Tanzania hakuna amani bali kuna utulivu wa wananchi kutojuwa haki zao...
Hakuna amani kama mwananchi hapati dawa hospitali, shuleni hakuna elimu bora na yenye tija, wakulima wa pamba wanadhulumiwa pamba yao, wakulima wa korosho wapunjwa bei ya korosho yao kuliko bei inayouzwa katika super markets, wakulima wa mahindi wanazuiwa kuuza mahindi yao nje, wananchi wanauwawa kila siku kwenye migodi na serikali imekaa kimya; watu wanateswa (mfano wa Dr. Ulimboka) na serikali haichukui hatuwa, tunaona watoto wa viongozi wakubwa wanavyotanua na kuwa watawala wadogo!
KATIKA HALI KAMA HII HUWEZI KUWA NA AMANI WAKATI SERIKALI HAITIMIZI WAJIBU WAKE