Sasa hapo unakuwa ujeuli wa mwajiri na unyonge wa mwajiliwa kwenye kudai haki zake ila kwa mtu wa mkataba akitumia huo mkataba anapata haki zake, mfano Kila mwezi kwenda kuangalia Nssf kama hela zake zimeingia maana namba ya Nssf mfanyakazi anakuwa nayo na kama hela haziigii kwenye account yako basi unawajulisha Nssf wafate hela zako, kuhusu kufanya kazi mpaka jumapili hapo inategemeana na mkataba wako umeandikwaje kama mlikubaliana na mwajiri utaranya kazi mpaka jumapili na mkataba ukaandika hivyo basi huna budi kufanya kazi maana hata serikalini Kuna watu wanafanya kazi mpaka jumapili ila mara nyingi kazi za hivyo Zina zamu hivyo kufidia masaa ya sheria za kazi na yakizidi ndo overtime, kingine Kila mkoa una ofisi za labor na ofisi za usuruhishi wa migogoro kazini kwaajili ya kumlinda mfanyakazi pale mkataba wake usipofatwa na mwajiri unakwenda kushitaki huko na mwajiri anawajibishwa pale akikutwa na makosa kikubwa uwe na mkataba na ufanye kazi kwenye sehemu zilizojisajili serikalini kwa usalama wako hizo sehemu au kampuni zilizojisajili serikalini na kutambulika huwa zinakaguliwa mara kwa mara kama zinafata sheria za kazi na usalama wa mfanyakazi kazini.kukatwa paye na nssf sio kigezo cha sector binafsi kufata masharti ya serikali.. uliza watu wangapi wa sector binafsi wanafanya kazi mpaka jpili...wangapi wanafanya overtime na hawalipwi hizo hela.. hizo nssf zenyewe maboss wanakata ila hawapeleki helaa ila HUWEZI KUFANYA LOLOTE zaidi ukitaka maslahi makubwa uache kazi ukatafute kwingine kwenye maslahi unayotaka.