Ombi kwa nyakati ngumu

Ombi kwa nyakati ngumu

Joined
Feb 28, 2022
Posts
78
Reaction score
73
Zungumza na Mungu usiku wa leo mwambie

"Mungu nimekuletea kilakitu kilicho ndani ya moyo wangu, wewe unayatambua mawazo yangu, hofu na tumaini langu, lakini nahitaji niyakabidhi kwako. Uzito wa hofu niliyonayo Kuna wakati unanielemea, na ninaomba uniongoze katika wakati ambao siioni njia sahihi, ninaomba uniimarishe katika udhaifu wangu, na unipe amani kwa wakati ninaotawaliwa na hofu, ninajua Wewe ni chanzo cha amani ya kweli, kwa hiyo ninakuamini ingawa bado nimesongwa na udhaifu na mashaka.

Ninakushukuru kwa baraka ulizonipatia, hata kwa zile nisizoziona, ninawaleta kwako ndugu zangu, changamoto zangu, na ndoto nilizobeba. Najua unaniona na kunisikia; hata nisipokuwa na maneno yanayotosha kuelezea. Nisaidie niweze kuelewa mipango yako- ingawa siwezi kuiona Kwa macho. Ninakabidhi maisha yangu kwako, natambua Upo pamoja nami, niongoze, siwezi kuwa mkiwa chini ya uwepo wako,
Amen"...

Ikiwa ombi hili imekupa mtazamo mpya na limekuchochea kuanza kuchukua hatua, ningependa kusikia kutoka kwako.

WhatsApp: 0785332053
 
Back
Top Bottom