Makindi N
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 1,066
- 173
mwanakijjii makala yako inawauliza wanaccm na rais wao mie ningependa niwaulize makamanda je katika kikao cha ikulu waligusia kusikitishwa kwao na ongezeko hilo au waliuchuna? Mara nyingi nemekuwa nikisoma makala zako naona zinaegemea upande mmoja bila kuangania upande wapi nao wanamsukumo gani katika tatizo husika. Huwa nafurahi kusoma makala za maggid mjengwa jamaa huwa anasimamia ukweli yaani yupo balanced sana.
Kwa sasa Tanzania baada ya miaka 50 ya uhuru tumekuwa na uhaba wa waandishi wa namna ya Maggid Mjengwa wengi wa waandishi ni "maslahi" wanaotetea makundi yanayowashibisha au yenye manufaa nao. Waandishi lazima wajue umuhimu wao wa kupasha habari jamii/hadhira na adhari zake pamoja na faidi katika maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Maggid Mjengwa hajawahi kuwa "balanced".... Maggid ni mwanaCCM, uchaguzi wa Rais na Ubunge uliopita alitumia blog yake na aliweka wazi kabisa kwamba yeye ni mwanaCCM na haoni ni nani wa kushindanishwa na JK..... Sema ni muwazi.... sijui km UWAZI na being balanced are synonymous.
Kwenye posho Watanzania ni km tumerogwa. Najiulizaga ni kwanini ni Tanzania tu mtu anaibiwa na serikali, mtu binafsi, kampuni etc lakini tuko kimya tu na tunapiga soga jioni iwe majumbani, vijiweni, bar etc kuhusiana na hilo, ila HATUTHUBUTU kusema basi...... TUtaandika humu, tutasema vijeweni jioni, wengine watalia etc ndo tumemaliza.......... Kwanini hatuna uthubutu wa kusema basi POSHO, BASI MEREMETA, BASI RICHMOND, nilikuwa Mtwara two weeks ago kunawazungu wanajidai wanafanya exploration ya oil, nilishuhudia kwa macho yangu kila lisaa meli nyingi sana zinaondoka zimejaza crude oil.... Wale wazungu wanaishi Dar, wanakula lunch Dar na kulala Dar...... nilishuhudia flight ikiwachukua saa 7 na kuwarudisha saa 9 na jioni saa kumi mbili...... Wadada zetu, watoto wetu wanaosoma SAUT - Mtwara, UTUMISHI ndio viburudisho vyao - wakitoka mle melini wanahongwa 200,000/= kwa udhalilishaji waliofanyiwa - TUTHUBUTU na tuseme BASI........ Its a high time for that..... "We must meet the needs of the present generation without compromising the ability of future generations to meet their own need" WCED: 1987:8)... to realize that TUANZE BASI KUSEMA BASI..............