Nono
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,536
- 643
Mkuu Nono;
Nadhani kiini cha hoja ya msingi bado hujakielewa . . .
Shida si kwa Watu Makini na uwezo mkubwa kujiunga CHADEMA na kupewa Uongozi. Shida ni viongozi wa namna gani wanatakiwa na je ni Waadilifu kiasi cha kuvuta Umma wa Tanzania kuwatambua kuwa wako serious?
Concept ya Watu Makini kuachiwa uongozi si suala jipya na limefanya kazi sana katika Historia ya Mabadiliko ingawa si wote wamefanikiwa kuleta mabadiliko ya kweli. Nyerere alifanya hivyo, CCM wao wana utaratibu wa Kung'atuka na hata kuchukua watu wanaohama Upinzani na kuwapa madaraka, Oliver Tambo alimwachia Nelson Mandela, Mabere Marando alimwachia Mzee wa Kilalacha n.k.
This issue if you look into the positive side, you will understand what I mean. Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambao ndiyo wenye nafasi kubwa ya kuleta Tranformation wamekuwa questioned sana juu ya uadilifu wao, matumizi mabaya ya pesa, upendeleo, na hata kwa baadhi ya maamuzi . . .
For sure these are not about constitution or about election procedures, it is about leadership. Wakati CCM wanaendelea kukumbatia Rushwa na hata Ufisadi, Makundi nk katika Chaguzi zao i.e UVCCM, UWT nk. CHADEMA inatakiwa ijisafishe . . .
Yote hayo kwa Ujumla wake ndiyo yanatakiwa yafanyiwe kazi. Na tunataka commitment yao . . . .
Mkuu Allien,
Mimi bado naendelea kuamini taratibu na sheria ndio kitu pekee ambacho kinaweza kuleta mabadiliko endelevu.
Ukitoa mfano wa ccm kuwa wanang'atuka sio kweli kwani aliyengatuka ni Nyerere pia baada ya kuona kuwa muda umekwenda na aliyokuwa anasimamia na kuyaamini yalikuwa hayaendi kwa dunia ya wakati ule (tunamshukuru sana kwa hilo). Kuwa wapinzani wanaojiunga na ccm wanapewa madaraka ni njia ya kuudumaza upinzani pamoja na kuwadumaza hao waliojiunga na ccm kwani vinafasi vyenyewe wanavyopewa ni vya kuwafunga midomo na baada ya muda hawasikiki tena.
Suala la msingi hapa nadhani ni je, vyama hivi vinafuata taratibu na demokrasia ya kweli ndani yake. Hili kama lipo, sioni haja ya kumpisha mtu, kwani cheo ni dhamana, utatumika leo na kesho mwenzio atapokea kijiti. Pale inapobidi nadhani chama husika kinaweza kuona umuhimu na baada ya kujihoji, kuridhika na kuondoa hofu na mashaka basi wanaweza kumpisha mtu katika nafasi ya juu ya uongozi hasa pale anapokuwa "Allien" (yaani ambaye alikuwa sio mwanachama) au wakiwa kama kina Mandela, amabo ni viongozi walikuwa walioachiwa huru, ila usisahau kufungwa kwao ndio kupandisha siasa kwenyewe!
Sheria na demokrasia ndani ya chama husika ikiwemo, basi akitokea kiongozi akavurunda, taratibu zilizopo zinatumika kumuwajibisha ikiwa ni pamoja na kusitisha nafasi yake ya uongozi pale inapobidi. Nadhani huu ndio msingi!
Kama demokrasia ya kweli ipo, basi wewe ukiwa mwanachama na wanachama wakikuona una sifa zinazostahili kwa nafasi yoyote, basi mazingira yatakuwa sawa kumpata kiongozi atakayekiongoza chama. Mimi nadhani tukisimama katika hili na vyama vikifanya mambo yake kama taratibu zilivyo na zinavyotakikana ziwe, huwezi kuwa na M/Kiti au Katibu mkuu kwa miaka 10-15 na idadi ya madiwani, wabunge na wanachama ni wawili wawili, labda kama hivyo vyama ni taasisi za watu binafsi! Unatakiwa upimwe kwa talanta zako.
Ahsante