Onyo kwa wanachuo wa UDSM

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Ni jana tu tulikuwa tunasherekea krisimass karibu wakristo wote duniani, ni sikukuu ya kumshukuru Mungu kwa kumleta mwanae wa pekee ambaye alikuja kutuokoa na dhambi zetu, kwa ujmla tunaoaswa kusherekea kwa furaha na amani, lakini si wote ambao hutumia sherehe hizo kwa kumheshimu Mungu, wengi wetu hujikuta tukifanya dhambi kama uzinzi, kunywa pombe kwa kupindukia, kudanganya (hasa katika mawasiliano ya simu n.k) n.kHapa UDSM kwa jana wanachuo wengi hawakuwepo maeneo ya chuo, karibu mchana wote mpaka mida ya usiku kama saa nane saa tisa n.k, nlijaribu kutoka nje kidogo ya campus nami nikaenjoy sikukuu, cha ajabu ndugu zanguni karibu maeneo mengi ukianzia survey , mwenge, sinza n.k wanachuo wengi walikuwa po huko. SI MBAYA KUWAPO HUKO KWANI SOTE TUNASHEREKEA.Ilipofika mida ya saa saba, ndipo ndugu zangu a.k.a watoto wa wakulima wakaanza kuingia chuo na bajaji pia bodaboda wamelewa vibaya huzani kama ni wasomi, na boom tulilopewa hili ni baya kuliko yote kwani kuna sikukuu ya xmass na mwaka mpya hivyo ukitumia vibaya boom hilo yamkini hata MTIHANI WA MWISHO HAPO JANUARY 2012 usifanye vizuri kwa kukosa pes, isitoshe sisi tukaao mbali tunahitaji nauli za kurudia huko na hali boom hilohilo ndo tunalitegemea.NDUGU zanguni, mi hatutakubaliana na mgomo wowote utajitokeza semister hii, eti kwasababu boom limeisha unless otherwise.
 
subiri watoke kwenye supu! Naogopa majibu yao, sifungui tena uzi huu.
 
Si hao wanachuo tu ndo wanajiachia hivyo wakati wa sikukuu, watanzania wengi tupo hivyo
 
Hivi tutafika kweli, kwa hali hii????
wakati mwingine tunailaum serikali yetu hali sisi wenyewe hatujishughulishi,

kwasisi wanachuo boom hili ukilitumia vizuri kwa kujinyima, unaweza kutengeneza maisha. WENGI WAO WANATHAMINI POMBE, STAREHE N.K.
KWELI TUTAFIKA???
 
Hawa watuhusumbua sana pindi waishiwapo.
just ushauri to them.
 
Hivi tutafika kweli, kwa hali hii????
kwani tunaendaga wapi?
wakati mwingine tunailaum serikali yetu hali sisi wenyewe hatujishughulishi,
kwa hiyo unataka serikali ikataze pombe nchini? dreams

kwasisi wanachuo boom hili ukilitumia vizuri kwa kujinyima, unaweza kutengeneza maisha.
kuwa mfano wao..jinyime tengeneza ilife saidia wakwenu...wewe hujui kuwa mchuma janga hula na wakwao?

WENGI WAO WANATHAMINI POMBE, STAREHE N.K.
KWELI TUTAFIKA???

wewe imeandikwa wapi kuwa pombe na starehe ndio chanzo cha kutokuwa na akili? na hao wanywa pombe wote unawapitaga darasani?
 
nchi yenyewe ishauzwa kwanini nisijiachie ata kidogo.. Unavyoongea inaonekana we ushamaliza boom lako ukataka 2kae wote chuo 2kupe cmpan.!!!
 
Ni jana tu tulikuwa tunasherekea krisimass karibu wakristo wote duniani, ni sikukuu ya kumshukuru Mungu kwa kumleta mwanae wa pekee ambaye alikuja kutuokoa na dhambi zetu, kwa ujmla tunaoaswa kusherekea kwa furaha na amani, lakini si wote ambao hutumia sherehe hizo kwa kumheshimu Mungu, wengi wetu hujikuta tukifanya dhambi kama uzinzi, kunywa pombe kwa kupindukia, kudanganya (hasa katika mawasiliano ya simu n.k) n.kHapa UDSM kwa jana wanachuo wengi hawakuwepo maeneo ya chuo, karibu mchana wote mpaka mida ya usiku kama saa nane saa tisa n.k, nlijaribu kutoka nje kidogo ya campus nami nikaenjoy sikukuu, cha ajabu ndugu zanguni karibu maeneo mengi ukianzia survey , mwenge, sinza n.k wanachuo wengi walikuwa po huko. SI MBAYA KUWAPO HUKO KWANI SOTE TUNASHEREKEA.Ilipofika mida ya saa saba, ndipo ndugu zangu a.k.a watoto wa wakulima wakaanza kuingia chuo na bajaji pia bodaboda wamelewa vibaya huzani kama ni wasomi, na boom tulilopewa hili ni baya kuliko yote kwani kuna sikukuu ya xmass na mwaka mpya hivyo ukitumia vibaya boom hilo yamkini hata MTIHANI WA MWISHO HAPO JANUARY 2012 usifanye vizuri kwa kukosa pes, isitoshe sisi tukaao mbali tunahitaji nauli za kurudia huko na hali boom hilohilo ndo tunalitegemea.NDUGU zanguni, mi hatutakubaliana na mgomo wowote utajitokeza semister hii, eti kwasababu boom limeisha unless otherwise.

nahisi tuna undugu.
Sio bure, una akili sana wewe kijana...
 
Si hao wanachuo tu ndo wanajiachia hivyo wakati wa sikukuu, watanzania wengi tupo hivyo

afadhali hao wengine hutumia kilicho chao, kipato halali kutokana na kazi ya mikono yao.
Hawa wanatumia kodi za Watanganyika, tena wale wa kipato kidogo, walevi wa Kibuku na wavuta sigara za TCC(maana African Barrick Gold, Serena et. al wapo mu-tax holiday).
Binafsi roho inaniuma kumwona msomi analewa sikukuu halafu mwisho wa semista anaanza kukomnika na kuopti core course ya RB600 au SP300 kwa wale wa Mabibo...
Where is the hell of your usomi wakati huwezi kubalance pesa ya miezi mbili?
Nijinyamazie.
Nisije kupata ban bure...
 
Hlo neno, udom uongozi uliliona hilo ndio maana boom la pili wamepanga kuwapa baada ya mwaka mpya. Bg up kikula
 
Back
Top Bottom