OILCOM Tabata Segerea mmezidi jamani!

OILCOM Tabata Segerea mmezidi jamani!

Mimi siangalii mita naangalia mkono akiweka hakuna kuachia ama kubonyeza mpaka yakatike. Yakikatika ndio nasoma mita. Nafanya hivyo kwa kumuonuesha kabisa kwamba namtazama kwa makini. Huwa wanaogopa sana.
 
Jipe pole mwenyewe. Mi nakaba hadi penalty hawaniwezi hao wezi wako.

Pale ambapo huo mpira hutokea kuna wakati usipokuwa makini jamaa anabonyeza na mita husoma haraka na ndo umeshaibiwa!! Urefu wa kamba!!!!
 
wakuu hawa jamaa naona kuna jinsi wanavyocheza na ile pampu ya kuwekea mafuta imenitokea mara mbili oil com ya kipawa na total yapale banana ,nimeweka mafuta ya 30,000 kutoka banana na natumia alteza kufika vingunguti taa inawaka na kulikuwa hakuna foleni na wakati anaweka nilikuwa naangalia kabisa
 
wakuu hawa jamaa naona kuna jinsi wanavyocheza na ile pampu ya kuwekea mafuta imenitokea mara mbili oil com ya kipawa na total yapale banana ,nimeweka mafuta ya 30,000 kutoka banana na natumia alteza kufika vingunguti taa inawaka na kulikuwa hakuna foleni na wakati anaweka nilikuwa naangalia kabisa

Alteza baadhi zinabugia mafuta hasa za four cylinder
 
Ukweli ndio huo!

Shell kama sheli haina matatizo!Tatizo ni wafanyakazi wa hiyo shell.Na si kwamba ni wafanyakazi wa shell hiyo,ni shell nyingi hapa mjini wenye tabia ya namna hiyo!

Mie nilienda kuweka mafuta sheli moja ya pale Ubungo external nikampa 10000/- mdada aniwekee mafuta, nikamuacha aendelee kuniwekea.

Baadae nikasikia akigonga gari kwenye ubavu akimaanisha ameshamaliza kuweka!Nikamuuliza mbona amechukua muda mfupi kuweka mafuta?Akanambia ndiyo hivyo ameshaweka!!

Ikanibidi nishuke kuangalia kwenye mita ya sheli,nikakuta 5000/- kwenye sheli moja na nyingine 7000/-!Nikamuambia mbona mita inayosoma 10000/- siioni?Akanambia hizo ni gharama za mafuta ya pikipiki ambazo ameweka baada ya kuniwekea mimi!!!

Wakati kwa muda niliokaa pale ni ndoto kuwawekea wateja watatu!!

Nikajilaumu kwa kuwa mzembe kwa kutoshuka kwenye gari alipokuwa akiweka mafuta!

Nikawa nimeshaibiwa tayari!

Tahadhari:
Hakikisha unapoweka mafuta kwenye gari unashuka kabisa na kusogelea mita kuhakikisha kuwa kiasi cha mafuta unayoweka ni ya gharama uliyolipia!
Shell ni kampuni la mafuta la kiitaliano, lilikuwa na vituo vingi vya mafuta nchini kiasi kwamba watu wakahisi vituo vya mafuta vinaitwa shell. Kwa sasa sijui kama wana tena vituo hapa nchini ila wanauza vilainishi.
 
yaani ile oilcom petrol station ni balaa, nakushauri kaweke mafuta lake oil, we chunguza tu utaona watu wana ruka ile oil com wanaenda pale lake oil sanene kupanga folen.
mi nshalizwa si chini ya mara tatu maana naishi jirani na hapo.
 
Shell ni kampuni la mafuta la kiitaliano, lilikuwa na vituo vingi vya mafuta nchini kiasi kwamba watu wakahisi vituo vya mafuta vinaitwa shell. Kwa sasa sijui kama wana tena vituo hapa nchini ila wanauza vilainishi.

Walishafungasha Virago hapa, nimewakuta Uganda.
 
Bodaboda na washikaji zangu pale Rose Hill ndiobwalinitonya juu ya Oilcom Segwrea kuwa wadokozi wa mafuta.
sawa na Camel pale Sanene jirani na kwetu pazuri,,the same drama....udokozi japo nasikia hivi karibuni wamejirekebisha.

LakeOil nasikia si wadokoZI,MAHILI ILA WAZEMBE NA WAVIVU, JUZI NIMEKWAZIKA KWA UJINGA WA DADA MUHUDUMU
 
Point of correction.

hakuna eneo la kijiografia au la kiutawala linaloitwa Tabata Segerea.
Tabata ni Tabata, Segerea ni Segerea.

Kata ya Tabata, Kata Ya Segerea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom