Ongezeko la Posho za Wabunge ni Wizi na Dhulma dhidi ya Wafanyakazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ongezeko la Posho za Wabunge ni Wizi na Dhulma dhidi ya Wafanyakazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 29, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Uchumi wa Tanzania uko mitatani. Hili ni kweli. Kuporomoka kwa thamani ya shilingi kumefanya bei ya vitu mbalimbali kuwa ya juu kulinganisha na kipato cha watu. Ili watu wamudu mambo waliyokuwa wanayamudu mwaka mmoja tu uliopita wanahitaji ongezeko la maana ya kipato. Bahati mbaya hawawezi kujiongezea kiwango na hivyo watu wanalazimika kubadilisha yao na kubana matumizi. Mamilioni ya Watanzania wanajikuta wanalazimika kuishi hivyo. Wale wenye nafasi ya kufanya ufisadi wanaweza kutumia nafasi hiyo kufanya ufisadi zaidi ili kujiongezea kipato kumudu maisha. Lakini hawana uwezo wa kuamua kujiongezea posho au mishahara ili wamudu maisha.

  Hili si kweli kwa wabunge wetu. Habari kwamba wabunge wamejiongezea posho kadhaa kwa karibu asilimia zaidi ya 150 ni habari za kuudhi, kukera na kama ni za kweli kabisa ni za kumfanya kila Mtanzania kupinga kwa nguvu zote dhulma hii ya wazi kwa wananchi wetu maskini wanaohenyeka kila siku kujitafutia ridhi zao. Ndugu zangu, wabunge ndio watu pekee ambao wanaweza kujipangia mishahara na posho zao bila kusimamiwa na chombo kingine chochote. Hata Rais hajipangii mshahara au posho!

  Ukweli ni kuwa hakuna sababu yoyote ya kiakili ya kuhalalisha posho zilizoongozwa kwa wabunge. Katika nchi ambayo watu wanadaiwa kuna hali mbaya ya kiuchumi na hasa kwenye mporomoko wa shilingi Wabunge kuongezewa posho ni unyonyaji wa hali ya juu na dhulma kwani fedha zote hizo zinatoka kwa wafanyakazi wanaohenyeka kila siku kujipatia maisha bora. Ni wizi na dhulma kwa utu wa Watanzania maskini ambao fedha kidogo waliyonayo wanaipanga wakijua kuwa uchumi uko katika hali mbaya. Kuhalalisha wizi huu wa mchana kweupe ni kuwa washirika wa dhulma hiyo.

  Tunapozungumzia "matumizi mabaya ya madaraka" mara nyingi watu wanafikiria mtu mmoja akitumia madaraka yake vibaya. Ukweli ni kuwa kuna wakati taasisi au vyombo vinaweza kutumia madaraka vibaya. Polisi wanapoua pasipo uhalali ni matumizi mabaya ya madaraka na wabunge wanapotumia haki zao za Bunge kujinufaisha wao wenyewe ni matumizi mabaya ya madaraka.

  Kisingizo pekee ambacho kinatolewa kuhalalisha wizi huu wa mchana ni kuwa wabunge wanahitaji fedha ili kusaidia wapiga kura wao. Wengine wanajenga hoja kuwa wabunge hutumia posho hizo kutoa misaada mbalimbali. Ndugu zangu, mtindo huu ni mitndo ambao umewafanya wabunge wasiwajibike Bungeni kwa sababu wanajua wanaweza kutumia fedha zao hapa na pale kutuliza wapiga kura wao. Lakini kama tukipiga marufuku wabunge kutoa fedha yao Bungeni kwa namna yoyote ile wabunge wagenfanya nini? Ni wazi wangejitahidi kuihimiza serikali kufanya mambo mbalimbali, kusimamia mapato, kufuatilia nidhamu n.k

  Bahati mbaya mfumo ulioruhusiwa chini ya CCM unaruhusu wabunge kutoa misaada na fedha zao wenyewe. Huu ni mfumo mbaya kwani kwa kisingio cha kutoa misaada wao huchota kwenye hazina ya taifa. Wanatumia hiki kama kisingizo cha kwanini wanastahili zaidi. Lakini wanashindwa kujiuliza ni mfanyakazi gani wa Tanzania ambaye haitaji kutoa misaada ya hapa na pale kwa watu wa familia yake? Karibu kila mfanyakazi wa Tanzania ana majukumu ya kusaidia hapa na pale kwenye familia yake ndugu zangu na hata jamaa zake kijijinbi. Sasa je huyu anaweza vipi wakati fedha anazopata ni za mshahara?

  Hivi ni Mtanzania gani ambaye akiulizwa kama anahitaji nyongeza ya posho au mshahara ili imsaidie kwenye matatizo yake anaweza kusema haitaji. Sasa kwanini Wabunge wanaamini kuwa wao ndio wanahitaji sana kuwasaidia watu wa majimbo na vijijini kwao na hivyo kujihalalishia posho. Kwanini wanafikiria wao ambao wanapewa posho za kufuru wanastahili zaidi katika kipindi hiki cha hali mbaya ya uchumi ambapo vijana wamekosa ajira, gharama ya kufanya biashara iko juu na bei ya bidhaa na huduma mbalimbali inazidi kupanda juu kila siku?

  Tuwe wa kweli. Bunge kama limehalalisha ongezeko hili la posho limekuwa mshiriki wa wizi wa mali za watu. NI sawasawa na kumkuta mkulima aliyelima na kutoka jasho ambaye baada ya kuvunja anaambbiwa hawezi kula alichovuna na badala yake arudi kulima tena. NI sawasawa na kuchomeka mrija wa unyonyaji kwenye mgongo wa mkulima na mfanyakazi wa Tanzania, mgongo ambao tayrai umekuwa na mirija mingine (bei ya umeme, mafuta, mafuta ya taa, nauli, nyumba, elimu n.k!).

  Tunachoweza kuomba tuambiwe ni kuwa hali ya uchumi imekuwa nzuri kuwweza kufanya jambo hili. Na tuna sababu kuwa hali ya uchumi imebadilika na kuwa nzuri. Vinginevyo, tutaelezea vipi ongezeko la posho za wabunge wakati wa hali mbaya ya uchumi. RAis Kikwete na chama chake wanaweza vipi kuhalalisha hili? Binafsi ningependa kusikia viongozi wa CCM wanaweza kuhalalisha vipi ongezeko hili. Hivi kweli kuna mtu anaamini kuongeza posho ndio kutawafanya wabunge kuwa wawajibikaji? Tunajuaje kama kiwango kilichoongezwa kinatosha kuwashawishi kuwajibika? Itakuwaje mwezi mmoja baadaye wakitaka kuongezewa zaidi ili wawajibike zaidi? Je hatuoni kuwa ni kama tumewadekeza - kwamba wasipoongezewa posho basi hawawajibiki. Je, yawezekana wabunge wa CCM wamelichukua taifa nyara na sasa taifa zima liko mbele ya huruma yao - posho au hatuwajibiki!

  Kwa kweli hii ni dhulma dhidi ya wafanyakazi wa Tanzania ambao kwa kweli hawana mtetezi kwani vyama vya wafanyakazi navyo vimelala kwenye kitanda cha ufisadi pamoja na watawala wetu walioshindwa. Binafsi sitaki kusikia mbunge ati analalamikia posho; hivi wabunge wakilalamikia posho wakati wao ndio wanatunga sheria na watu walioko nje wafanye nini? Kama kuna mbunge anaona posho hazistahiki walete miswada Bungeni kutengeneza sheria ya kusimamia posho na kura za roll call zipigwe ili tujue ni mbunge gani anapinga sheria hiyo iili wananchi wajue nani ni adui yao. Haitoshi kwa wabunge na wenyewe kulalamikia posho kwa sababu ndio watu pekee wanaoweza kubadilisha sheria ; haiitaji serikali kufanya hivyo. Sasa kwanini hakuna mswada wa mabadiliko ya sheria ya fedha au hata sheria ya kusimamia posho?

  MMM
   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wapiganaji wetu mbona hatuwasikii?
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  mwanakijjii makala yako inawauliza wanaccm na rais wao mie ningependa niwaulize makamanda je katika kikao cha ikulu waligusia kusikitishwa kwao na ongezeko hilo au waliuchuna? Mara nyingi nemekuwa nikisoma makala zako naona zinaegemea upande mmoja bila kuangania upande wapi nao wanamsukumo gani katika tatizo husika. Huwa nafurahi kusoma makala za maggid mjengwa jamaa huwa anasimamia ukweli yaani yupo balanced sana.

  Kwa sasa Tanzania baada ya miaka 50 ya uhuru tumekuwa na uhaba wa waandishi wa namna ya Maggid Mjengwa wengi wa waandishi ni "maslahi" wanaotetea makundi yanayowashibisha au yenye manufaa nao. Waandishi lazima wajue umuhimu wao wa kupasha habari jamii/hadhira na adhari zake pamoja na faidi katika maendeleo ya jamii kwa ujumla.
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Nami niana kiu ya kutaka kusikia kutoka kwao!
   
 5. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  sie wengine tunapigania income zetu zipande(salary) which means PAYE nayo inakuwa juu watu wengine wasio na huruma wanatafuta namna ya kuzitafuna hizi hela jamani kuweni na huruma hata kidogo sasa mtakata tumuamini nani hapa.. mbona mnaziweka dhamira zenu za ulafi waziwazi agrrrrrrrh ... KIMA CHA CHINI WAMESHINDWA KUKITETEA WAMEWACHIA TUCTA hivi hawa ndio wawakilishi wetu kweli ........WATATUKAMUA SANA MORE TO COME........
   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  MJ, mimi nitasema nini? maneno yangu hayata fika mbali kama ya mwandishi kama Mwanakijiji. Nitakachosema kitaishia hapahapa jf na wakati mwingine kinaweza kuondolewa na mods (nadhani unaelewa what I mean)

  Inasikitisha kuona hawa watu walisoma bure leo wanawabana vijana wanaosoma elimu ya juu kwa kuwapa posho njiwa na wengine kukosa mikopo hata kama wamefanya vizuri (wenye vipaji) ilhali wao wakijiongezea vipato kupitia posho.

  Habari hii ya kuongezeana posho na ile ya udhamini wa kampuni ya bia dhidi ya wanafunzi wa nne waliofanya vizuri na wakakosa mkopo kutoka bodi ya mikopo imenifedhehesha sana.
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Yaani hii serikali ni kama ya kishetani, hebu fikiria Mahita alishawahi kusema posho moja ya mbunge ni sawa na mshahara wa askari wangu polisi kwa mwezi mzima!! Kauli hiyo ilimuingia kwenye majibizani makali sana na wabunge lakini ndiyo ulikuwa ukweli.

  Leo hii nina imani polisi anayeanza take home haizidi 200,000.00 licha ya kutumiwa kukandamiza demokrasia lakini mbunge kwa siku moja tu anapewa Tshs 200,000.00 sawa na askari polisi anayetakiwa alipe chumba kutokana na serikali kutojenga nyumba n.k!!

  Lakini si hao tu, hata walimu wanaoanza na magroup mengine ya wafanyakazi ambao mishahara yao bado ni duni, serikali inashindwa kuwaboroshea na hata ikibororesha inakuwa ni kama hakuna halafu leo unakimbia kuwaongezea watu maposho mkubwa makubwa inashangaza sana.
   
 8. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  hapa mpiganaji wa dhati nitakae mwaamini ni yule tu atakeyegoma hiyo posho kwa vitendo . Excuse za kusema zijui hatausiposign kitabu cha mahudhurio inaingia kwenye account yako hii ni changa la macho
   
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kwa maelezo yako ina maana kunao wenye haki ya kuwa na maisha mazuri na kipato chenye kuridhika na kuna wenye kuvuja jasho ili kuwawezesha wenye haki kuyafurahia maisha. Je hizi posho wanagaiwa wabunge wa chama tawala peke yao? if so nadhani kuna matatizo sehemu fulani.
   
 10. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ma ubinafsi yamewajaa haya majitu!Hayana huruma na masikini.
   
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kwa maelezo yako ina maana moja tu kwangu. Kuwa wale wote wanaozunguka kwenye vile viti vyekundu wana dhamira zao kufikia malengo yao wanawatumia wananchi/wapiga kura kama ngazi kuyafikia malengo yao, na kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kufikiri na ng'amua tutaendelea kuwa ngazi mpaka kiama.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Hakuna "balance" kati ya wema na uovu na hakuna neutrality kati ya ubovu na uzuri. Kuogopa kuchukua upande kwa kisingizo cha uandishi ni sawasawa na kumtaka mwandishi akifika mahali anaona mwanamke anabakwa basi achukue kalamu na kuandika vizuri ili aweze kuripoti bila kuonekana anapendelea upande wowote (kati ya anaebakwa na anayebakwa). Ni sawa na kumtaka mwandishi wa aina hiyo ajivunie kusema kuwa "nilishuhudia msichana anabakwa na kwa kweli nilikuwa neutral!"

  Kwenye ufisadi na utawala mbovu mtu anaitwa kuchukua upande. Mwandishi asiye na upande kwa sababu hataki kuudhi upande mmoja au kuonekana anapenda upande fulani basi amechukua nafasi ya udhaifu. Remember - neutrality is always a position of weakness. I for one ninao upande. Wengine wanaweza wasiwe na upande au wasitake kuwa wazi juu ya upande wao. Wengine wanafikiria kulaumu CDM na CCM sawasawa basi ndio balance! Well it is not.

  Sasa mnawauliza "wapiganaji" ili wafanye nini? Well wangeuliza basi ingewaridhisha? Ni sawasawa na wengine waliotaka CDM wapinge mswada Bungeni kuwa angalau wanaonekane wamepinga. Ukweli ni kuwa jukumu la posho, utawala bora na usimamizi wa sheria linaangukia CCM na serikali yake peke yake. CDM hawana mteule hata mmoja, hajawatunga sheria hata moja, hawana Rais, hawana WAaziri Mkuu, watendaji wote tunaowaona wameteuliwa na viongozi wa CCM na wanasimamiwa na viongozi wa CCM. Sasa kuwauliza CDM wamefanya nini inasaidia nini? Tunatakiwa kuwabana walioko madarakani na katika hili ni CCM.

  Watu watazunguka lakini ukweli utabakia pale pale - CCM ndio wanawajibika na kashaf hii - Spika wao, Naibu wa Spika wao, Rais wao, Waziri Mkuu wao, wana wingi mkuu (absolute majority) Bungeni na hawahitaji hata ushauri wa CDM kupitisha jambo lolote. They are soley responsible of what is happening in the country right now. Kuwaangalia CDM ni kupoteza muda unless tungewapa wao madaraka ndio tungeanza kuwabana.
   
 13. m

  mluguh New Member

  #13
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wawakilishi hawa ni wanyang'anyi wa jasho la wanyonge. Kama wangeisimamia serikali ipasavyo kuwapatia wananchi huduma stahili isingekuwa tatizo, lakini bahati mbaya taasisi zote mbili ni vipofu walioshikana mikono dhidi ya watanzania wenzao waliowalaghai wawapigie kura wapate kula. Lakini wakumbuke kuwa vibaka wakamatwapo huchomwa moto kutokana na hasira iliyolundikana muda mrefu katika nyoyo za waliodhulumiwa kwa muda mrefu. 40 yako itafika tu kwani machungu wanayopata wananchi huzinoa bongo zao kuyaona maovu yanayofanyika dhidi yao. Wakati ukiwadia watatafuta pa kujificha wasipaone.
   
 14. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  acha tabaka la walionacho na wasionacho liendelee kujengwa mpaka hapo watu watakapojitambua na mi naona kama watu wanachagua ccm kuwa wanaenda kuwawakilisha sasa waone huo uwakilishi uko sawa ?/?
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye RED nina mashaka makubwa sana juu ya uwelewa wako wa mambo,labda tu ungetueleza Chadema walikwenda ikulu kwa mazungumzo kuhusu nini, hapo ndipo utakapojiona upeo wako ni mdogo sana.
   
 16. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  wabunge wote wanazichota na linapokuja suala hili si muoni mbunge wala chama cheenye maelezo na msimamo ulionyooka kabisa mpaka mwisho kuhusu hili la posho inauma sana maana nilitegemea hata hichi kidogo tunachopata tungewana in proportional ila wapi wee
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  "POSHO SI DHAMBI , DHAMBI NI POSHO INAPOKOSA UTU" - LEMA

  Nimetafakari sana niliposoma kwenye magazeti kuwa sisi wabunge tumeongezewa posho bila hata sisi kufahamu jambo hilo .

  Na kila mtu ametoa maoni mbali mbali juu ya jambo hili , ni kweli ni msimamo wa chama chetu (Chadema) kupinga posho mbali mbali zisizokuwa na tija na tulikubaliana hivyo kwenye vikao vya Chama Chetu vya Wabunge na kupinga mfumo wa posho uliopo kwa sasa ni msingi sahihi wa Chama kuonyesha hisia na ubadhilifu mkubwa unaotokana na ulipwaji mbaya wa posho kama ambavyo imejitokeza mara nyingi na hata hivi karibuni tumeshuhudia madudu mengi kwenye ripoti ya kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Jairo.

  Lakini suala hili haliwezi kuepukwa kabisa na Chama kinajua ila utaritibu wa ulipwaji posho kwa watumishi mbali mbali wa umma ni tatizo kubwa na kuna mapungufu mengi sana ndio maana kupinga posho haina maana tu ya kupinga kiwango cha pesa anachopokea Mbunge au mtumishi yeyote wa UMMA bali mfumo mzima wa sera ya posho ili uweze kuwa na tija na kupunguza mianya ya wizi katika mfumo huu ambao umekuwa ukitumika vibaya kuliibia Taifa.

  Pengine sisi wabunge ni vyema tukatambua kwanini wananchi wanapiga kelele kuhusu posho nilishawahi kusema Bungeni wakati nachangia kwenye Wizara ya Ustawi wa Jamii kuwa mshahara wa Wabunge , posho mbali mbali za Wabunge pamoja na marupurupu mengine yanaonekana kuwa anasa pale watumishi wengine wa serikali kama Manesi ,Asikari Magereza,Polisi ,Makarani Mahakamani wanapolipwa chini ya shilingi laki mbili na nusu kwa mwezi na wakati huo huo wanasikia mwakilishi wao akipiga kelele Bungeni kuwa posho ya laki mbili kwa siku ni ndogo.

  Ndio maana nimesema "POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU , Na hapa lazima kutokee ugomvi wa kimasilahi na mgogoro mkubwa kati ya mwakilishi na anaye wakilishwa.

  Pengine masilahi anayopata Mbunge ni ya kawaida sana tena sana ila yanaonekana kuwa anasa pale ambapo yeye kama mwakilishi anapolipwa kiwango cha posho cha siku moja ambacho ni sawa na mshahara wa mpiga kura wake kwa siku thelasini.

  Mimi nafikiri namna peke ya wabunge kutetea masilahi yao bora kwanza ni kupigania masilahi ya wapiga kura wote Tanzania na tukifanya hivi kama Wabunge hakuna Mwananchi hatakayeshangaa kwanini Mbunge awe na masilahi bora kwani ubunge ni nafasi kubwa pia inayositahili heshima kubwa kwani ni uwakilishi katika jamii.

  Ebu jiulize wananchi wanaposikia Wabunge wamepewa milioni tisini kununua magari na wakati huo huo serikali imenunua bajaji kuwa ndio magari ya kubeba wakinamama wajawazito yaani (Ambulance) ni wazi kabisa wabunge wataonekani ni watu katili na walioenda bungeni kwa masilahi binafsi japo kuwa ukweli unabaki kuwa Wabunge wanahitaji magari imara na mazuri.

  Lakini Wabunge kama watafikiri Bajaj ni sawa kuwa gari la wakinamama wajawazito na wao kuchukua milioni tisini kwa magari ya binafsi bila kupiga kelele na kukataa unyanyasaji huu kwa wakina mama na Wagojwa ,hivyo ni dhahiri kuwa ugomvi hapa katika posho na masilahi ya Wabunge utasababishwa na tofauti ya masilahi dhidi ya wale waliowachagua kuwatetea ,Hivyo namna pekee Mbunge anaweza kutetea masilahi yake bora bila kuingiliwa na na kubugudhiwa ni Mbunge kuanza kufikiria masilahi ya watu wengine ambao pia ni watumishi wa UMMA ambapo yeye ni mwakilishi wake .

  Nafahamu kuwa pamoja na kupinga mfumo mzima wa utaritibu wa posho ulivyo sasa tafakari ya kweli ni kwamba masilahi ya watumishi wa UMMA bado ni madogo sana kwa hiyo Uzalendo wa kweli sio tu kupinga masilahi bora bali serikali iwajibike kikamilifu kudhibiti wizi na ufisadi unaotokana na utaritibu mbaya wa ulipwaji posho , kuongeza makusanyo katika kodi mbali mbali ,kutumia rasilimali za Nchi vizuri ili masilahi ya watu wote Nchi hii yaweze kuwa na tija kwa maisha ya Watanzania na watu wengi waweze kuishi maisha ya faraja na kutimiza malengo yao muhimu ya maisha
  Ndio maana nimesema "POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

  Nitakuwa ni mtu mwenye mashaka sana kama nikiwaza kuwa masilahi duni na maisha ya kuishi chini ya kiwango ni Uzalendo , Sasa Wabunge mkitaka msipigwe mawe barabarani ,msitukanwe , msionekane ni wasaliti wa jamii aliyowachagua , Sasa huu ni wakati wakusema , Mshahara wa Polisi ,Magereza,JWTZ, Walimu, Makarani Mahakamani na hata sekta zote za Serikali na Binafsi masilahi ya mishahara yao yaongezwe kwa asilimia kama ambavyo mmjiongozea nyie kwenye posho zenu tena zinazohusu siku moja tu lakini wao wanaomba kwa mwezi lakini hawapati.

  Sasa pamoja na kupinga mfumo mzima wa sera ya posho kama ambavyo Mwenyekiti wetu wa Taifa alisisitiza na kuomba sera hii iangaliwe upya ili kupunguzia Taifa mzigo mkubwa na kuboresha viwango vya mishahara vya watumishi wa UMMA , ni vyema nikarudia kusema kuwa ""POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

  Ni kweli gharama za Maisha zimepanda lakini hazikupanda kwa Wabunge tu pia kwa Wananchi wote wanaoishi Tanzania , Hivyo tukiacha ubinafsi tukawajibika vizuri Bungeni kulinda masilahi ya Taifa na kutetea maisha ya Wananchi wetu, bila shaka hata tukionekana tunaendesha magari ya kifahari kama Rolls Royce, Bentley, Benz , hakuna mwananchi hatakeyesema kwa nini Mbunge anaendesha gari zuri kwani kila mtu atakuwa na afadhali ya maisha ktk Nchi yetu.

  "Baba yangu aliniambia " Watu wengi wanaokwenda Kanisani na Misikitini huwa wanatoa sadaka ndogo kuliko pesa wanayotumia sehemu mbali mbali za anasa ndio maana Taifa lina Bar nyingi kuliko nyumba za Ibada" TAFAKARI

  LEMA- MP
   
 18. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  kwa kweli kwa hili posho ni shaka na wabunge wote unless aje mmoja ambaye atagomea kabisa hili ongezeko sihitaji longolongo ooh zijui zipite mfuko wa mbunge mara zitumikaje aahh hapa swala no posho tu
   
 19. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  pana ka ukweli fulani
   
 20. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ndo nchi ilipofikia huko so hakuna la kushangaa
   
Loading...