Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,815
- 11,992
Mkuu wa Wilaya ya Hai Mh. Lengai Ole Sabaya amemtaka Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Aikael Mbowe kuanzisha maridhiano ndani ya chama chake cha chadema kabla ya kutoka nje kulalamika.
Ole Sabaya amedai mbunge huyo anapaswa kutafuta maridhiano ndani ya chama chake kwanza dhidi ya shutuma mbalimbali ikiwemo za matumizi binafsi ya fedha zaidi ya milioni 600 za Chadema alizonunulia matrekta na kuyapeleka Ifakara kufanya biashara zake binafsi za kilimo lakini akiziweka katika matumizi ya kiofisi ndani ya chama hicho.
Ole sabaya pia amemtaka Mbowe atafute maridhiano ya zinapoenda ruzuku za chama hicho ambazo zinaoneka hakuna kazi zinafanya ndani ya chama hicho.
Ole Sabaya pia amemtaka Mbowe kutafuta maridhiano na wagombea wa nafasi za ubunge ndani ya chama hicho wanaolalamikia ada ya milioni 6 kwa ajili ya uchukuaji fomu ya ugombea.
Pia DC huyo amemshangaa Mbowe kulilia tume huru nyingine ilihali yuko mbungeni kwa tume hii huru iliomfikisha huko awamu hii.
Ole Sabaya amemtaka Mbowe kwenda Hai kutafuta suluhu na wananchi waliompigia kura ambao hajawatembelea muda mrefu na sio kutafuta suluhu na Rais Magufuli.
Ole Sabaya ameyasema hayo wakati akigawa pikipiki kwa makatibu wa CCM wa kata 17 zenye thamani ya sh mil 39.1 za wilaya hiyo.
Ili kuwasaidia katika ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na kusaidia shuguli mbalimbali za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi October.
Sent using Jamii Forums mobile app