nyachina
JF-Expert Member
- Nov 10, 2013
- 423
- 761
DENI LA TAIFA
Naomba kutoa hoja hii tafakarishi kwa mustakabali wa nchi yetu.
Naomba tuwapime viongozi wetu katika ukuaji wa uchumi wa nchi ukilinganisha na ongezeko la deni.
Tulinganishe ukuaji wa deni kati ya awamu ya Nne ya JK (miaka 10) na awamu hizi mbili za JPM na SSH.
Wakati JK anaingia madarakani alikuta deni la taifa ni Shilingi trilioni 10.93 na wakati anaondoka aliacha deni limefikia 35 trilioni sawa na ongezeko la 221%. Ongezeko hili lilichangiwa kwa kiasi fulani na riba pamoja na kupungua kwa thamani ya Shilingi ya Kitanzania.
JPM alipoingia madarakani alikuta amerithi deni la trilioni 35 ambapo mpaka anafariki deni lilifikia 60.7 trilioni sawa na ongezeko la 73.4%
SSH alikuta deni likiwa 60.7 trilion na mpaka muda huu pamoja na kila mwaka kutenga bajeti kubwa ya kulipa deni la taifa lakini bado deni limesogea hadi kufikia 107 trilioni sawa na ongezeko la 76.3%
Ukiangalia kwa miaka hii 10 deni la taifa limeongezeka kutoka 35 trilioni hadi 107 trilioni sawa na 205%.
Katika miaka hii 10 serikali imetumia fedha nyingi sana katika miradi mikubwa ya maendeleo katika kilimo, miundombinu ya Elimu, Afya, barabara, maji, mahakama, umeme, SGR na kujenga Makao Makuu ya nchi Dodoma.
Pia haikuwa nyuma katika utoaji wa huduma katika Elimu, Afya na huduma nyinginezo.