Ole Sabaya na wenzake wakutwa na kesi ya kujibu kwenye mashtaka ya Uhujumu Uchumi

Huyu anakula mvua ya 30 tena.
Hivi wafungwa wa namna hii huwa wana nafasi ya msamaha wa raisi huko mbele ya safari? Isije kuwa mtu anakula mvua 30 baada ya miaka 7 anarudi uraiani kupunga upepo
 
Sabaya alipewa madaraka yakamlevya. Sabaya alijiona yy ndio kila kitu, hakuna wa kuzungumza mahali alipo. Akatengeneza tengeneza figisu za kubambikiza watu kesi na kuwadhulumu.

Leo Sabaya hana wa kumtetea tena wala kumpa kichwa. Yupo yeye sabaya na nafsi yake. Kila anapoangalia kuna kiza kinenene. Sometimes anajutia kwa nn alikubali kuwa mkuu wa wilaya.

Ni matatizo aliyosababisha mwenyewe yanampata sasa. Hatuyafurahii lakini tunafurahi kwamba anaenda kujifunza na atafunza wengine.

Nenda sabaya, ukiwa huko tafakari uliyofanya na ikiwezekana kiri hadharani na kuwaomba msamaha uliowadhulumu na kuwatesa.
Umesahau jamaa hata kabla hajala shavu si alikuwa na kimeo cha TISS?
 
Hivi wafungwa wa namna hii huwa wana nafasi ya msamaha wa raisi huko mbele ya safari? Isije kuwa mtu anakula mvua 30 baada ya miaka 7 anarudi uraiani kupunga upepo
Huyu inabidi aende huko Kigoma akalime michikichi au maharage
 
Tumeshaelewa delilah ndio kitendo chake cha mwanzo kutuonyesha hakua kitu kimoja na jpm. Kwa sasa tunaelewa yuko upande gani nasi tuko upande upi. Rip jpm
Kwamba sabaya anaonewa au?

Sabaya anastahili kukinywea kikombe hiki ,na nashukuru mungu kwa kumuongoza rais wetu ili kuruhusu uchunguzi wa sabaya,mungu amrehemu rais wetu SSH .

Utawala wa sheria ni muhimu Sana,na zaidi Kuna wengine twajifunza toka kwake.
 
Kwamba sabaya anaonewa au?

Sabaya anastahili kukinywea kikombe hiki ,na nashukuru mungu kwa kumuongoza rais wetu ili kuruhusu uchunguzi wa sabaya,mungu amrehemu rais wetu SSH .

Utawala wa sheria ni muhimu Sana,na zaidi Kuna wengine twajifunza toka kwake.
Sabaya, bashite,gambo,muro, kihongosi, chalamila,mnyeti hawana sifa za kuwa viongozi,
 
Hili tatizo la Sabaya siyo la kufurahia hata kidogo.wananchi wanatakiwa tuungane tuweze kupata katiba mpya.kwani hivi vyeo vya kupewa havina maana kazi ni kujipendekeza kwa aliye kuteuwa.mkuu wa wilaya ni mkuu wa usalama ndani wilaya. Jeshi lote liko mikononi mwake.je ni nani wa kumpeleleza akifanya uhalifu?hata hao maaskari wa hai wana kesi za kujibu je uhalifu wote uliokuwa ukifanyika walikuwa wapi?katiba mpya sasa itaokoa taifa.wateule wa raisi ni wengi zaidi ya wapigiwa kura na wananchi.poleni sana wadanganyika
 
Kashahukumiwa miaka 30,kesi gani tena za kipuuzi km hizo zinaendelea?si atumikie kifungo tu.
Huu ni upumbavu kukaa tunajadili upuuzi wa mtu aliyefungwa.
Kashafungwa otherwise mumuachie mumuhukumu tena.
Huu ni uonevu.
Nchi ni yetu sote,
Hamna binadamu yuko sawa mnamtesa mtu kijingajinga tu.
Kama Sabaya alikosea si anaonywa na adhabu aliyopata inatosha.
Nyie watu mnaishi kama wanyama aisee.
 
Back
Top Bottom