Ole Sendeka: Hali ya umaskini imeongezeka Mirerani, amuomba Waziri Mkuu biashara yote ya madini ya Tanzanite iishie Mirerani

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Mbunge wa Simanjiro, Ole Sendeka ametoa Ombi kwa waziri Mkuu alipokuwa mkoa wa Manyara kuzindua kituo cha Tanzanite Magufuli, kwanza ameomba ukaguzi wa Staha kwa watu wake bila kuathiri mapato ya Serikali mgodi wa Mirerani.

Pia ameomba kuongezwa chumba kimoja kwa ajili ya ugaguzi wa wanawake kwani wanaume wanavyo vitatu na wanawake kimoja pekee.

Ole Sendeka: Mheshimiwa Waziri mkuu, hali ya umaskini imeongezeka Mirerani, mzunguko wa fedha haupo. Dhamira ya mheshimiwa Rais ya wananchi kunufaika na rasilimali za nchi na Tanzanite kupewa hadhi yake kwa kudhibitiwa ili iwanufaishe watanzania kwa ajira, uongezaji wa thamani na usafirishaji wa nje ikiwa na utambulisho wa Tanzania, nina ombi kwako, ikupendeze haya nitakayoyasema

Tunalo geti hili na kituo cha Magufuli, tunaomba badala ya Mirerani kutumika kama uchochoro kwamba madini yanatoka hapa, yakishatathminiwa hapa yanakwenda Arusha, Madini yote naomba biashara yake imalizike hapa Mirerani, soko Mirerani na uongezaji wa thamani
 
Umasikini umewashinda CCM na serikali yao zaidi ya miaka sitini sasa toka tupate uhuru, huyo Sendeka anapoteza muda na hilo ombi lake, sasa hivi chama dola wanachoweza ni kuwatisha wananchi tu wasidai Katiba Mpya.
 
Umasikini umewashinda CCM na serikali yao zaidi ya miaka sitini sasa toka tupate uhuru, huyo Sendeka anapoteza muda na hilo ombi lake, sasa hivi chama dola wanachoweza ni kuwatisha wananchi tu wasidai Katiba Mpya.
Waisema tukichagua wabunge wa ccm tutapaya maendeleo 😅😅
 
Ujenzi wa ukuta ulikuwa uamuzi mzuri. Kuanzia hapo yahitaji usimamizi mzuri na ubunifu
 
Sendeka akili zake ziko kwenye tumboni,mnunuzi akatie mawe mererani ambapo hakuna mtu hata mmoja anakatia mawe huko...kukata mawe kunahitaji mashine,wataalam n usalama wa mawe yako.
 
Back
Top Bottom