Vipaumbele vyangu nikiwa rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mbahili

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
260
469
Kuwa raisi sio jambo dogo/jepesi hata kidogo. Kongole kwa La mama anaeendelea kugongelea misumari kuhakikisha gurudumu halichomoki na tunakwenda mbele bila wasi.

Twende sasa....
Cha kwanza nikiwa Raisi nitakuwa mbabe.

Tupa kule ilani ya chama Changu, nitatengeneza ilani itakayohakikisha mpambanaji anaishi mlalaji anakufa..

1. Nitaachana na dhana nzima ya usocialist nitabeba ucapitalist, nitahakikisha nawafundisha wananchi yangu kusave muda na fedha.

2. Nitafuta mlundikano wa uongozi kv mkuu wa wilaya vs mkuu wa mkoa; wa kazi gani? Kwanini tulipe mishahara lukuki, hiyo mishahara nitakayo walipa bora nitoe ruzuku na mikopo rahisi kwa wapambanaji

3. Nitafuta dhana ya kimkoa, hatutakuwa na mikoa na mipaka ila mashariki, magharibi, kusini na mashariki plus kati, hii utatusaidia katika uongozi wetu na kupunguza gharama ya uongozi.

4. Nitafuta Kitu kinachoitwa Muungano kinguvu na kibabe. Si kufuta tu bali nitafuta pia sikukuu ya Muungano, nitapandisha hadhi zanzibari na kuwa na mwakilishi kama maeneo mengine ya bara, nitahakikisha wazanzibari wanapata maeneo bara na bara wapate zanzibari ndani ya miaka 20 zijazo hii idea ya ubara na uvisiwani ipotee.

5. Nitawafundisha watu wangu kazi za usalama kwamba polisi ni watumishi wao na si wao watumishi wa polisi, nitahakikisha rushwa inaogopeka, adhabu ya kunyongwa mpaka kufa kuwe kipimo cha mtoa rushwa na mdai rushwa.

6. Nitahakikisha bunge na mahakama vinakuwa vyombo vya kujitegemea. Endapo kuna shughuli ya bunge ifanywe na bunge ila visichanganywe

7. Nitaamka toka usingizini
 
Back
Top Bottom