Ombi Maalumu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Ndugu Dkt. Magufuli na Watanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,272
110,859
Ni matumaini yangu makubwa kuwa Wanachama wote wa huu Mtandao wa JamiiForums mpo salama kabisa na Mwenyezi Mungu anabariki japo najua Changamoto za hapa na pale kwa Mwanadamu haziepukiki ila Kikubwa ni kutokata tamaa na Kumtumainia Yeye tu Maulana / Mola kwani Yeye ndiye mpangaji na mtoaji wa Riziki na Baraka.

Naanza Kwanza kwa Kukiri kuwa najua Watanzania wote tuna Matatizo yetu pamoja na Shida za Kimaisha ambapo kila Mtu kwa namna moja au nyingine nae anahitaji Msaada mkubwa wa Kiuwezeshwaji ili Maisha yake yaweze Kusimama ili aondokane na Ugumu wa Kimaisha mkubwa ambao unamkabili.

Naandika huu Uzi kwa Serikali ya Tanzania hasa Kwake Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli juu ya Kumuomba amuangalie huyu Binti Anna Zambi ambaye nakiri wazi kuwa tokea jana nilipoanza Kuona na Kusikia taarifa zake kama Mwanadamu ambaye huwa nina Hisia Kali kila mara najikuta napatwa tu na Huzuni huku Machozi yakinitoka.

Najua Watanzania wengi (hasa Watumiaji wa Mitandao) wameshapata hii taarifa juu ya Msiba mkubwa ambao umemkubwa Mdogo wetu, Mwanetu, Mjukuu Wetu, Dada yetu na Mtanzania Mwenzetu Anna Zambi wa Kufiwa na Wazazi wake wote Wawili pamoja na Ndugu zake wote kwa Ajali ya Basi iliyotokana na Mafuriko yaliyotokea Mkoani Tanga wakiwa njiani Kuelekea katika Mahafali yake ya Kidato cha Nne.

Kila nikivivaa Viatu vya Anna Zambi najikuta nalia tu na nashindwa kupata Majibu kuwa kama hali iliyomkumba Yeye ingenitokea Mimi GENTAMYCINE ningeihimili vipi kwa Machungu makubwa ambayo ningekuwa nayo huenda na Mimi nisingeona tena Thamani ya Kuwepo Kwangu hapa Duniani hivyo Kuamua Kuwafuata Wazazi wangu na hao Ndugu zangu huko Makaburini walikolala Milele.

Ombi langu kwa Serikali ya Tanzania na hasa kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kama litakuwa ndani ya Uwezo wake basi aweze Kumsaidia huyu Binti Anna Zambi hasa kwa Kumsomesha hadi Elimu ya Juu huku wakimsaidia na Huduma zote muhimu za Kibinadamu ili basi hata kama amewakosa Wazazi wake wote Wawili pamoja na Ndugu zake aweze kupata Elimu na Mafanikio ya Kimaisha ambayo angalau yatakuwa nafuu Kwake na Kumpunguzia Machungu ambayo naamini yataendelea Kubakia Moyoni mwake hadi Umauti wake.

Pia huyu Binti asaidiwe haraka Kisaikolojia kwani siyo Siri tena kwamba kwa hili Tukio Kubwa na la Huzuni lililomkuta hivi sasa huyu Binti Anna Zambi hayuko vizuri Kiakili (Kisaikolojia) na kuna Uwezekano mkubwa kama hatopata huo Msaada basi huenda nae akaamua Kujitoa Uhai au hata ‘ akawehuka ‘ kwani kwa Umri wake mdogo na tukio zima sidhani kama ana Kifua cha Kuhimili Machungu aliyonayo.

Na kama itawezekana pia nje ya Serikali basi hata Watu binafsi (Mimi na Wewe) au Mashirika au Taasisi mbalimbali nazo zinaweza Kujiwekea Utaratibu wa Kuchukua Jukumu la angalau Kufanya Jambo jema tu kwa huyu Binti Anna Zambi ili tu aweze Kufarijika na Kuona kuwa hata kama amepatwa na Tukio hili la Kihuzuni lakini Maisha bado yanatakiwa yaendelee na Kikubwa ni Kuomba Rehema kwa Mwenyezi Mungu kwani Yeye ndiye anajua kwanini aliamua Kuwachukua Wazazi wake na Ndugu zake wote kwa wakati mmoja huku akibakia peke yake.

Waswahili wenyewe tunajijua kwani wapo wale Wahuni ambao labda wanaweza Kutumia Matatizo ya huyu Binti Anna Zambi wakaamua ama ‘ Kumuhadaa ‘ kwa hapa na pale huku wale Wanaume wenzangu ‘ Mabazazi/ Mafataki ‘ nao wakaamua Kuanza ‘ Kumtongoza ‘ na Kumuharibia kabisa Malengo yake ya Kitaaluma na Kimaisha. Hapa nawaomba mno Wanasheria na hasa Watu wa Haki za Binadamu wawe nae karibu ili basi kama ana Haki zake azipate na wazilinde huku pia wakimsimamia yote hii ikiwa ni sehemu ya Kumfariji.

Najua wengi Wetu nasi tuna Mahitaji yetu na Maisha tuliyonayo sasa ni Magumu huku tukiwa tunahangaika huku na kule ili kuyaweka sawa lakini naamini kama kweli tuna Mioyo ya Kibinadamu ni dhahiri shahiri kuwa kwa Kilichomkuta huyu Binti Anna Zambi nadhani anatakiwa Kupata Msaada Kwanza kuliko Sisi ( Mimi na Wewe ) hasa kutokana na Mazingira yake Kiujumla na tukizingatia kuwa bado ni Binti kabisa anayehitaji Kuongozwa, Kusimamiwa na Kutiwa Moyo.

Mwisho kabisa natoa Pole zangu za dhati kwa huyu Binti Anna Zambi na Wanafamilia wake pamoja na wana Mkoa wa Tanga wote. Najua wengi wetu tumefiwa ila Kufiwa kwa huyu Binti Anna Zambi ni kwa aina yake na Mimi GENTAMYCINE naona amepata Pigo moja Kubwa sana hivyo anahitaji Kuombewa, Kupewa Moyo na Kusaidiwa kwa hali na Mali hadi nae aje Kuyafikia Malengo yake ili basi huko mbeleni aje kuwa na Faida kwa nchi (Taifa) na Watanzania wote Kiuwajibikaji.

Serikali ya Tanzania na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli msaidieni huyu Binti Anna Zambi mtabarikiwa sana. Pole sana Mwanangu Anna Zambi Mwenyezi Mungu atakupigania, utaishi na utakuja Kufanikiwa mno Maishani.
 
mkuu GENTAMYCINE habari yako! kwanza kabisa napenda kukupongeza kwa kuliona hili kwa namna hii!

Binafsi nimehuzunishwa sana na hili! naomba nisema ukweli mimi ni mgumu sana kutoa machozi lakini toka jana kila nikiangalia video za huyu binti machozi yananitoka sana! kwa kweli mungu ampe faraja sana, sidhani kama kuna mtu anatamani kukutwa na haya!

Nimesoma leo maeneo kadha wa kadha nimona Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameongea kidogo kuhusu hili na hatua ambazo yeye na na wizara yake wanaweza wakafanya "Tunashukuru kwa hili pia". Pia nimeona kuna baadhi ya watu wamechukua hatua zaidi akiwemo ZAMARADI MKETEMA, (kwa kweli mimi sio mshabiki sana wake lakini ninampongeza na kumshukuru sana kani) amejitoa sana na jana alifika mpaka kuonana na familia yake na kuongea kuhusu dhamira yake ya kumlea binti yule.

Pamoja na kwamba familia yake walisema watamlea lakini hakukata tamaa alienda mbali kwa kufungua akaunti ya banki ili wale wote walioguswa waweze kutoa chochote kitu kwa ajili ya huyu binti. Naomba niiweke hapa pia
1573987275090.png


Mwisho nami namuombea sana binti huyu mungu ampatie faraja sana hasa kipindi hiki kigumu!
 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ni baba yake mdogo marehemu Lingtone Zambi, hivyo huyu ni babu mdogo wa Anna Zambi, nitashangaa kama mtoto atapelekwa kulelewa na watu wengine.
 
gango2,

Akhsante Mkuu gango2 na tupo pamoja ila Maelezo yako yaliyojaa Hisia Kali na Huzuni kama nilizonazo Mimi yamezidi Kunifanya nitokwe na Machozi zaidi. Mwenyezi Mungu ampiganie mno huyu Mwanetu Anna Gabriel Zambi. Hata uwe Mgumu ( Bandidu ) vipi ila Kiubinadamu hili tukio ni lazima tu litakuliza na Kukufanya uwe na Huzuni.
 
Aendelee kuishi kwa ndugu zake,huku wasamalia wema wakiendelea kutoa misaada mbali mbali ya kiroho,kisaikolojia na uchumi kwa ujumla.
 
Ufafanuzi kidogo...

Pamoja na kwamba familia yake walisema watamlea lakini hakukata tamaa alienda mbali kwa kufungua akaunti ya banki ili wale wote walioguswa waweze kutoa chochote kitu kwa ajili ya huyu binti. Naomba niiweke hapa pia
 
Hiki tukio limegusa mioyo ya wengi.
Mungu aendelee kumpa faraja kubwa
Naamini watu waliojitolea watafanya hivyo na kwa utanzania wetu wa kushirikiana kwenye mambo Kama haya all will be well to her...she has become mdogo wa taifa zima.. shukrani kwa zamaradi aliyejitolea kwa vitendo zaidi na kufanikisha hili la account na mengine.
 
Back
Top Bottom