OILCOM Tabata Segerea mmezidi jamani!

OILCOM Tabata Segerea mmezidi jamani!

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
579
Reaction score
887
WanaJF nashangaa jana nimeweka mafuta ya Tsh elfu ishirini kwenye hii sheli sijui walinijazia hewa,gari ndogo ya CC 2000 sijatembea hata Km 1 taa inawaka ikabidi niingie sheli tena kuongeza mafuta,naomba EWURA na Mamlaka ya Vipimo wafanye kazi yao jamani.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
CC 2000 si gari dogo kama unavyosema, pia 20000 ulipata chini ya lita kumi, so taa ya warning kuwaka ilikuwa sahihi
 
Ungerudi ndugu. Ni kweli pale ni wezi mnoooo.
Wameshanifanyia mara mbili.
Mara ya kwanza nilipotezea kama wewe.
Mara ya pili nikaenda nikawaambia kabisa wasinifanyie usanii, wakaleta sanaa. Nilifika hadi baracuda....niligeuza mbona na wanafanyaga kusudi
 
Tatizo wewe unaenda kuweka mafuta kisha unawafungulia tanki unabaki umeketi na kustarehe kwenye gari kwanini wasikulize? Mimi nikfiungua kabla sijamwambia weka mafuta ya bei fulani ninakuwa nimeshatelemka. Naangalia meter reading hadi mwisho. Chezea wajaza mafuta wewe, NI LAZIMA UKATWE KIDZAINI FULANI.
 
next time nikipita huko najimiminia wese mwenyeeewe
 
Kaka nimeogopa af kabla sijaweka mafuta taa ilikuwa haijawaka ila mafuta yalikuwa down naweka mafuta natembea hadi kwa bibi taa inawaka kucheki Gauge imekula kwangu ikabidi niingie Lake Oil nikaweka upya,nimewaogopa aisee!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
CC 2000 si gari dogo kama unavyosema, pia 20000 ulipata chini ya lita kumi, so taa ya warning kuwaka ilikuwa sahihi

Kaka kabla sijaweka taa ilikuwa haijawaka ila mafuta yalikuwa down nimeweka hata kama ni lita tisa nitembee chini ya Km 1 kweli taa iwake sii wizi huu?Mafuta ya elfu 20 kaka?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kaka kabla sijaweka taa ilikuwa haijawaka ila mafuta yalikuwa down nimeweka hata kama ni lita tisa nitembee chini ya Km 1 kweli taa iwake sii wizi huu?Mafuta ya elfu 20 kaka?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Huo ni wizi wa mchana kweupeeee
 
Tatizo wewe unaenda kuweka mafuta kisha unawafungulia tanki unabaki umeketi na kustarehe kwenye gari kwanini wasikulize? Mimi nikfiungua kabla sijamwambia weka mafuta ya bei fulani ninakuwa nimeshatelemka. Naangalia meter reading hadi mwisho. Chezea wajaza mafuta wewe, NI LAZIMA UKATWE KIDZAINI FULANI.

NAni kwakuambia mita yao huwa haisomi!! Pole !!
 
next time nikipita huko najimiminia wese mwenyeeewe

Ndo maana mimi huwa huwa siweki moja kwa moja kwenye tanki,natembea na kidumu cha LITA TANO,yanapitia humo kwanza ndo namiminia garini.haha haaaaa
 
hahaha umenipa wazo jingine wewe, ngoja nisake kidumu ila nikiwa na familia sifanyi maana wife atahisi niemanza kuwehuka. :smile-big:
 
WanaJF nashangaa jana nimeweka mafuta ya Tsh elfu ishirini kwenye hii sheli sijui walinijazia hewa,gari ndogo ya CC 2000 sijatembea hata Km 1 taa inawaka ikabidi niingie sheli tena kuongeza mafuta,naomba EWURA na Mamlaka ya Vipimo wafanye kazi yao jamani.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Hawawafikii wa PUMA ya Sinza kijiweni hawa ni balaaa ukiongozana na Boda boda tu lazima wakukate kidizaini , nimeshagombana nao zaidi ya mara Tatu . anaanza kukuwekea inasoma 5000,7000 au 10,000. jiulize kama unaweka ya 20,000 utakuwa umepunjwaje . siendi tena pale ikibidi kwenda nashuka kwenye gari .
 
Tembelea VICTORIA PETROL STATIONS....hutajuta!
Ni "petrol station" na si "sheli"
 
Tatizo wewe unaenda kuweka mafuta kisha unawafungulia tanki unabaki umeketi na kustarehe kwenye gari kwanini wasikulize? Mimi nikfiungua kabla sijamwambia weka mafuta ya bei fulani ninakuwa nimeshatelemka. Naangalia meter reading hadi mwisho. Chezea wajaza mafuta wewe, NI LAZIMA UKATWE KIDZAINI FULANI.

Ukweli ndio huo!

Shell kama sheli haina matatizo!Tatizo ni wafanyakazi wa hiyo shell.Na si kwamba ni wafanyakazi wa shell hiyo,ni shell nyingi hapa mjini wenye tabia ya namna hiyo!

Mie nilienda kuweka mafuta sheli moja ya pale Ubungo external nikampa 10000/- mdada aniwekee mafuta, nikamuacha aendelee kuniwekea.

Baadae nikasikia akigonga gari kwenye ubavu akimaanisha ameshamaliza kuweka!Nikamuuliza mbona amechukua muda mfupi kuweka mafuta?Akanambia ndiyo hivyo ameshaweka!!

Ikanibidi nishuke kuangalia kwenye mita ya sheli,nikakuta 5000/- kwenye sheli moja na nyingine 7000/-!Nikamuambia mbona mita inayosoma 10000/- siioni?Akanambia hizo ni gharama za mafuta ya pikipiki ambazo ameweka baada ya kuniwekea mimi!!!

Wakati kwa muda niliokaa pale ni ndoto kuwawekea wateja watatu!!

Nikajilaumu kwa kuwa mzembe kwa kutoshuka kwenye gari alipokuwa akiweka mafuta!

Nikawa nimeshaibiwa tayari!

Tahadhari:
Hakikisha unapoweka mafuta kwenye gari unashuka kabisa na kusogelea mita kuhakikisha kuwa kiasi cha mafuta unayoweka ni ya gharama uliyolipia!
 
Nikweli kabisa ewula inatakiwa wafuatilie
Hizi shell za hapa dar zote mtindo huo si kwa oil com pekeyake mtindo huo pia unafanywa na shell ya temeke mtongani gapco ukiweka mafuta ya elfu ishilini kama unakwenda mbagala haufiki. Mchezo huo huwa unakuwa hivi mfano mwenye piki piki akifika kuweka mafuta kama ya sh.3000 huwa ile pump huwa haifutwi kwahiyo unapo sogeza gari lako wakuwekee mafuta wanaendelea na ileile bili inayo soma sh.3000 sasa kama umeweka mafuta ya sh.10,000 ujue unapata mafuta ya sh.7000/:
 
Hapa hauhitaji EWURA wala Dawasco, unatakiwa wewe mwenyewe uwe makini. Ewura watatoka wapi huko Mlandizi? Wakati mwingine na sisi to play our party.
 
Tembelea VICTORIA PETROL STATIONS....hutajuta!
Ni "petrol station" na si "sheli"

Naona watu wengi wanawasifia sana hawa watu. Hongera zao. jamaa yangu mmoja aliniambia hata service za gari ziko poa sana hakuna uchakachuaji.
 
Mimi nikiwa nataka kuweka full tanki, itabidi nitembee na pipa kabisa, waweke kwenye pipa kisha nihamishie kwenye tanki la gari yangu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom