Okwa: Baada ya Zoran kuondoka mambo yalibadilika

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
16,410
25,350
“Wakati Zoran akiwa Simba ilikuwa unacheza kulingana na ulivyoperfom kwenye mazoezi, lakini baada ya kuondoka ikawa kama Kuna watu wanaleta list ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na hawa wasicheze bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi,” Aliyekuwa mchezaji wa Simba Sc, Nelson Okwa.

NB: Kwa hali hii tutaishia tu Robo fainali

Source: Wasafi FM

1687775111164.jpg
 
Uto wenye akili ni wawili tu.

Yaani kasema "ikawa kama..."

Kwa ufupi ni kuwa maelezo yamejaa mashaka na yasiyo na chembe ya hakika. Hana uthibitisho wowote kama kinafanyika ama. Uthibitisho ungekuwa umenyooka. Kwamba 'Try again ndiye anapanga kikosi'.

Alafu aina gani ya mchezaji anasema? Ambaye alishindwa kudhihirisha uwezo wake. Sawa wanapangiwa na Viongozi.

Tulimpeleka kwa mkopo kwingine, mbona alishindwa ku-outshine? Au viongozi wa Simba wanaenda mpaka huko Ihefu?

Tumia huo Ubongo vizuri kuliko kuufanya mzigo juu ya mabega.
 
Ni kweli haipaswi kuingilia majukumu ya kocha hilo tunalifahamu na tunaliheshimu.

Lakini lazima tukubali kuwa wewe kuwa kocha haina maana wasio kuwa makocha hawana vision ya kujua mpira na kumtambua mchezaji mwenye uwezo.

Pia ikumbukwe kuwa huyo alikuwa ni kocha mgeni kwenye timu ambayo aliikuta ina wachezaji wengine.

Hivyo kuja na wachezaji wake sio kitu kibaya.

Ubaya ni pale unapowapa nafasi hao wachezaji wako na uwanjani hawatupi ile performance ambayo tulitarajia iwe juu zaidi ya hawa wenyeji ambao Kocha huwapangi.

Badala yake tunaona hao wachezaji aliokuja nao Kocha wanacheza under performance ukilinganisha na wachezaji ambao wako benchi.

Sasa kwa hatua hiyo tuendelee kumuamini kocha azidi kuchezesha wachezaji wake ambao hawana mchango wowote ndani ya timu na timu izidi kupoteza alama kwa kuhofia tukimpa ushauri wa kuwapanga wachezaji wengine ambao number zinaonesha wazi kuwa ni bora kuliko hao anaowaamini yeye, kuingilia majukumu ya kocha?
 
Watu wanabidi wajue kuwa hakuna mtu anayeweza kuingilia majukumu ya kocha ikiwa kikosi chake kinapata matokeo mazuri.

Na sina maana kupata matokeo mabaya ndio tiketi ya kupata uhalali wa kumpangia Kocha.

Bali performance mbovu ya wachezaji.

Unajua kwanini Gongowazi walikuwa na confidence ya kusema no Feisali no problem?

Ni kwasababu walikuwa wanapata matokeo mazuri yaliyofanya wasione pengo la Feisali , ila isingewezekana kwa namna yeyote ile wapate matokeo mabovu under poor performance then wasipige kelele kuhusu Feisali.
 
Aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Nelson Okwa amefunguka juu yaliyokuwa yakijiri klabuni hapo ambapo amefichua kuwa wachezaji hawachezeshwi kulingana na utendaji wao mazoezini bali ‘yupo mtu ambaye huja na orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na wasiotakiwa kucheza bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi.’Akizungumza na kituo cha habari cha G&T Online TV, Okwa amesema, "Wakati Kocha Zoran akiwa Simba ilikuwa mchezaji unacheza kulingana na ulivyo-perfom kwenye mazoezi, lakini baada ya kuondoka ikawa kama Kuna watu wanaleta Orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na hawa wasicheze bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi"
✍️
JE haya yana ukweli au maneno ya mkosaji?

252BC958-0D43-4BDA-A85B-CC5F8F8ECAA2.jpeg
 
Aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Nelson Okwa amefunguka juu yaliyokuwa yakijiri klabuni hapo ambapo amefichua kuwa wachezaji hawachezeshwi kulingana na utendaji wao mazoezini bali ‘yupo mtu ambaye huja na orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na wasiotakiwa kucheza bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi.’

Akizungumza na kituo cha habari cha G&T Online TV, Okwa amesema, "Wakati Kocha Zoran akiwa Simba ilikuwa mchezaji unacheza kulingana na ulivyo-perfom kwenye mazoezi, lakini baada ya kuondoka ikawa kama Kuna watu wanaleta Orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na hawa wasicheze bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi"

JE haya yana ukweli au maneno ya mkosaji?

#KitengeSports
FB_IMG_1687778965674.jpg
 
Mlete na thread ya timu lenu kufungiwa baada ya kushinda kumlipa kocha mwenye akili aliewahi kufundisha utopoloni
 
Kama ni kweli hiyo siyo nzuri kabisa, lakini mchezaji wa kubaniwa atakuwa okwa? Like seriously, okwa amuweke benchi chama?😀😀
 
Back
Top Bottom