Bi. Senti 50
JF-Expert Member
- Apr 17, 2007
- 287
- 12
kuna huyu memba ambaye anajifanya anajua kila kitu. Naomba kutuma ujumbe wa wazi kabisa. Tafadhali acha! Hili ni onyo la mwisho. Kelele zako za mambo ya siasa zimekubalika na ni kweli zimekutengenezea jina, lakini hili la sasa ni jambo ambalo ni kinyume na uungwana na lina lango moja nalo ni kuwapaka viongozi matope. Nilikuwa naunga mkono mambo ya Mbowe na Slaa kuwekwa hadharani, lakini naona mambo yote ni ya upuuzi. Nawaomba JF tuungane na kuyakataa haya kwani ingawa yana faida kidogo lakini madhara yake ni makubwa zaidi. Naomba kutoa wazo kuwa mada zote zinazohusiana na mambo ya binafsi kama ya kina Slaa, Mbowe, na Mhe. Kikwete au Waziri wetu Mpendwa Lowassa, yapelekwe kwenye udaku au kwingine. Wengine tumejaribu kuwakaribishwa wakubwa wetu ofisini, lakini leo wengi wametoka wakitikisa vichwa vyao. Nawasihi.
Asante.
Asante.