Onyesha upendo, kosoa, pongeza

j'cob mushi

Member
Feb 26, 2013
21
13
Usisubiri mtu afe ndio umpost mtandaoni na kuandika Rest In Peace my lovely Friend.

Wakati yupo hai ndio wakati sahihi wa kuonyesha ni your lovely friend kwake na kwa wengine.

Usikimbilie kumlaumu, kukosoa, kutukana mtu kwa kosa lolote alilolifanya wakati hujawahi kumsifia hata mara moja alipofanya Vizuri.

Tena inawezekana kakosea Kwasababu hajaona mchango wowote kwako wakati anafanya mazuri☹

Sijasema umsifie kila mtu La Hasha! Sijasema umpost kila mtu unaekutana nae mtandaoni. La Hasha! Ninachokimaanisha ni hivi kama Utaweza kuja kumpost siku akifa basi Jitahidi basi uanze sasa hivi akiwa hai.
Kama Utaweza kuja kumkosoa anapokosea Jitahidi basi umpongeze anapofanya Vizuri.

Nakutakia Mwaka Wenye Baraka za Mungu 2017.
Jacob Mushi.
 
Ni sawa lakini wengine hawapongezeki, Hawashauriki, Muda wote unaweza kumpamba kwa sifa lakini akaishia kukuita shetani still bado atasema umuombee sikupindi ila wakati mwingine unaangaia na rafiki wa kutimiza naye hayo usemayo..yaani kuna marafiki wengine wana visa Faru John kasingiziwa.
 
Pamoja na visa nk,

unatakiwa usiache kumwonyesha upendo

mwisho wa siku atakupenda tu km si kukubali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom