Sikonge:
Kumbe tuko kuipa mkono CHADEMA? Nilikuwa sijui. Na hata kama ni Chadema, basi huyo Mbowe basi aje hapa na kama kweli atakubali kupokea watu wengi kutoka JF, basi lazima vitu kadhaa viingizwe humo ndani. Kama amekuwa anaibeba Chadema kwa nguvu basi lazima aridhike kuwa sasa atakuwa na upinzani.
Kama nilivyosema mwanzo, itabidi hata wale ambao hawapo Dar kama mimi hapa, tuweze shiriki mkutano ONLINE. Tutachangia ila kwa makubalioano tuwe na SAY yetu. Kwa mtindo huo basi, Chadema kiwe chama cha kwanza kuanza kutumia INTERNET katika maswala yake mengi na hii inwe NYONGEZA katika maneno ya Nyerere kuwa "Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, Watu, Ardhi, Siasa safi, Uongozi bora na sisi tuseme TECHNOLOGY".
Chadema, njooni hapa, nendeni Tanzanet, nendeni kwa Michuzi nk ili muone jinsi Mtandao unavyovuta watu. Someni kutoka kwao na hapo anzisheni mtandao wenu. Ikibidi msaada wa kufungua kitu kama hiki basi nafikiri wapo watu wengi sana watakaokuwa tayari kuwachangua kwa mawazo, ufundi, fedha na vifaa kama mtaonyesha moyo wa kupokea hivyo vitu kutoka kwao na kuvitumia kwa faida ya Watanzania.
Ila cha muhimu ni "nini kitatokea kwa viongozi wataokiuka masharti na kuiba au kutumia vibaya hivyo vitu?" Hapa ndipo patakapotofautisha chama hiki na CCM.
Allien,
Najua Ndoto yako toka wiki ianze ni kuona wewe Muungano wa Vyama Vya siasa na hasa Vya Upinzani.
Na lengo lako has ni kuona kuna hatu kubwa ya maendeleo infikiwa katika Nchi hii,Unataka wananchi wapewe Maisha Bora bila ya kuyasotea.
Muungano wa Upinzani ni Muhimu sana na ulikuwapo sana miaka ya Nyuma ila siku zote ulikuwa ukivunjiaka baada ya chama kimoja kujiona kipo juu ya vyama vingine.
Mwaka 2000 Mrema alijiona yeye ndiyo baba wa vyama vyote hivyo TLP ilikuwa inastahili kupewa madaraka katika nchii hii na vyama vingine vya upinzani viunge mkono tu
2005 CHADEMA ilionekana ina Nguvu na kwa kutumia Viiongozi wa juu ambao walionehsa kuwa wao wanaweza kuliko Vyama vingine.
Ili ilisababisha vyama kama NCCR na CUF kuamua kujitoa katika Muungano ambao tayari ulishaasisiwa.
Tanzania inawezekana ila tatizo ni jambo Moja.Uroho wa Madaraka,Ubinafsi ambao umo miongoni mwa viongozi wa vyama vya Upinzani.
To make it clear ni kuwa Upinzani wa kwelli utaanza pale CCM itakapovunjika na kitokee Chama kingine..Inawezekana??
Allien,
Muungano wa Upinzani ni Muhimu sana na ulikuwapo sana miaka ya Nyuma ila siku zote ulikuwa ukivunjiaka baada ya chama kimoja kujiona kipo juu ya vyama vingine.
Tanzania inawezekana ila tatizo ni jambo Moja.Uroho wa Madaraka,Ubinafsi ambao umo miongoni mwa viongozi wa vyama vya Upinzani.
To make it clear ni kuwa Upinzani wa kwelli utaanza pale CCM itakapovunjika na kitokee Chama kingine..Inawezekana??
Allien,
Najua Ndoto yako toka wiki ianze ni kuona wewe Muungano wa Vyama Vya siasa na hasa Vya Upinzani.
Na lengo lako has ni kuona kuna hatu kubwa ya maendeleo infikiwa katika Nchi hii,Unataka wananchi wapewe Maisha Bora bila ya kuyasotea.
Muungano wa Upinzani ni Muhimu sana na ulikuwapo sana miaka ya Nyuma ila siku zote ulikuwa ukivunjiaka baada ya chama kimoja kujiona kipo juu ya vyama vingine.
Mwaka 2000 Mrema alijiona yeye ndiyo baba wa vyama vyote hivyo TLP ilikuwa inastahili kupewa madaraka katika nchii hii na vyama vingine vya upinzani viunge mkono tu
2005 CHADEMA ilionekana ina Nguvu na kwa kutumia Viiongozi wa juu ambao walionehsa kuwa wao wanaweza kuliko Vyama vingine.
Ili ilisababisha vyama kama NCCR na CUF kuamua kujitoa katika Muungano ambao tayari ulishaasisiwa.
Tanzania inawezekana ila tatizo ni jambo Moja.Uroho wa Madaraka,Ubinafsi ambao umo miongoni mwa viongozi wa vyama vya Upinzani.
To make it clear ni kuwa Upinzani wa kwelli utaanza pale CCM itakapovunjika na kitokee Chama kingine..Inawezekana??
Sidhani kama "maswali" mnayo..!!
Huu ni upotoshaji uliovuka mipaka! Hakukuwa na ushirikiano mwaka 2005 kisha CHADEMA ikajitoa! Kulikuwa na majadiliano ila waliokuwa wanajiona chama kikubwa walikuwa ni CUF amabao walikuwa wanataka waachiwe kila kitu!
Lazima ikumbukwe kuwa mwaka 95 CHADEMA haikusimamisha mgombea wa Uraisi ili muunga mkono Mrema alie kuwa mgombea wa NCCR. Mwaka 2000 CHADEMA ilimuunga mkono Lipumba.
Kwa hiyo mpaka sasa chama ambacho kimedhihirisha dhahiri kuwa kina nia njema na kuwa tayari kuunga mkono wenzake ni CHADEMA Pekee!CUF, TLP NA NCCR ni lini wamemuunga mkono mgombea wa chama kingine katika nafasi ya uraisi? Hata hivyo kuunga mkono huku hakuleta manufaa kwa CHADEMA kutokana na ubinafsi wa vyama vilivyoungwa mkono.
Mwaka 2005 CHADEMA ilisimamisha mgombea wake wa uraisi, ili kuwa kama inajitambulisha kitaifa kuwa imeingia rasmi katika siasa za kitaifa na mapambano ya moja kwa moja! Jambo ambalo limeta hamasa na mvuto wa aine yake na kukisogeza CHADEMA kuelekea kuwa chama kikuu cha Upinzani nchini kabla ya kuchukua madaraka kamili mwaka 2015, ila mahesabu ya kikosewa wanaweza kuingia 2010 kabla ya mda wao! Mda utasema.
Tuitendee haki CHADEMA. Ndio pekee wamewahi kumuunga mkono wenzao, NCCR ilikuwa na nguvu mwaka 95 CHADEMA walikubali kuiunga mkono na ndivyo ilivyokuwa mwaka 2000 kwa CUF, Leo CHADEMA ina nguvu zaidi, CUF, NCCR na TLP waiunge mkono! Ni kivipi sasa tunasema CHADEMA ndio wana uroho wa madaraka?
Nimewasoma, mengi ni maoni mazuri yanayostahili kufanyiwa kazi na mengi tayari yameshafanyiwa kazi.
Hapa si mahali pa kulaumiana. Kinachoongelewa hapa ni kuwa, je CHADEMA wako tayari kujiunda upya na kwenda katika misingi inayotarajiwa na Wananchi wengi ili hatimaye ichukue Nchi?
Rev. Kishoka
Samahani kwa kukuelewa vivyo sivyo.
Hayo mengine nimekupata, tuendelee kuyajadili kule kwenye "CHADEMA must reform"
Mtanzania wa kawaida anachojua tu ni kwamba waCHADEMA wanapinga ufisadi na kutetea rasilimali za Taifa; wanachojua ni Mbowe wa Helikopta anayekemea rushwa ya CCM kwa kuwaapiza, Zitto Kabwe aliyefukuzwa Bungeni kwa sababu ya Dili la Karamagi la Buzwagi, Dr Slaa ambaye ameshika pabaya Balali kwenye BOT na Tundu Lissu ambaye ameshirikiana na Slaa kutaja orodha ya mafisadi. Hizo ndio stori za vijiweni! Ukiwauliza kuhusu falsafa na itikadi hawayajui mambo hayo, changamoto ni CHADEMA kuweza kueleza zaidi sera zake mpaka watanzania wajue kwamba ni chama cha itikadi ya mrengo wa kati chini ya falsafa ya "Nguvu ya Umma", taratibu tutafika. Hatua ya kwanza ambayo tumeanza nayo ni kutoa mafunzo kwa viongozi wetu ngazi za chini, taratibu tutafika. Safari ya maili mia huanzia na moja!
Elimu ya bure tunayoipata hapa inapenya katika akili zetu na tunaitoa tunapokaa katika vikao vya chama ama vya ushirikiano wa vyama ama tunapoandaa rasimu ya nyaraka mbalimbali za kutoa mwelekeo. Tunaitumia pia tunavyopanda jukwaani kuhutubia wananchi ikiwemo huko vijijini. Kwa hiyo, chukulia kila unachoandika hapa kinasadia katika kujenga demokrasia na maendeleo nchini. Sisi ni watumishi na wawakilishi, vyama vya siasa ni taasisi za umma!
CHADEMA ina kurugenzi mbalimbali ambazo zinawataalamu wa fani mbalimbali, lakini hawa pekee hawawezi kutosha kusambaa maeneo mbalimbali nchini. Tunahitaji wataalamu mbalimbali, hata kama wanakazi zao huo mawilayani ama kwenye taasisi mbalimbali watenge japo siku moja kwa mwezi huko walipo kujitolea utaalamu wao kwa ajili ya kusaidia mikakati ya kuleta demokrasia na maendeleo nchini. Vinginevyo, usomi wao utakuwa ni wa kibinafsi kama yule aliyechangiwa chakula chote kijijini avuke jangwa akalete chakula kwa waliobaki wenye njaa, huyo asiporudi ni msaliti! Kadhalika, wasomi wetu wakishindwa kuchukua japo muda mchache kukumbuka wajibu wao kwa wasiosoma na taifa kwa ujumla, nao ni wasaliti. Kama tunaweza kukaa kwenye pub masaa kadhaa tukipiga soga, tujue kuwa tunaweza kabisa kuwa na muda kwa ajili ya hii noble course tukitaka.
Wapinzani wanafanya nini kuchukua tuzo za siasa na ujamaa na kujitegemea? Tunafanya. Mimi na Profesa Baregu tulikuwa kwenye kamati ya kufanya mapitio ya itikadi ya CHADEMA kutenganisha bayana itikadi na falsafa ya CHADEMA katika muktadha wa malengo, sera za CHADEMA na mwelekeo wa Taifa kwa ujumla. Hatimaye katiba ikafanyiwa mabadiliko 2006- nimeweka kwenye "CHADEMA must reform" nakala ya Katiba ya CHADEMA- ukisoma 'itikadi ya CHADEMA ya mrengo wa kati" na falsafa ya CHADEMA ya "Nguvu ya umma" utaona kwamba imechota baadhi ya tunu za Ujamaa na kujitegemea ikachanganya na baadhi ya manufaa ya ubepari. Mchanyato uliopatikana utawezesha CHADEMA ikichukua dola- kuendesha nchi bila dola kuhodhi nyanja zote, lakini kuhakikisha pia uchumi unamilikiwa na wananchi waliowengi na si uchumi unaomilikiwa na kunufaisha kwa kiasi kikubwa tabaka la watu wachache ama wawekezaji kutoka nje chini ya ubepari wa kimataifa wa ukoloni mamboleo.
JJ
Kwanza tunashukuru kwa kuitikia wito wa kutembelea thread hii. Ingawa naona umejibu kwa haraka haraka na kuacha maswali ya msingi yaliyoulizwa na wadau katika post zao.
Kwanza, CHADEMA wako tayari kupokea Wanamapinduzi kutoka JF na kwingineko ambao wataleta changamoto ya kweli?
Je, mko tayari kufanya marekebisho ya kiuongozi na mfumo wa uongozi kukidhi Demokrasia ya kweli kivitendo katika uendeshaji wa chama?
Je, kwa wale watu makini na ambao ni rasilimali ya Taifa wakija CHADEMA je, viongozi wa sasa wako tayari kutoa nafasi za uongozi kwa wadau hawa?
Maswali haya na mengine katika post yanatakiwa yajibiwe. Tutayapima majibu yako kwa hiyo ni vema majibu yakiwa detailed with facts.
Mkuu Allien,
FYI
Hebu jaribu kubofya hapo chini, kuna nasaha, na majibu mengi tu kuhusu CHADEMA mafikirio yangu yatakusaidia...
'Focus 2010'-'The Road towards 2010 Elections'-'Chadema Must Reform'
Kama sijakosea hizo hapo juu ziliunganishwa.
Hili hapa chini lilikuwa swali mojawapo kwa JJ kutoka kwa Rev. Kishoka...
Na kuhusu hapo juu, ninamnukuu JJ akimjibu Rev. Kishoka...
Matarajio yangu ni kuwa hili litakufungulia wigo.
Aksante
He, hapa kweli naona unatoka Sayari ya MBALI.
Haya maswali yako unategemea watu wakujibu ndio au wakujibu hapana?
Ninachoamini ni kuwa vyama vyote vya siasa vinahitaji wanachama waaminifu na wenye nia thabiti kufikia malengo chama kiliojiwekea.
Naamini kuna taratibu na sheria za kuendesha chama ikiwa ni pamoja na kupata viongozi wake. Naamini nawe unafahamu kuwa viongozi wote waliopo ndani ya chadema sio walionza, ila hawa ni wa awamu ya 3 kama sikosei. Swali, ni je walipatikana kwa mtindo unaooujadili wewe au ni kwa kufuata katika ya chama?
Unataka, leo ukijiunga upewe uenyekiti, ukatibu, ukurugenzi hapo hapo? ipo wapi nafasi ya kupimwa na kuujua uzalendo wako? Je watajuaje kuwa sio miongoni mwa waliotumwa kukiangamiza chama chao?
Jiweke kwenye nafasi yao halafu ujaribu kujibu maswali yako.
#NB. HUU NI MTIZAMO WANGU NA WALA HAUHUSIANI NA CHADEMA, NA WALA MIE SIO MWANACHAMA.