Ujio wa kocha mpya Simba SC hauna tofauti na kupika mchele wenye chuya

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,288
12,786
NALIA NGWENA sitorudi nyuma kuandika ukweli japokua ni jipu chungu kwenye mioyo ya wanasimba.

Ukweli mtupu huu Kama utafanyiwa kazi Basi utaleta furaha na kukata kiu ya mtu alietoka jangwani baada ya kupigwa jua Kali.

Mpaka Sasa Simba sc kwa misimu miwili hii Ina makombe mawili tu kabatini yaani kombe la MAPINDUZI na NGAO YA JAMII na ukipiga tathimin hayo makombe siyo lolote siyo chochote.

Simba sc imeleta kocha mpya (BENCHKHA) lakini swali la kujiuliza je Simba sc wanabadili makocha je wao pia Wanaweza kusajili wachezaji wenye hadhi Kama makocha wanavyotaka?

Jibu hapana! Ukiangalia kuletwa kwa kocha Robertinho hakuna wachezaji wazuri walioletwa ili kwenda na Falsafa za kocha Robertinho Ila tu kilichofanyika ni ujanja ujanja na kununua wachezaji wa mafungu (Bei Chee).

Kwani Nani aliyemleta sawadogo, Nelson Okwa na wachezaji wengine walioonekana kabisa hawana hadhi ya kucheza Simba sc?

Hapo tunapata picha kuwa Kocha anapendekeza mchezaji huyu lakini viongozi (wazee wa ten percent) wanaleta wachezaji wanao wataka wao.

Ameletwa kocha mpya BENCHKHA kwa takwimu ni kocha mzuri lakini ukija kwenye timu aliyopewa hakuna wachezaji wazuri na timu ikifanya vibaya lazima atafukuzwa tu na atatafutwa kocha mwengine.

NALIA NGWENA nafungua ubongo wa msomaji kuwa mchele ni ngumu kupikwa na chuya Ina maana ujio wa kocha mpya akikabidhiwa timu yenye wachezaji Kama Saidoo ntibazonkiza, John Bocco, Chama n.k Basi itakua ni kazi ya kutwanga maji kwenye kinu.

Maoni Yangu: Simba sc isipoondoa wazee katika kikosi hata aje Morinho au Gadiola nao watafukwa tu baada ya mechi tatu.
1700984935094.jpg
 
UONGOZI wa Simba unachapia nyufa badala ya KUJENGA ukuta, na hakika safari hii NYUMBA yenyewe imegoma na mafuriko ni mazito kiasi kwamba wakiendelea kukaza SHINGO basi tujiandae na mfuatano wa majanga...

Kufanikiwa kunahitaji kijikana kwakweli, hili linalotokea leo lilikuwa lazima lifike kwasababu klabu zetu zipo kwa ajili ya leo... Simba iko na uwanja Bunju miaka 10 inaenda lakini mpaka muda hakuna hata mtoto mmoja anayetokea pembeni ya uwanja hata wa kujua kudaka na tunaoyeshana Ndoto za mafanikio Afrika...

Haya kutengeneza cha kwetu tumeshindwa, sasa huko kununua nako tunabebana na sagula sagula za mwisho maana hata mtumba nao una grade zake, halafu tukishakusanyana na hayo magalasa tunayapamba kwenye magazeti ili kuhalalisha udhalimu wetu, halafu bila aibu TAJIRI tunamdanganya kuwa tumetumia Bilioni 3 kusajili 🤣🤣🤣, lakini ukichukua kalkuleta na peni Kila ukipiga hesabu huziona hizo Bil 3 zimeishia kwa nani?? 😂😂😂 Hapo MHINDI tushampiga kwa kumuuzia JUMBA LA UDONGO LILOCHAPWA PLASTA ambalo soon litavimba tu...

Na Sasa ndo limeanza kuvimba 🤣🤣🤣 maana wakati tunamwongezea MHINDI sifuri kwenye hesabu tunasahau kuwa mwisho wa siku yooote yanaishia uwanjani,,,, hapo ndo tunabaki na mazoea kuwa kwa "MKAPA HATOKI MTU" 😂😂😂.... huku chini ya VITI tunacheka tu 😂😂😂 tunasubiria dirisha dogo....
 
Kiungwana kabisaa na kimichezo kuna Viongozi(wale walio mleta Manzoki wakati wa uchaguzi) wangetakiwa hadi muda huu wawe wamekabidhi ofisi kwa faida ya Simba.
Lakini ajabu bado wanashupaza shingo.
Kwanini nasema viongozi kwasababu ndiyo wahusika katika usajili kwa wachezaji na makocha
 
Kiungwana kabisaa na kimichezo kuna Viongozi(wale walio mleta Manzoki wakati wa uchaguzi) wangetakiwa hadi muda huu wawe wamekabidhi ofisi kwa faida ya Simba.
Lakini ajabu bado wanashupaza shingo.
Kwanini nasema viongozi kwasababu ndiyo wahusika katika usajili kwa wachezaji na makocha
Tuliahidi kumleta sio kumsajili.

Tulimleta hatukumleta? Tena mbele ya mkutano Mkuu na microphone akapewa.
 
NALIA NGWENA sitorudi nyuma kuandika ukweli japokua ni jipu chungu kwenye mioyo ya wanasimba.

takwimu ni kocha mzuri lakini ukija kwenye timu aliyopewa hakuna wachezaji wazuri na timu ikifanya vibaya lazima atafukuzwa tu na atatafutwa kocha mwengine.

NALIA NGWENA nafungua ubongo wa msomaji kuwa mchele ni ngumu kupikwa na chuya Ina maana ujio wa kocha mpya akikabidhiwa timu yenye wachezaji Kama Saidoo ntibazonkiza, John Bocco, Chama n.k Basi itakua ni kazi ya kutwanga maji kwenye kinu.

Maoni Yangu: Simba sc isipoondoa wazee katika kikosi hata aje Morinho au Gadiola nao watafukwa tu baada ya mechi tatu.View attachment 2825495
Ni kweli ila kuelekea dirisha dogo faida mara 9999999999999999999999999999999999%
 
Back
Top Bottom