Allien
JF-Expert Member
- Jul 6, 2008
- 5,546
- 1,861
- Thread starter
- #41
Allien, hoja zako ni nzuri sana na CHADEMA wanatakiwa wazifanyie kazi. Kwa maoni yangu si vizuri mtu kukimbilia kwenye chama kutafuta uongozi. Inakuwa vizuri kama unajiunga na chama kutoa mchango wako katika jambo ambalo chama hicho kinalisimiamia na endapo wewe unaliamini (towards attaining a common goal). Lakini mtu anayefika mahali na siku hiyo anataka ukubwa ni hatari. Ni bahati mbaya kwamba watu wengi tunapenda sana kutumikiwa kuliko kutumikia. Hii ni hali ya hatari sana na nadhani ndio chanzo cha wakulu wetu kudai kwa nguvu kuitwa waheshimiwa!! Ni upuuzi mtupu!
Ila kama mtu anataka kuongoza basi awashawishi wanachama kwanza kwa kuwatumikia ili wampime na si kuanza kunadi rekodi zake za huko alikotoka katika mtindo wa hadithi na ngonjera za paukwa pakawa.
Pia nakuunga mkono kwamba CHADEMA watafute jambo ambalo litawatofautisha na vyama vingine hapa TZ ikiwemo CCM. Na jambo rahisi la kutumia ila gumu kulitekeleza kwa hali TZ ya sasa ni UADILIFU. Kama wakiweza hilo na kuweka mikakati mizuri ya kuonyesha kuwa wana kitu kipya cha kuwapa Watz, sioni sababu kwa nini wananchi wasiwaami na kuwaunga mkono, na hatimaye kuwapa jukumu la kuongoza nchi yetu. Vinginevyo wataishia kutamani tu kuwakomboa WaTz lakini hawataweza kwa kuwa hawana mbinu za kufanya hivyo.
Mkuu, sasa tuko pamoja 100%! Umeongea kama Mwanamapinduzi na si kama Mwanasiasa.
Big up!