Maamuzi yanakuwa mepesi iwapo nchi au taasisi inaendeshwa kwa kufuata misingi ya sheria na kanuni walizojiwekea wenyewe. Lakini hilo linaonekana kufutika kutokana na kauli yako mwenyewe: "Kuna watu wazito nyuma ya akina Halima na wenzake."
Kama tunavyoshuhudia uvunjifu mkubwa wa katiba na sheria hivi sasa, kwa kauli yako, tunaongozwa kwa matakwa ya watu wazito wasiojali sheria tulizojiwekea wenyewe. Ni kweli hiyo ndiyo hali inayoendelea kwa sasa. Mtizamo wa wakubwa (kwa maslahi yao binafsi) ndio katiba, sheria, kanuni ya nchi, taasisi, n.k.
Nchi imetumbukia ktk pori kubwa kwenye giza totoro, alafu viongozi wamevaa miwani ya jua, huku wakiamini hisia zao zitatutoa porini bila ramani mkononi. Jamaani twafaaaa!