtu is against them...Ndo maana hata Middle east..progressive muslims wameshaamka..sasa hivi wanajenga vyuo, mahospitali.... kuwapeleka watoto wao kwenye best American/European colleges...We all know what an idle mind can do..Na kama umeshagundua Tanzania...wakristo hawapendi kulalamika..wanajua what it takes to be at the summit.

Mwisho nasema, dini ni imani ya mtu, huwezi mzuia mtu asifikirie anachotaka kufikiri. Kama nimeamua kuamini kwamba Mkandara au YN or Fundi ni mdini..hata kama ukinishauri vipi..I will always think so! Cha muhimu watu wajipange waweke mikakati ya kujiletea maendeleo.
 
YournameisMINE umesema kweli. Tatizo la sasa JF, mada yoyote yenye mwanya wa kuingiza Dini, basi kuna watu huingia kuutusi Uislamu, nawana julikana. Katika Thread ya "Ustadh akamatwa!!! niliwahi kuandika kuuliza kwanini ile thread inaachwa wakati masuala ya Dini ni "Private", nilijua itahamishwa haikuhamishwa. Kwanini nilijua itahamishwa, hapa katika hii forums mods hufanya mambo kwa wakati, ukisema tu mods hii thread mpya iunganishwe na thread fulani, utakuta baada ya muda wanafanya hivyo. Sasa nilipoandika hiyo post wakakaa kimya, na post yenyewe ni no. 51 (Jan 3, 2009) katika thread ya "Ustadh akamatwa!!!, niliandika ifuatavyo:-

"pia kuna suala linanitatiza, sijui kuna wakati mods wa jf hawaoni ama wanaacha. ukumbi wa dini ni "private", lakini hili limeachwa. Sasa nawashauri muufungue uwe kama habari nyingine ili tupate kujadili kjwa uhuru. Sio inaonekana ni "private", lakini bado kuna mada za dini si "private".
 

Eeeh! hata wewe humo kwenye kundi hilo hilo...!? Hypnotised... Hawakusoma... hawapendi kusoma... elimu dunia... elimu... ah ah ah... Sasa hata Historia ya dunia pia inakushinda kuisoma na ukaelewa mchango wa hao unaodai kuwa hawakusoma...!? Hizo elimu za chemistry au Physics unajuwa asili yake...!? Kaaazi kweli kweli!

Mmh! Sasa kwa mtazamo wako... tuchukulie kuwa hawakusoma...(!?) Je hao waliosoma na wakasoma mapaka wakasoma...! Ndipo walipo tufikisha hapa!? Unataka kunambia kwenye hiyo theory yako ya "Hawajasoma" Hao ambao unadai hawajasoma hawana mchango wowote katika uongozi wa nchi hii...! Kwa mantiki hiyo basi nchi imejaa ufisadi, elimu imekuwa bomu... uchumi clinical dead... Watz wamekuwa maskini wa kutumwa...! Azimio la Arusha... Vita vya Kagera... Maduka ya kaya... Vita vya Waujumu uchumi... Haya yote yatakuwa yameletwa na hao waliosoma.... Vipi hapo?

Wakati wa harakati za kuondoa ukoloni... wapo waliosema hawa nao... Kila kukicha migogoro tu...! Hivi watamuweza mjerumani...!?

Tunawasoma kwene historia... wakina Mkwawa na kina Mirambo...! Leo hii Wtz wanajivunia historia ya nchi hii... Lakini wanasahau michango ya hao mnaodai hawakusoma...! Hivi kweli hawakusoma!?

Hivi mtawacha lini ulimbukeni wenu...!
 
Hivi hizi dini zilitoka wapi? Hizi dini dini dini ni Siasa tu nazo kwangu mimi naona hazitengamani.
Ila ukiniambia Mungu na Siasa hapo ndipo nitakwambia ni vitu viwili tofauti lakini dini na siasa ni kitu kile kile.

Mfano maji kile kimiminika cha kunywa na kupikia chakula wewe ukikita MAJI na mimi kimiminika hichohicho nikakiita KUBWA JINGA kutakuwa na tofauti??
 
Huu mjadala haukustahili hata kuwepo in the first place. Sababu hauna maslahi kwa taifa. Sanasana una radicalize watu wa both sides. Ntashangaa sana kuona kama kuna mtu anatarajia dini yake kushinda such mjadalawa wa kidini... Its not gonna happen!

Mi tatizo langu ni hivi vyombo vya habari vyetu na wahariri wetu. Hivi hilo jukwaa la wahariri hawana mwongozo wa common stand when it comes to issues of national interest?... I mean hayo magazeti kuwaandika kina Mwaipopo kila kukicha kunawapa more mileage kina mwaipopo kuliko wakizunguka kwenye mihandara mwaka mzima.

Its about time wahariri waweke utaifa mbele. wakubaliane tu kuwa kwenye mambo ya national interest, lazima wawe na common stand. Hakuna kuwapa airtime au coverage kwa waharibifu wa national interests. Watu wanaogawa watanzania wanini kuwapa airtime. Hata awe mwanasiasa gani asipewe airtime. Wenzetu nchi zilizoendelea wanavitu kama hivyo. Vita ya Gazza wamarekani wa kawaida wanaoneshwa mateso ya israel tu, kwa hiyo lazima wawaunge mkono,... Lakini hiyo ni sawa kwa ajili ya national interest yao. Na hiyo nchi ndio kinara wa demokrasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…