ONYO; Wafuatao wasithubutu kuilaumu au kuidharau Taifa Stars

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,301
Watu wengi wanailaumu na kuibeza Taifa Stars kwa kufanya vibaya ila wafuatao marufuku hata kufikiria kutamka neno baya dhidi ya Taifa Stars;

1. Kiongozi yeyote mwenye dhamana na michezo ambaye hutafuna pesa za maendeleo ya soka. Badala ya kukuza soka yeye anakuza tumbo lake.

2. Mtu yeyote anayetajwa kwenye ufisadi serikalini. Hayo mabilioni unayopiga zingejenga vituo vingapi vya michezo au kusomesha makocha? Kaa kimya kabisa.

3. Mzazi yeyote ambaye hajali kipaji cha mwanae. Mzazi kama huyu ni wa kucharazwa viboko. Mzazi asiye na busara na kuamua kuzima ndoto za mwanae kupitia viboko hapaswi kuilaumu Stars.

4. Mtu yeyote anayetuhumiwa au kukutwa na hatia ya unyanyasaji kwa watoto hasa vijana wadogo. Hao ni future ya soka la nchi hii kwahiyo unavyowafanyia ukatili madhara ni kwa taifa zima.

5. Kiongozi yeyote wa CCM mwenye dhamana ya kutunza viwanja vya mpira lakini hafanyi hivyo hapaswi kufungua mdomo wake. Viwanja vingi viko chini ya CCM.

6. Mtu yeyote aliyetelekeza mtoto/watoto wake na kumwachia majukumu yote mwanamke hatakiwi kuilaumu Stars.

7. Kiongozi yeyote wa klabu ya mpira anayebania vijana kutoka nje ya nchi kucheza mpira. Katika hili Yanga kwa muda mrefu wamekuwa na upuuzi wa kuwang'ang'ania wachezaji. Tujikumbushe Mrisho Ngasa.

8. Viongozi wote wanaotegemea hamasa badala ya maandalizi makali ya kisayansi kabla ya mashindano. Stars haiwezi shinda kwa hamasa za kina Mwijaku na Babalevo.

9. Watu wote wenye usimba na uyanga kwenye timu ya Taifa.

10. Wachezaji wote wa zamani ambao walichezea muda wao bila kufanya lolote wakati wakiwa timu ya taifa.

ONGEZEA WENGINE
 
Back
Top Bottom