Operation DUSTCOVER: Mawimbi Yame-Intercept Kabla ya Code Kuingizwa kwenye Server

Operation DUSTCOVER: Mawimbi Yame-Intercept Kabla ya Code Kuingizwa kwenye Server

TUsioelewa tuko wengi ngoja tuone kama nyama ziko chini tuzikombee mchuzi ukiisha
 
Kaeni na mafumbo yenu yote na viingereza uchwara ila mjue tu tumechoka kuomboleza misiba ya watu wasio hatia kila siku, mengine Kaeni nayo tu mpeane na kina kifua kipana mkwe, sisi tunataka vifo vyetu vitokane na mapenzi ya Mungu tu mengine yote yenu
 
Katika mazingira ya Tanzania ya sasa, wapo watu wanaotumia jukwaa la dini kuendesha siasa za kivuli, kwa nia ya kupunguza uhalali wa mamlaka ya nchi. Mfumo wa usalama umeshatambua njia hizi — hata pale zinapokuja kwa sura ya uongozi wa kiroho.
Whatever the case kila anayekemea utekaji na mauaji na arbitrary Detention tupo naye kenge, period
 
Usiumize kichwa, hamna jipya.
Sasa kama tunatakiwa tusiumize kichwa, hamna jipya, huu uzi na ma conspiracy theories yote haya, na kujitutumua kote huku kujionesha Jason Bourne ni kwa nini?

Unatuletea thread ya kuumiza kichwa yenye ramli kibao, halafu watu wakiuliza maswali unasema wasiumize kichwa, hamna jipya?

Huoni contradiction hapo?

Au huu uzi ni wa riwaya za kuchangamsha ukumbi tu?
 
Wewe hata uongee Kwa matumbo na lugha isokuwepo.

Gwajima anatuwakilisha tulio wengi.

LISSU anatuwakilisha .

Kwa Ufupi, CCM na Samia wake hatuwataki Kwa namna yoyote
Katika majira haya yenye kelele zisizo na ala, tunalazimika kunyoosha antenna zetu kupokea kile ambacho hakijasemwa wazi. Japo mitetemo ya chini ya ardhi haionekani kwa macho ya kawaida, waliofunzwa kusoma hewa tayari wameshaweka dots kwenye ramani ya mwelekeo.

Kwa muda mrefu, baadhi ya wahudumu wa mwanga bandia wamekuwa wakicheza michezo ya kivuli, wakijivika kanzu za rohoni huku wakitekeleza protokali za kitengo kisicho rasmi. Wanajifanya manabii, kumbe ni ma-agent wa mpango unaofadhiliwa nje ya perimeter ya Taifa.

Katika lugha ya operesheni, wamekuwa wakipiga soft codes kuhusu “mwisho wa mpango”, wakitumia maneno ya kiroho kufunika intel drops za ajenda ya kupindua msitari wa amri kuu. Kaburi halijachimbwa, lakini wao tayari wana orodha ya wasomaji wa hitma.

Operesheni yao iliitwa “Dark Days”. Ilijikita kwenye principle ya target destabilization. Malengo yakiwa ni mmoja, lakini njia walizochagua zilikuwa za kuteremka giza kwa kutumia taa za bandia. Kwa bahati mbaya kwao, mlengwa aliingia kwenye secured zone kabla ya trigger sequence kutimia.

Taarifa za deep comms kutoka kwenye mitaa ya kimya zimeshatambua walengwa na walengaji. Aliyevaa kivuli cha username sasa ana sura kamili kwenye mfumo wa face recognition. Hawa si wapambanaji wa haki, bali ni watoa taarifa bandia kwa bei ya kiapo cha hila.

Harakati za kutabiri “mabalaa ya uchaguzi mkuu” zilikuwa sehemu ya psyop campaign. Wengine waliingiza jina la mpita njia maarufu kwenye skripti ya mwelekeo wa bendera, lakini kwenye meza ya war room, script yao ilishakataliwa.

Wamesahau kuwa baadhi ya maombi ni silaha za kimya. And those who pray in encrypted tongues have already activated firewall ya taifa. Vazi lao la uaminifu sasa limechanwa, na mfumo wa kufuatilia miendo yao uko kwenye live monitoring.

Kwa sasa, watendaji wa kazi ya chini ya ardhi wameingia phase two: neutralization ya propaganda, kufuta metadata ya hila, na kuzuia access ya red zone kwa wale waliopoteza malengo.

Kwa kifupi, kifaa cha kufukua kaburi kimefungiwa. Wale waliotumwa kwa giza sasa wamelazimika kutafuta nuru bandia ya kukimbilia. And just as it’s said in the field: He who operates at dawn will face dusk before his time.
 
Kaeni na mafumbo yenu yote na viingereza uchwara ila mjue tu tumechoka kuomboleza misiba ya watu wasio hatia kila siku, mengine Kaeni nayo tu mpeane na kina kifua kipana mkwe, sisi tunataka vifo vyetu vitokane na mapenzi ya Mungu tu mengine yote yenu
Viingereza vingi lakini ukivichambua pumba tupu.
 
Sasa kama tunatakiwa tusiumize kichwa, hamna jipya, huu uzi na ma conspiracy theories yote haya, na kujitutumua kote huku kujionesha Jason Bourne ni kwa nini?

Unatuletea thread ya kuumiza kichwa yenye ramli kibao, halafu watu wakiukiza maswali unasema wasiumize kichwa, hamna jipya?

Huoni contradiction hapo?

Au huu uzi ni wa riwaya za kuchangamsha ukumbi tu?
Hahaha wabongo tunajifanyaga tuna akili na viingereza uchwara wakati hatuna uhakika wa kurudi kwnye slums zetu jioni! Hii ni takataka tu kama zingine, wakija genzee wa Kenya hapa wote tunaingia uvunguni
 
mleta Uzi asizingatiwe! hana issue. wanajiona wao ndio wanapaswa kuishi na sio wengine. Mdude ana tofauti gani na Abduli.

waliokutuma waambie wananchi tuko nyuma ya wapigania haki.
 
Hawa wapiga ramli na sisi tukiwapigia ramli kwamba wametumwa na CCM kupoteza watu akili tutakuwa tumekosea kweli?
 
Kiufupi ni GWAJIMA alitumia MANABII wenzake kutengeneza TABIRI za kutisha kuelekea UCHAGUZI 2025, lakini wenye nchi yao wameshamng`amua sasa wanadili nae..
 
mleta Uzi asizingatiwe! hana issue. wanajiona wao ndio wanapaswa kuishi na sio wengine. Mdude ana tofauti gani na Abduli.

waliokutuma waambie wananchi tuko nyuma ya wapigania haki.
Kuna Watanzania wengi bado wana fikra za kizamani za kudhani ukiungaunga viingereza vingi na kujinadi unajua Usalama wa Taifa sana za ndani ndani, ukiungaunga vimsamiati na vinukuu vichache vya Kiingereza, ukiwekaweka vi code vya uongo na kweli vichache, basi watu watakuamini.

Wakati watu tuna uwezo wa kuangalia kwa dakika tano tu tukajua kuwa this is showboating performative distraction.
 
Hawa wapiga ramli na sisi tukiwapigia ramli kwamba wametumwa na CCM kupoteza watu akili tutakuwa tumekosea kweli?

Yani kila mtu mchumia tumbo sasa hivi atajifanya usalama wa taifa na kuja na mafumbo hapa apate tu kula bure, wasitupoteze njia sisi tumechoka damu zisizo na hatia kumwagika bure tu na kila anayepinga hata kwa unafiki tutakua naye tu bila kujali katoka wapi wala historia yake!
 
Kaeni na mafumbo yenu yote na viingereza uchwara ila mjue tu tumechoka kuomboleza misiba ya watu wasio hatia kila siku, mengine Kaeni nayo tu mpeane na kina kifua kipana mkwe, sisi tunataka vifo vyetu vitokane na mapenzi ya Mungu tu mengine yote yenu
Wanapiga vingereza vingi sana
 
Back
Top Bottom