Ongezeko la Posho za Wabunge ni Wizi na Dhulma dhidi ya Wafanyakazi

Mimi nafikiri inawezekana walizungumzia posho ya mafuta maana ni TSh 50,000.
hapana
hawa jamaa wanachua

  • fedha za mafuta 50000/=
  • posho za vikao 200000/= from 70000/=
  • fedha ya kujikimu nje ya jimbo ya jimbo lake 80000/= ....

total 330000/= per day
 
Matarajio yangu yapo kwangu mwenyewe. Siwezi kumtarajia Chadema wala CCM wala chama chengine chochote cha kisiasa kunifikisha nitakapo.

Tunisia, Misri wameweza, nguvu ya umma haimaanishi vyama vya siasa.

hapo umenena mkuu. swali ni kuwa, tutafikiaje huko?
 
hapana
hawa jamaa wanachua

  • fedha za mafuta 50000/=
  • posho za vikao 200000/= from 70000/=
  • fedha ya kujikimu nje ya jimbo ya jimbo lake 80000/= ....

total 330000/= per day

mtu kujikusanyia laki tatu kwa siku, wakati mie kazi ngumu, siku 30 nakwapua 190,000/=? kazi ipo, et maisha yamepanda kwa aliyekuwa anachukua 80,000/=+70,000/=+50,000/- = 200,000/, yamepanda sasa anachukua 200,000/-+80,000/-+50,000/- =330,000/- kwa siku, wakati huyu anayechukua 190,000/= yuko vilevile. sikubaliani
 
Kila nikiinagalia na kuongea na watanzania kila mmoja anataka kuwa mwanasiasa ama Mbunge, Raisi au Diwani. Nikadadisi sana kulikoni leo hakuna anayependa taaluma tena? Mbona zamani ilikuwa mtu akiwa daktari injiinia, mwalimu , Prof ilikuwa ni sifa kubwa na heshima? Hii imekwenda wapi.

Taaluma zilikuwa zinaheshimika sana, mwenye elimu, ambayo alikuwa anaitumia kuendeleza jamii alikuwa anapa heshima kubwa sana. Utu, uzalendo, kukubalika na kuheshimiwa viliwafanya wote wenye taaluma kujiona nao wananafasi kubwa sana katika jamii. Ilikuwa ni jambo la kawada mwalimu wa primary kujiendeleza mpaka kuwa mkurugenzi. Hali hiyo imepotea kabisa.

Leo Tanzania kila raia anatafuta bora elimu, iwe ya wizi, kuibia mitihani, vodafasta, au kwenda India wiki mwezi mwaka na kurudi ama degree, masters, phd nk kutokana na aliyemtuma kamwambia alete nini. Umuhimu wa taaluma yetu sisi wazawa umekufa kwani wapoanga bajeti na wakusanya kodi hawahitaji elimu yetu kwa lolote. Leo Serikali ya wanasiasi ikihitaji tiba Appolo India, ikihitaji injinia analetwa kutoka nje, ikihitaji kutoa tender inaagizwa kampuni ya nje, watoto wao wakihitaji shule wanapelekwa nje. Utaalamu wa Mtanzania umewekwa kampuni.

Kwa matumizi haya wanasiasi wamekuwa ndio ajira yenye mshahara mkubwa kuliko ajira yeyote Tanzania. Wanasiasa hawa wanapigania maslahi makubwa kwani wanajua wazi hakuna huduma wanaipata Tanzania.

Leo Tanznaia imeuuwa elimu, viwanda, ubunifu, na uzalendo. Ni nchi pekee wanasiasa ndio matajiri bila kulipa kodi, kuwa na biashara zaidi ya siasa. Sitashangaa kwamba hakuna mbunge ambaye hali rushwa kwa njia moja au nyingine.


Ukitaka kujua Mbunge ni mla rushwa mwizi au fisadi anagalia maisha yake na watu wanamzunguka gawanywa na fedha anazolipwa pamoja na kwamba ni nyingi sana ila 144M kwa mwaka ukiingalia sana ni zaidi 244M wengine 344M na wengine 2B kwa ajira ya siasa tu. Wanaoibiwa ni sisi wananchi.

Wananchi inatakiwa kuungana na kudai fungu letu la kodi kwa lazima, tuungane kudai fungu letu la gesi, madini, wanyama, twiga, bandari, nk kwa lazima. Imefika wakati kujitawala wenyewe kwani tuliowaamini wanatuibia bila kujali sisi ndio tuliowaajiri.

Tatizo kubwa la wanasiasa sio kujilipa tu mishahara mikubwa bali kutusahau kwamba sisi ndio ndio tunawapa hiyo mishahara. Hawana utu wala uzalendo. Ukiwaona wanapiga kelele sana ujue mtu anataka kamati akipewa ulaji zaidi anakuwa zaidi ya kimya anakuwa zezeta unabakia unashangaa.

Nimechoka mgomo wa madaktari ambao umekuwapo kwa miaka kadhaa sasa, hawa wameamua kuingia tu mahospitali kutimiza wajibu ila wamegoma kutiba. Wanahaki kabisa huwezi kuwadharau kuwadhalilisha halafu ukataka huduma zao. Nimechoka mgomo wa waalimu , wameamua kuzalisha ziro na bongo hoi. Hakuna mwalimu anayefunisha tena, wameona liwalo na liwe wanakwenda shule kupiga soga kila mmoja akifikiri ni vipi atailisha familia yake, hawa sio tu wanadharauliwa bali wananyanyaswa, kuonewa na kutengwa na watawala wanasiasa wezi.

Leo Tanzania kila taaisisi imekufa kwani elimu imekufa. Kilichobakia ni kuhangaika na lama za ufaulu kama vile hizo alama zikiwa (A) zote ndio tumetatua tatizo. Na walivyo vipofu kunasiku watasema (0) ifanywe (A) kwani uwezo wao wa kufikiri ni ile 12M mengine hawajali. Wabunge hawa na mawaziri wao wapo tayari kuiwa nchi kwa kipande hiki cha keki.

Nimeoteshwa ndoto kuwa siku moja watanzania watesema hapana, itakuwa ni kasheshe kuanzia Mwanza mpaka Mtwara, Kigoma mpaka Arusha, Tanga mpaka Tabora, Moro mpaka Dar dodoma mpaka iringa na mbeya mpaka sumbawanga. Siku hiyo polisi watatangulia mbele na wanajeshi watalinda raia ndio itakuwa siku ya uhuru kamili na heshima itarudishwa kwa raia na sanduku la kura la ukweli.

Nimeota ndoto kuwa siku moja watanzania watamkaa kila mwanasiasa mnafiki, anayetulaghai anatutetea kumbe anatucheka usogo. Watanzania watamtaka mwanasiasa anayeishi nao kijijini, wanatumia barabara moja, maji bombo moja, hospitali moja, shule moja ili aweze kuwatetea kwani anashiriki matatizo yao na kero zao. Leo wote wanaodai wanatutetea wanaishi Mijini na kuja huku kuomba kura, hawashiriki matatizo wala hawana kitu cha kutuombea kwani hawatujui. Wanajenga vijichanja vya kuombea kura, wakipata wansepa.

Siku inakuja nimeota, nimewaona watanzania wanagawana mali zao zilizoibiwa, kila mtu anabeba chake. Wamechoka. Hata wana wa Israel walikaa misri kwa muda, herodi aliimini watumwa wale hawawezi kuerevuka alishangaa sana. Mzungu wa marekani hakuaamini kuna siku mweusi ataerevuka pamoja na kumnyima elimu, huduma za afya nk ila aliamka akatumia street justice akapewa haki yake. Leo mweusi ni Raisi Marekani, chimbuko lake ni street justice na wengi sana walipoteza maisha.

Nimeota siku moja mbavu za ulimboka zitaimbwa uhuru, damu ya Mwangosi itasifiwa ni shujaa, kilio cha uhuru wa habari kitakuwa historia.

Nimeota siku moja kila mtoto wa mtanzania atakuwa na haki sawa za kujiendeleza, kuwa tajiri, kuwa na elimu bora na ushindani wa kweli sio leo ukiwa mtoto wa mwanasiasa lazima utajirike kwa wizi, na hila.

Nimeoteshwa kuwa haki hii haitahusisha viongozi wengi wa dini kwani nao wamemsaliti Mungu kwa kuwa makuwadi wa wanasiasa wadhalimu. Nyumba za ibada zimetumika kama kichanja cha kulinda siasa chafu na kuinua wezi wa wananchi kwa mgongo wa siasa.

Heri siku hii isikukute wewe mwanasiasa mnafiki na mwizi. Heri siku hii isikukute wewe unayeshiba leo kwa fedha za kodi za masikini. Heri siku hii isikukute wewe unayefunga wasio na hatia ili uendelee kuishi kwa hila. Heri siku hii isikukute wewe unawadanganya eti unawatetea wakati huyajui maisha yao.

Chief Mkwawa
Tanzania imekufa-itafufuka mpya na itajengwa upya sio na wanasiasa hawa-wote wameonja damu ya asiye na hatia.
 
Bado Lema na mambwiga wengine wanasema mshahara mdogo na posho waongezewe.

Nimemshangaa sana Lema na baadhi ya wabunge wa CCM.

Kama mnaona ubunge haulipi tafuteni kazi zingine.

Wengine rudini kwenye kazi zenu za zamani mkapambane na Interpol.
 
Siasa inachafuliwa kwa sababu watu wasiopenda siasa chafu wameruhusu wanaopenda siasa chafu wafanye siasa kwa gharama ya Tanzania.
 
Bado Lema na mambwiga wengine wanasema mshahara mdogo na posho waongezewe.

Nimemshangaa sana Lema na baadhi ya wabunge wa CCM.

Kama mnaona ubunge haulipi tafuteni kazi zingine.

Wengine rudini kwenye kazi zenu za zamani mkapambane na Interpol.

Leo umeongea kizalendo sana umenifurahisha sana. Tunahitaji hii kusonga mbele. Lema nae sio chadema na kama chama chake kimepinga posho yeye asituletee uroho ktk hili tusimchekee mbunge yeyote. Leo bungeni nimependa wabunge wa CCM nao walivyomshukia kaghasheki na mathayo kwa uzembe wao unaomhaibisha rais wameonesha uzalendo sana.
 
Bado Lema na mambwiga wengine wanasema mshahara mdogo na posho waongezewe.

Nimemshangaa sana Lema na baadhi ya wabunge wa CCM.

Kama mnaona ubunge haulipi tafuteni kazi zingine.

Wengine rudini kwenye kazi zenu za zamani mkapambane na Interpol.

.
.
.
.
.

.
.
mjomba wewe sometimes yes,sometimes no!
ningelike,natumia simu.
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom