Ole Sabaya: Mbowe, nyumba inawaka moto na maridhiano yaanzie ndani ya chama chako

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Mkuu wa Wilaya ya Hai Mh. Lengai Ole Sabaya amemtaka Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Aikael Mbowe kuanzisha maridhiano ndani ya chama chake cha chadema kabla ya kutoka nje kulalamika.

Ole Sabaya amedai mbunge huyo anapaswa kutafuta maridhiano ndani ya chama chake kwanza dhidi ya shutuma mbalimbali ikiwemo za matumizi binafsi ya fedha zaidi ya milioni 600 za Chadema alizonunulia matrekta na kuyapeleka Ifakara kufanya biashara zake binafsi za kilimo lakini akiziweka katika matumizi ya kiofisi ndani ya chama hicho.

Ole sabaya pia amemtaka Mbowe atafute maridhiano ya zinapoenda ruzuku za chama hicho ambazo zinaoneka hakuna kazi zinafanya ndani ya chama hicho.

Ole Sabaya pia amemtaka Mbowe kutafuta maridhiano na wagombea wa nafasi za ubunge ndani ya chama hicho wanaolalamikia ada ya milioni 6 kwa ajili ya uchukuaji fomu ya ugombea.

Pia DC huyo amemshangaa Mbowe kulilia tume huru nyingine ilihali yuko mbungeni kwa tume hii huru iliomfikisha huko awamu hii.

Ole Sabaya amemtaka Mbowe kwenda Hai kutafuta suluhu na wananchi waliompigia kura ambao hajawatembelea muda mrefu na sio kutafuta suluhu na Rais Magufuli.

Ole Sabaya ameyasema hayo wakati akigawa pikipiki kwa makatibu wa CCM wa kata 17 zenye thamani ya sh mil 39.1 za wilaya hiyo.

Ili kuwasaidia katika ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na kusaidia shuguli mbalimbali za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi October.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani huyo Ole Sabaya huwa anahudhuria vikao vya Kamati Kuu ya Chadema?

Kumbe anajua taifa linahitaji maridhiano kutokana na mfano wa matendo yake ya hovyo anayomfanyia Mbowe huko Hai.

Vipi alituambia wafanyabiashara wanahujumu miundombinu ya reli, mkuu wa polisi akamfundisha kufanya kazi sio kupiga umbeya tu.

Bado haoni aibu kuendelea kubwabwaja hovyo kwenye jamii iliyostaarabika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wa Kilimanjaro wananeemeka sana kwa siasa za kijinga za ccm. Hapo CCM imegawa pikipiki kwa makatibu wote wa kata wa ccm wilaya ya Hai ila utashangaa mwenyekiti wa ccm wa jimbo la Chato anakotoka Magufuli hajawahi kupewa baiskeli na ccm.
 
Hilo la fomu ya ubunge kuuzwa sh milioni 6 ndio limenishangaza!
Mashine ya umbea.
IMG-20200211-WA0000.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Wilaya ya Hai Mh. Lengai Ole Sabaya amemtaka Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Aikael Mbowe kuanzisha maridhiano ndani ya chama chake cha chadema kabla ya kutoka nje kulalamika.

Ole Sabaya amedai mbunge huyo anapaswa kutafuta maridhiano ndani ya chama chake kwanza dhidi ya shutuma mbalimbali ikiwemo za matumizi binafsi ya fedha zaidi ya milioni 600 za Chadema alizonunulia matrekta na kuyapeleka Ifakara kufanya biashara zake binafsi za kilimo lakini akiziweka katika matumizi ya kiofisi ndani ya chama hicho.

Ole sabaya pia amemtaka Mbowe atafute maridhiano ya zinapoenda ruzuku za chama hicho ambazo zinaoneka hakuna kazi zinafanya ndani ya chama hicho.

Ole Sabaya pia amemtaka Mbowe kutafuta maridhiano na wagombea wa nafasi za ubunge ndani ya chama hicho wanaolalamikia ada ya milioni 6 kwa ajili ya uchukuaji fomu ya ugombea.

Pia DC huyo amemshangaa Mbowe kulilia tume huru nyingine ilihali yuko mbungeni kwa tume hii huru iliomfikisha huko awamu hii.

Ole Sabaya amemtaka Mbowe kwenda Hai kutafuta suluhu na wananchi waliompigia kura ambao hajawatembelea muda mrefu na sio kutafuta suluhu na Rais Magufuli.

Ole Sabaya ameyasema hayo wakati akigawa pikipiki kwa makatibu wa CCM wa kata 17 zenye thamani ya sh mil 39.1 za wilaya hiyo.

Ili kuwasaidia katika ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na kusaidia shuguli mbalimbali za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi October.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anataka kusema Serikali inayomiliki Vyombo Vya uchunguzi vimeshindwa kumchukulia Mbowe hatua kwa tuhuma zote hizo?Mtu anatumia ruzuku ambayo ni kodi ya toka kwa wananchi halafu Vyombo vinavyohusika vipo kimya tu?Basi Serikali hiyo haitufai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Wilaya ya Hai Mh. Lengai Ole Sabaya amemtaka Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Aikael Mbowe kuanzisha maridhiano ndani ya chama chake cha chadema kabla ya kutoka nje kulalamika.

Ole Sabaya amedai mbunge huyo anapaswa kutafuta maridhiano ndani ya chama chake kwanza dhidi ya shutuma mbalimbali ikiwemo za matumizi binafsi ya fedha zaidi ya milioni 600 za Chadema alizonunulia matrekta na kuyapeleka Ifakara kufanya biashara zake binafsi za kilimo lakini akiziweka katika matumizi ya kiofisi ndani ya chama hicho.

Ole sabaya pia amemtaka Mbowe atafute maridhiano ya zinapoenda ruzuku za chama hicho ambazo zinaoneka hakuna kazi zinafanya ndani ya chama hicho.

Ole Sabaya pia amemtaka Mbowe kutafuta maridhiano na wagombea wa nafasi za ubunge ndani ya chama hicho wanaolalamikia ada ya milioni 6 kwa ajili ya uchukuaji fomu ya ugombea.

Pia DC huyo amemshangaa Mbowe kulilia tume huru nyingine ilihali yuko mbungeni kwa tume hii huru iliomfikisha huko awamu hii.

Ole Sabaya amemtaka Mbowe kwenda Hai kutafuta suluhu na wananchi waliompigia kura ambao hajawatembelea muda mrefu na sio kutafuta suluhu na Rais Magufuli.

Ole Sabaya ameyasema hayo wakati akigawa pikipiki kwa makatibu wa CCM wa kata 17 zenye thamani ya sh mil 39.1 za wilaya hiyo.

Ili kuwasaidia katika ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na kusaidia shuguli mbalimbali za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi October.

Sent using Jamii Forums mobile app

Webmaster topic za Sabaya ni za kujitangaza mwenyewe hana tija. Na yeye ndiyo mwandishi hapa anajifanya ni watu wengine. Futa hizi topic zake za kijinga.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom