Ongezeko la kodi ya Mafuta ni kuwalipa fadhila "Wakubwa" wanaomiliki hisa/makampuni/vituo vya Mafuta?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,515
Serikali awamu ya 4 ilikuwa ni moja ya Serikali Fisadi zilizopata tokea Barani Afrika. Kwa wanasiasa na watoto wao kuchuma mali kadri ilivyowezekana.

Mpaka kufikia kuuza/gawa viwanja/maeneo ya Serikali kutumika na Makampuni binafsi. Refer eneo la Tazara kupewa Kampuni moja ya kuuza Mafuta ya Magari.

Nadhani hawa watu wamerudi sasa. Wamerudi kuja rudisha pesa zao. Na wameingia kwa nguvu kupitia ongezeko la kodi ya mafuta.

Ni akina nani walio nyuma ya hili? Ni akina nani wamiliki wa Vituo kama Lake Oil, Oil Com n.k?
 
Hamna bhana.

Hebu tupitie bei za mafuta soko la dunia miaka 5 iliyopita kama zinavyotolewa na Trading Economics:-

Oil.png

Hapo utaona July 2018 bei ya mafuta soko la dunia ilikuwa sawa na ya hivi sasa!

Now tuangalie bei ya mafuta Tanzania hapo July 2018

Ewura.png

Sasa je, bei ya TSh. 2409 wakati wa JPM, yeye alikuwa analipa fadhila kwa nani?

No wonder Wabongo ni rahisi sana kudanganywa na wanasiasa!! Kumbe hapa bei ingekuwa TSh. 1,200/= watu wangeanza kumsifia Rais! Yaani hadi kesho bado watu hamjui kwamba bei ya mafuta inategemea sana na bei ya bidhaa husika soko la dunia?!

Yaani hadi leo mnashindwa kufahamu kwamba, njia pekee ya kutoathirika na bei ya soko la dunia ni kwa serikali kupunguza tozo na baadhi ya kodi kwenye bidhaa hiyo muhimu?

As long as Serikali ya CCM imeshindwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato, na kufanya kodi kwenye mafuta kama moja ya vyanzo vikuu vya mapato, basi, no one. I repeat, NO ONE can control gasoline price!

Hata huyo Magu hakuwa na huo uwezo!
 
Mkuu, nakuuliza swali moja tu na ukifahamu jibu basi ndilo jibu la hii hoja yako nzito, unadhani ni kwanini serikali ya CCM imegoma kubadili mfumo wa Elimu ?
Serikali zote zisizojiamini mtaji wao mkuu ni kundi la wajinga!

Kama una mfumo wa elimu unaotengeneza wajinga wengi zaidi, basi huo ndio mfumo bora kwa serikali zote zisizojiamini na serikali za hovyo kwa sababu katu hawapo tayari kuwa na kuongoza watu wenye uelewa na wadadisi!

Ukibadilisha na kuleta mfumo bora zaidi, maana yake unataka kupunguza kundi la wajinga kwenye taifa. Kundi lile lile linalokufanya uwe unarudi madarakani tena na tena, hata kama unarudi kwa hila!

Yote hayo, kundi la Wajinga wala hawatayaona, na badala yake wataishia kukushangilia hata kama baada ya shamra shamra zao, watarudi nyumbani na kulala njaa huku wakiwa hawana hata uhakika wa kesho!
 
Serikali zote zisizojiamini mtaji wao mkuu ni kundi la wajinga!!

Kama una mfumo wa elimu unaotengeneza wajinga wengi zaidi, basi huo ndio mfumo bora kwa serikali zote zisizojiamini na serikali za hovyo kwa sababu katu hawapo tayari kuwa na kuongoza watu wenye uelewa na wadadisi!...
Asante
 
Hivi mkuu! Kuingiza mafuta hapa nchini ni sh ngapi kwa lita kabla ya kodi?
Hilo swali linaweza kujibiwa na importers (or TRA) kwa sababu ndio wanaofahamu ALL COSTS associated with oil imports!!

Bei niliyoweka hapo juu ni ya soko la dunia ambayo by average, ni $75 kwa pipa, ambayo ni takribani Sh. 174,000!!

Pipa moja la mafuta ni takribani 160 liters, which means, ni takribani Sh. 1090 kwa lita wakati yakiwa bado sokoni!
 
Hamna bhana....

Hebu tupitie bei za mafuta soko la dunia miaka 5 iliyopita kama zinavyotolewa na Trading Economics:-
View attachment 1837439

Hapo utaona July 2018 bei ya mafuta soko la dunia ilikuwa sawa na ya hivi sasa!

Now tuangalie bei ya mafuta Tanzania hapo July 2018

View attachment 1837441

Sasa je, bei ya TSh. 2409 wakati wa JPM, yeye alikuwa analipa fadhila kwa nani?

No wonder Wabongo ni rahisi sana kudanganywa na wanasiasa!! Kumbe hapa bei ingekuwa TSh. 1,200/= watu wangeanza kumsifia Rais! Yaani hadi kesho bado watu hamjui kwamba bei ya mafuta inategemea sana na bei ya bidhaa husika soko la dunia?!

Yaani hadi leo mnashindwa kufahamu kwamba, njia pekee ya kutoathirika na bei ya soko la dunia ni kwa serikali kupunguza tozo na baadhi ya kodi kwenye bidhaa hiyo muhimu?!!

As long as Serikali ya CCM imeshindwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato, na kufanya kodi kwenye mafuta kama moja ya vyanzo vikuu vya mapato, basi, no one... I repeat, NO ONE can control gasoline price!

Hata huyo Magu hakuwa na huo uwezo!!

Good analysis bro
 
Serikali zote zisizojiamini mtaji wao mkuu ni kundi la wajinga!!

Kama una mfumo wa elimu unaotengeneza wajinga wengi zaidi, basi huo ndio mfumo bora kwa serikali zote zisizojiamini na serikali za hovyo kwa sababu katu hawapo tayari kuwa na kuongoza watu wenye uelewa na wadadisi!...
Kabisa mkuu,hili ndilo jibu sahihi. Na ndio sababu pekee CCM hawataki hata katiba mpya.
 
Hilo swali linaweza kujibiwa na importers (or TRA) kwa sababu ndio wanaofahamu ALL COSTS associated with oil imports!!

Bei niliyoweka hapo juu ni ya soko la dunia ambayo by average, ni $75 kwa pipa, ambayo ni takribani Sh. 174,000!!

Pipa moja la mafuta ni takribani 160 liters, which means, ni takribani Sh. 1090 kwa lita wakati yakiwa bado sokoni!
Kuna mtu kaniambia mpaka mafuta yanaingia hapa nchini ni sh. 1,110 kwa lita bila kodi.

Kama hiyo bei ni kweli basi wanaolalamika bei kuwa juu wako sahihi maana inaonekana bei inakuwa juu kutokana makodi yasiyoeleweka,.

Kama hiyo bei ni kweli, mafuta yanatakiwa yauzwe si zaidi ya 1,600
 
Hamna bhana....

Hebu tupitie bei za mafuta soko la dunia miaka 5 iliyopita kama zinavyotolewa na Trading Economics:-
View attachment 1837439

Hapo utaona July 2018 bei ya mafuta soko la dunia ilikuwa sawa na ya hivi sasa!

Now tuangalie bei ya mafuta Tanzania hapo July 2018

View attachment 1837441

Sasa je, bei ya TSh. 2409 wakati wa JPM, yeye alikuwa analipa fadhila kwa nani?

No wonder Wabongo ni rahisi sana kudanganywa na wanasiasa!! Kumbe hapa bei ingekuwa TSh. 1,200/= watu wangeanza kumsifia Rais! Yaani hadi kesho bado watu hamjui kwamba bei ya mafuta inategemea sana na bei ya bidhaa husika soko la dunia?!

Yaani hadi leo mnashindwa kufahamu kwamba, njia pekee ya kutoathirika na bei ya soko la dunia ni kwa serikali kupunguza tozo na baadhi ya kodi kwenye bidhaa hiyo muhimu?!!

As long as Serikali ya CCM imeshindwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato, na kufanya kodi kwenye mafuta kama moja ya vyanzo vikuu vya mapato, basi, no one... I repeat, NO ONE can control gasoline price!

Hata huyo Magu hakuwa na huo uwezo!!

Hoja ni kwamba jIrani yako anaetoa kwako ana bei ndogo kulipo wewe.
 
Kuna mtu kaniambia mpaka mafuta yanaingia hapa nchini ni sh. 1,110 kwa lita bila kodi.

Kama hiyo bei ni kweli basi wanaolalamika bei kuwa juu wako sahihi maana inaonekana bei inakuwa juu kutokana makodi yasiyoeleweka,.

Kama hiyo bei ni kweli, mafuta yanatakiwa yauzwe si zaidi ya 1,600
Mchina anatafutiwa soko na gesi yake, kuna watu wana mikono kwenye mpango ule. Wakisema wakae kimya kukibuma, nao watapata shoti. Hebu fuatilia ununuzi wa magari yanayotumia gesi hivi sasa umeongezeka au kupungua
 
Kuna mtu kaniambia mpaka mafuta yanaingia hapa nchini ni sh. 1,110 kwa lita bila kodi.

Kama hiyo bei ni kweli basi wanaolalamika bei kuwa juu wako sahihi maana inaonekana bei inakuwa juu kutokana makodi yasiyoeleweka,.

Kama hiyo bei ni kweli, mafuta yanatakiwa yauzwe si zaidi ya 1,600
Kimsingi, na bei kwa lita yakishaingia TZ kabla ya kodi, na yenyewe itategemea na bei ya soko la dunia! Haiwezi kuwa Sh. 1,110 wakati wote, labda kama amesema hiyo bei ni kwa mzigo wa mwisho ulio-determine bei ya sasa ya rejareja!

Hata hivyo, usisahau hii nchi ina lundo la mikodi na tozo mbalimbali, kwa sababu serikali inafanya mafuta kama moja ya vyanzo vikuu vya mapato, na hivyo kuendelea kuchomekea kodi na tozo mbalimbali!

Bunge la Mwigulu sikufuatilia(nasikia wameongeza tena) , lakini nakumbuka mwaka jana, kodi kwa lita moja ilikuwa TSh 313. Sasa ongeza hapo kwenye 1,110... tayari inakuwa Sh. 1410. Na ukumbuke, hiyo sio kodi au tozo pekee, which means, hata inapokuwa Sh.1110, bado hawawezi kuuza Sh 1600/=

The Boss kwenye thread yake ameonesha bei ndogo sana kwa Zambia (Zambia), hata nami nikashituka! Nilivyofuatilia, kumbe wenzetu wametoa kipindi cha mpito kuanzia February hadi August ambapo wameondoa makodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta!
 
Back
Top Bottom