Habari wadau? Sikumbuki kama mada ya aina hii imewahi kutoka. Ila Kama Bado, nataka kuchangia na wadau kwamba, historia ya dunia tangu kuumbwa kwa ulimwengu, mtu wa karibu amekuwa akitajwa sana katika kuua, kukwamisha mambo, kusaliti, kulipa kisasi n.k.
Mifano; Adamu alisalitiwa na mkewe, Hawa. Samsoni aliingizwa chaka na demu wake, Delila. Yuda 'alimuuza' Yesu. Kaini alimuua Abeli. Lusifa alitaka kumpindua Mungu wake. Yakobo alimzunguka kaka yake, Esau kuhusu mbaraka wa baba yao, Isaka.
Marehemu Indira Gandi (alikuwa waziri mkuu wa India), aliuawa na walinzi wake. Laurent Kabila (alikuwa Rais wa DR Congo), aliuawa na walinzi wake. Wajane wengi wanadhulumiwa mali na mashemeji zao. Wanaofukuzwa makazini wanachongewa na watu wa karibu yao.
Kikubwa, historia inaonesha kwamba mtu wa karibu yako ni wa kuchukua tahadhari sana. Hata mke au mume husalitiwa na wa ubavuni mwake. Weka mifano mingine ya wazi.
Sent using Jamii Forums mobile app