mmmhhh...!!! mungu apishe mbali. Nakumbuka miaka za zamani kwenye makutano ya barabara ya Zanaki na Libya, pale kwenye masoko ya wahindi, kuna mwendawazimu alimvamia mama wa watu wa makamu, akambaka, nasikia mume wake alipopata habari alimuacha mkewe, eti haku imagine kuishi nae tena baada ya aibu hiyo. Tamwa nadhani au NGO inayofanana na hiyo kwa wakati huo, walitetea sana hiyo ndoa lakini baba alikataa kata kurudiana na mkewe.
Mungu atunusuru kwa kweli kwa majanga ya namna hii.
Mwendawazimu alibebwa akapelekwa Muhimbili, nadhani walimmaliza kwa sindano ikawa mwisho wake maana alikua tatizo mjini na ndugu zake ni kama walimtelekeza fulani.