Wadau;
Kulingana na thamani ya kile kilichotokea na kuwafumbua macho na akili za maelfu ya makundi mbalimbali ya wananchi kutokana ya Ukweli na ufahamu waliopata baada ya Mdahalo ulioandaliwa na Nyerere Foundation na kurushwa na ITV na Radio One tarehe 04/08/2014. Wengi wameomba ITV iandae Kipindi Maalum kurudia Mdahalo huo ambao umezidisha kujiamini kwa wananchi, ufahamu mkubwa wa maudhui ktk Rasimu ya 2, na watu wengi wanakiri waziwazi kuwa ITV na Radio One ndio mkombozi wa habari aliyebaki kwa jamii ya Tanzania kinyume na TBC1 (na Kituo kingine walichosema cha Mwanza, Star TV) ambavyo wanasema vimepoteza hadhi sana na kuwa vimedakwa na CCM kinyume taaluma zao). Watu wamelalamika sana kuwa TBC1 mbali na kuendeshwa kwa kodi za wananchi waliojaa umaskini, ndiyo ya kwanza kuwakandamiza kupita kiasi kwa kwa maslahi ya kundi la wachache na hivyo kutowapa habari za ukweli, taarifa sahihi na za wazi na kuwaua kufikra kwa faida ya watawala wa muda mfupi.
My take:
IPP MEDIA na vyombo vyake vya Habari (TV, Radio na Magazeti) wajitambue kuwa Umma sasa umewakubali kwa umakini wao na uthabiti wa kusimamia maslahi ya Taifa na elimu kwa wananchi wake na hivyo wasiogope vitisho vyovyote vya watawala wachache ambao wataondoka madarakani 'kesho', huku taifa likiendelea kuwepo daima.
Ipp Media wasirudi nyuma
Nawasilisha kwenu wachangiaji hapa kuunga mkono !