Ole Sabaya: Rais Samia atatuvusha

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
4,246
2,000
Mkuu wa wilaya ya Hai Ole Lengai Sabaya wakati akihojiwa kwenye kipindi cha 360 cha Clouds Fm amewajibu wanaosema kuwa enzi zake zimekwisha baada ya kifo cha hayati rais Magufuli.

Sabaya amesema wanaosema zama zake zimekwisha wanapoteza muda kwa sababu wakati wa utawala wa rais Magufuli alikuwa anaripoti kwa rais, makamu wa rais (Samia) waziri mkuu, na wakuu wa mikoa, anasema hao ndiyo waliomtuma kuitoa wilaya ya hai kutoka ya 192 kwenye ulipaji kodi hadi sasa hivi iko nafasi ya 4. Sabaya amesema wilaya ya Hai ikiongozwa na Mbowe ilikuwa hub ya wakwepa kodi, wezi ,wazurumaji ,na wasaliti nchini.

Ole Sabaya amesema kitendo cha Mama Samia kusifiwa na hayati Magufuli kwenye mkutano CCM Dodoma mwaka 2020 kinaonyesha alikuwa anamwamini sana na alitaka kama yeye hayupo basi sisi watanzania tumwamini rais Samia kwani atatuvusha.

Pia amesema uzuri ni kwamba hata rais Samia ameanza vizuri baada ya kukataa hadharani kumsaliti Magufuli pale alipowajibu wahuni Lisu, Heche, Msigwa ,Mbowe, Nape, Makamba na bavichaa kwa ujumla kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja.
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,889
2,000
Anafaa sana huyu kijana. Kutoka 192 hadi ya 4. Ni zaidi ya maendeleo
Yeye ni mkusanya kodi au ni TRA?

Pia kuonyesha upimbi na ujinga ulio mjaa Dc ata toaje takwimu wakati Rc yuko ndie kiongozi wa mkoa?

Bado ana lalamika picha ni ya 2018. Na hii dharau ya leo ni ya mwaka gani?? Lazima kuwe na chain of organisation. Uta kuta hata kuwepo clouds Mkuu wake wa Mkoa hana taarifa.
 

tzkwanza

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,577
2,000
Kama mama Samia angekuwa kiongozi makini wa kwanza kumfukuza kazi alikuwa ni huyu Sabaya.

Huyu dogo ametumia mwamvuli wa TISS kutesa na kunyang'anya pesa kwa watu wengi sana.

Bila haki taifa haliwezi kuinuka na hapa huyu kijana anapiga kampeni awe mkuu wa mkoa.

Yajayo yanahuzunisha.
 

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,292
2,000
Yeye ni mkusanya kodi au ni TRA?
Pia kuonyesha upimbi na ujinga ulio mjaa Dc ata toaje takwimu wakati Rc yuko ndie kiongozi wa mkoa?...
Sabaya amekuwa kero sio kwa wananchi tu bali hata kwa Mkuu wake wa Mkoa kiasi kwamba hata Dr. Mpango alipokuwa Waziri wa fedha aliwahi kutumwa na mwendazake kwenda Mkoa wa Kilimajaro ili kusuluhisha matatizo yaliyoleta kutoelewana kwa Viongozi wa huo Mkoa kinara wake akiwa huyo Dc wa Hai!! Huyu haendani kabisa na dhana ya utawala bora.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom