Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,697
Ajira ni daraja la kuvukia shida kuelekea ktk kutimiza ndoto zako, hatima ya ajira si nzuri Kwa mwajiriwa maana humfanya abweteke na kuliwa mshahara, haumizi kichwa kutafuta pesa nje ya ajira zaidi ya kuwaza kuwa mfanyakazi bora, mwisho wa Siku kazi ikiisha au akistaafu na kurudi mtaani maisha yake yanakuwa magumu Sana maana hata biashara hajui kabisa, mara nyingi huishia kutapeliwa tu au kufeli ktk biashara baada ya kuvamia biashara asiyoijua hata kidogo.
Anafeli biashara na kuanza kutafuta kazi tena, hadi anazeekea kazini na kufa maskini wa kutupwa na ndo maana hutakaa uone ktk maisha yako mfanyakazi yoyote yule akiwa tajiri.
Ajira haina future hata kidogo, mfanyakazi ni toilet paper ktk nchi nyingi duniani, analipa kodi Kwa serikali kila mwezi na bado tu ananyanyaswa.
Sasa hivi serikali imefunga mafao yasichukuliwe na wafanyakazi hadi baada ya miaka 55 Umri ambao kuufikia ni Majaliwa, hayo yote ni manyanyaso Kwa mfanyakazi.
Epuka kuajiriwa jifunze Sana kujiajiri ndo utatengeneza hatima nzuri ya maisha yako.